12 Imani Za Homa Ya Korona Zafafanuliwa!: Imani Unazo Paswa Kujua

12 Imani Za Homa Ya Korona Zafafanuliwa!: Imani Unazo Paswa Kujua

Katika wakati wa dharura, kuna imani nyingi ambazo huenezwa kuhusu jambo linalo tendeka. Makala haya yana angazia imani tofauti kuhusu homa ya korona na iwapo ni kweli ama la.

Sio kila mtu katika nchi ya Nigeria angesahau kuzuka kwa Ebola na drama zilizofuata kama vile watu kuoga saa sita usiku na chumvi. Ni jambo la kawaida sana kwa visasili kadhaa kufuata magonjwa ambayo yanazuka. Katika makala haya tutaangazia imani zilizoko za homa ya korona, na kama kuna ukweli ndani yake au la.

12 Imani zisizo za ukweli unazo paswa kujua

Katika makala haya, tunataka kufafanua kwamba COVID-19 (homa ya Korona) ni jina la ugonjwa huu. Ilhali SARS-Cov-2 ni jina la virusi ambavyo husababisha ugonjwa huu.

Visasili hujitokeza pale ambapo watu wana uoga; uoga huu husababishwa na ujumbe ambao hatuufahamu. Hii husababisha kuenea kwa uoga zaidi au kufanya mambo yawe mabaya kushinda vile yalivyokuwa hapo awali. Katika wakati huu wa mtandao wa kijamii, kinacho hitajika ili kueneza uoga ni machapisho kadhaa katika mtandao, baada ya hapo wanawasiliana na wapendanao ambao hawako mtandaoni ili kuwajulisha kuhusu chapisho lile. Makala haya yatakusaidia ili  tofautisha ukweli na uongo wa imani za homa ya korona.

coronavirus myths

Picha: Pixabay

 • Barakoa za uso/ mask za uso zinaweza kulinda

Sio tu barakoa hizi za uso ambazo watu wanaharikisha kununua katika maduka ya kienyeji ya dawa ambazo zitakusaidia kujikinga kutokana na homa ya korona. Walakini, barakoa hizi ni muhimu sana kwa wale ambao tayari wana virusi hivi. Inazuia kuenea kwa virusi hivi kwa kuziba matone yoyote ya upumuzi kutoka kwa midomo yao. Lakini lazima uhakikishe kwamba umetilia maanani vitendo ya kiafya kama vile kuoga mikono na mengine mengi.

 • Una uwezekano mdogo wa kupata homa ya korona ikilinganishwa na mafua

Kisasili kingine ambacho lazima kilainishwe ni kile ambacho watu wanaamini kwamba mtu naa uwezekano wa kupatwa na homa ya korona ikilinganishwa na mafua. Huu sio ukweli. Wanasayansi wameangazia jinsi ambavyo virusi hivi vinaenea kwa kuhesabu kiwango cha kawaida cha uzaaji. Homa ya korona inakadiriwa kuwa katika kiwango cha 2.2, kumaanisha kwamba mtu mmoja anaeza kuathiri wastani ya watu 2.2. Homa hii iko katika kiwango cha 1.3.

 • Virusi hivi ni aina nyingine ya homa ya kawaida 

Mjadala kuhusu homa ya Korona kuwa umba lingine la homa ni kisasili tu. Homa ya korona inatokana na familia kubwa ya virusi ambayo huhusisha magonjwa mengine mengi. Ilhali SARS-Cov-2 haifanani na homa ya Korona, haitumii binadamu kama majeshi ya msingi kamahoma ya Korona.

 • Virusi hivi vilitengenezewa kwenye maabara

Kuna nadharia ya njama ambayo imekua ikienea kwamba virusi hivi vilitengenezwa katika maabara kwa makusudi kwa lengo la kuathiri watu na virusi hivi. Hili sio jambo la ukweli. Hakuna ushahidi unaounga mkono nadharia hii. Walakini, homa hii ina tabia zinazofanana na homa zingine za asili ambazo zimetoka kwa popo na kufikia binadamu katika miongo ya hivi karibuni.

coronavirus myths

 • Kuambukizwa homa ya korona kuna maana utakufa

Kuna ujumbe ambao umesababisha hofu ambayo imekuwa ikienea kwamba kuathirika na homa ya Korona ni hukumu ya kifo. Huu sio ukweli. Kulingana na utafiti wa Kikao cha China cha kudhibiti ugonjwa, asilimia ya watu 81 ambao wameathirika na homa ya Korona wana kesi kali za COVID-19. Hivi kwa urahisi inamaanisha kwamba watu ambao wameaga dunia kutoka na homa hii mpaka sasa kwa wingi walikuwa wameathirika na ugonjwa mwingine au ni wazee.

