Kupoteza mimba huathiri hisia, mawazo na fizikia ya mwanamke. Itachukua muda kabla ya kupona na kurejelea maisha yake ya hapo awali. Kupona kifizikia hulingana na umri wa mimba aliyopoteza. Muda wa kupona hutofautiana kati ya wanawake. Huku wengine wakichukua wiki chache kupona, wengine huenda ikawachukua miezi ama miaka kupona. Ni muhimu kwa mama kuchukua muda kupona kufuatia kupoteza mimba. Kutofanya hivi kutakuwa na athari hasi baadaye maishani mwake. Tazama afya baada ya kupoteza mimba na njia kumi za kupona baada ya kupoteza mimba kifizikia na kihisia.
Njia za kupona baada ya kupoteza mimba

Kuponya mwili wako baada ya kuharibika kwa mimba
Pumzika vya kutosha. Hasa katika masaa ya kwanza 24 hadi 48 baada ya kuharibika kwa mimba. Mwili wako unahitaji kupumzika. Mapumziko ni muhimu kwa uponaji. Hata kama unahisi sio muhimu, ni lazima upumzike.
Chukua temprecha yako kila jioni kwa siku 5 zijazo. Kuharibika kwa mimba huambatana na joto jingi na ni vyema kuwa tayari kuidhibiti unapougua.
Huenda ukawa unatokwa na damu sawa na hedhi. Kwa siku chache zijazo, nafasi kubwa ni kuwa huenda ikawa utakuwa unatokwa na damu kiasi cha unapokuwa na hedhi. Tumia pedi na wala sio tampons katika kipindi hiki ili kupunguza nafasi za kupata maambukizi. Kunywa maji tosha kisha ule matunda na mboga za kijani kwa wingi.
Epuka kufanya mapenzi hadi kutokwa na damu kuishe. Usirejelee kufanya tendo la ndoa kabla ya damu kukoma kutoka.
Fanya masi kwenye tumbo. Baada ya kupoteza mimba, huenda ukawa unahisi uchungu mwingi kwenye tumbo, ipige masi ili kusaidia uterasi kurejelea hali yake ya awali.
Kuponya akili yako baada ya kupoteza mimba

Jipe wakati wa kuomboleza. Hauwezi epuka kuomboleza baada ya kupoteza mimba. Ni muhimu kwa afya yako ya kihisia. Jipe wakati tosha kupitia hatua zote za kuomboleza.
Zungumza na mtu. Usikimye na kujiwekea yanayo endelea. Sema unachohisi na unachokipitia kwa watu walio karibu nawe. Zungumza na mchumba wako, yeye pia anaomboleza kilicho wapata.
Usijilaumu. Kuharibika kwa mimba sio hatia yako, wala ni kufuatia matatizo ya kimatibabu. Kubali kilichofanyika kisha uwe tayari kuendelea na maisha yako.
Usiwe na mawazo mengi. Baada ya kupoteza mimba, homoni zako haziko sawa na itachukua muda kabla ya kurejelea kawaida. Homoni zinazo badilika zitakufanya uhisi unakasirika ovyo na hutaki kuwa kati ya watu. Jaribu kutembea na kufanya mazoezi. Unaweza anza kwa kutembea kwa dakika chache kwa siku.
Chukua dawa za afya yako ya kiakili. Iwapo mama amefilisika zaidi kimawazo kufuatia kilicho wakumba, daktari huenda akashauri kuchukua dawa za anti-depressants kurejesha afya baada ya kupoteza mimba.
Itachukua kati ya siku chache hadi miezi kadhaa kwa mwili wako kupona kifizikia na kiakili baada ya kupoteza mimba. Usiwe na mbio ya kupona, upe mwili wako muda tosha upone vya kutosha kabla ya kurejelea juhudi za kujaribu kupata mimba tena.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Jinsi ya Kudhibitisha Ishara za Kupoteza kwa Mimba Baada ya Wiki Mbili