 • Uwezekano Wanyama wa Nyumbani Kueneza Virusi

Hakuna ushahidi ambao unaoonyesha kwamba mnyama anaweza kuathiri na virusi hivi.Wataalam hawana uhakika kwamba paka na mbwa wanaweza athirika na virusi hivi na pia kuueneza kwa binadamu. Katika mji wa Hongkong, mbwa alionyesha matokeo ya chanya dhaifu kutokana na virusi hivi, lakini wataalam hawana uhakika kama mbwa huyu alithirika kutokana na uso ulikuwa na virusi hivi. Mbwa huyu alipelekwa katika karantini lakini hakupatikana na dalili zozote. Kuwa salama, osha mikono yako na sabuni na maji baada ya kushika wanyama hawa.

coronavirus myths

 • Kufungwa kwa mashule ni jambo lisilo epukika

Katika kuzuka kwa ugonjwa huu, wakuu  wa afya walifunga shule zote kwa muda ili kuzuia kesi zingine za homa ya korona. Jambo hili limefanyika hapo awali na linaweza fanyika tena. Ingawa homa ya Korona ina dalili tofauti, kuenea na kipindi cha kupevuka, jua kwamba shule zitafungwa kuzuka kwa ugonjwa huu kukuendelea.

 • Watoto hawawezi ugua homa ya korona

Tofauti na imani hii maarufu,hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba watoto hawaezi shikwa na ugonjwa huu. Watoto wanaweza shikwa na homa ya Korona, lakini kuna ujumbe wa hapo awali ambao amabao unaonyesha kwamba watu wazee wana uuwezekano wa kukabiliwa na ugonjwa huu wakilinganishwa na watoto. Walakini, watoto wanaonyesha dalili kiasi, kumaanisha wanaweza eneza dalili hizi bila kuonyesha dalili zozote wenyewe.

 • Utajua ukapo athirika na homa ya korona

Huu sio ukweli. Watu ambao wamethirika na homa ya Korona wanaonyesha dalili nyingi ambazo zinafanana na dalili za magonjwa ya kupumua. Dalili hizi ni kama vile: kukohoa, joto mwilini, shida ya kupumua, kusunzi, kutapika na mafua. Hii huifanya kazi ya kugundua ugonjwa ngumu. Kama unaashi katika maeneo ambayo imethirika na una dalili hizi, temebelea daktari.

 • Homa ya korona ina athari chache ikilinganishwa na homa

Kulingana na ushahidi kwa hivi sasa, homa ya Korona ina madhara kushinda  mafua. Ikilinganishwa na mafua, utafiti wa hivi karibuni unaonyesha homa ya Korona katika kiwango cha asilimia 2.3, kiwango cha kifo ambacho ambacho kiko mara ishirini juu kushinda mafua.

 • Sio salama kupokea kifurushi kutoka Uchina

Kuna mjadala kwamba ukipokea kifurushi kutoka China unaweza athirika na virusi hivi, sio ukweli. Kulingana na Shirika la afya duniani(WHO), vifurushi au barua kutoka china ni salama. Utafiti umeonyesha kwamba virusi hiviishi kwa muda mrefu katika barua na vifurushi.

imani za homa ya korona

 • Hauna uhuru wa kula vyakula vya Uchina

Unaweza kula vyakula vya kichina katika nchi ya Nigeria bila hofu ya kushikwa na virusi hivi. Virusi hivi vinaweza kuwa asili yake ni China lakini haimaanishi kwamba virusi hivi vimo ndani ya kila kitu kinachohusishwa na nchi hii.

Kwa jumla,endelea kujikinga kwa kuosha mikono mara kwa mara na kwa makini, punguza upatano wa uso kwa uso na mikusanyiko. Kama una dalili za mafua na hauna uhakika, tafuta matibabu haraka.

Soma pia: The Effect of Good Sanitation Practices On Public Health

ChanzoLive Science, WHO

Originally written by Lydia Ume

Translated by Risper Nyakio

Je, ni imani zingine zipi zisizo za ukweli ambazo umesikia kuhusu homa ya korona? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa!

 

Written by

Risper Nyakio