Njia Tano Za Kukaa Na Afya Katika Kazi Ya Dawati

Njia Tano Za Kukaa Na Afya Katika Kazi Ya Dawati
Je, nitawezaje kudumisha afya katika kazi ya dawati? Mfanyakazi wa kawaida atachukua muda mrefu kufanya kazi kwa dawati. Lakini asimilia kubwa ya watu wanaofanya kazi kwa dawati hupatwa na shida za kusimama ambazo huwa ni shida ya mgongo na shingo.Watakuwa na uwezo mkubwa wa kushikwa na maumivu ya kichwa, ambazo katika kesi zingine inaweza sababisha ukosefu wa umakinifu, na upungufu wa mazao katika kazi yako.

kudumisha afya katika kazi ya ofisi

jinsi ya kudumisha afya katika kazi ya dawati

Sote twahitaji tabia nzuri ili kukaa na afya njema katika kazi ya dawati

Je, utazuia vipi shida hizi zinazo husishwa na kufanya kazi kwa dawati? Jibu ni kwa kirahisi, kujifunza tabia za kiafya. Tabia hizi ni kama vile:

  • Kuyanywa maji mengi

Huenda likawa jambo lisilo la kawaida kuwa jambo hili ni mojawapo ya njia bora zaidi unapo fanya kazi kwa dawati ama kwa ofisi. Maji yanahusiana kivipi na tabia za kikazi?

Lakini fikiria kwa umakini jinsi ambavyo unavyo hisi vibaya unapo kosa maji wakati unafanya kazi.

Sio tu muhimu kunywa maji mengi iwezekanavyo unapofanya kazi, ila tabia hii inaongezeka baada ya kunywa maji siku kadhaa.

Tumia chupa ambayo inaweza tumika mara nyingi inayochukua maji mengi. Eka chupa hii karibu na dawati yako ya kufanya kazi na uhakikishe kwamba umefinika vizuri ili kuzuia maji kumwagika katika vifaa vyako vya stima.

  • Hakikisha umekaa wima

Ni jambo la kawaida kupatana na mja anayefanya kazi kwa dawati anayeteta kuhusu kuumwa na mgongo, uchungu wa shingo na kutokaa vizuri.

Chanzo kuu cha kutokaa vyema ni kutokaa wima. Kwa shukrani njema za ukuaji wa kiteknolojia, kazi zingine za kukaa zimeunda aina ya viti na meza ambazo zitasaidia uti wa mgongo na kuzuia shida za shingo.

dumisha afya katika kazi ya dawati

  • Tumia kompyuta yako vizuri

Ngoja! Kuinama unapotumia kompyuta yako. Ila, Keti wima na kisha uhakikishe kwamba macho yako yamo katika pembe inayofaa na kompyuta yako.

Kuna vifaa vinavyosaidia kusimamisha kompyuta, ili kuweza kukaa katika pembe inayofaa mbali na macho yako kidogo kama ulivyoshauriwa na mtaalam.

Nunua kifaa cha kusimamisha kompyuta yako ili uweze kuaga shida za mgongo na shingo kwaheri.

Sahau kuhusu mwendo wa muda mrefu

  • Chukua mapumziko madogo

Ni salama kusema kwamba wafanyakazi wengi hawana mwili sawa. Wengi wao watamaliza wakiwa wameketi katika madawati yao kwa muda wa masaa mengi kwa siku moja. Maisha haya yatasababisha ukosefu wa usawa mwilini. Watu ambao hawana afya lakini itaadhiri ufanyakazi wa akili na kusababisha kufanya kazi polepole.

Kwa kuchukua muda kidogo wa kupumzika unapofanya kazi, unaipa akili yako fursa ya kuhisi utulivu ata baada ya kupatiwa tarehe za kukamilisha kazi fulani.

kudumisha afya katika kazi ya dawati

  • Fanya mazoezi baada ya muda

Kwa kuketi katika dawati kwa masaa mengi kwa siku, wakati mwingine kwa wiki, ni rahisi kuwa na ukosefu wa usawa mwilini.

Jaribu kujinyoosha baada ya nusu saa. Nyoosha vidole vyako, mikono, shingo kiuno na miguu yako.

Kama pia unapenda, wataalam wakiafya wanashauri utembee kidogo ndani ya ofisi. Kwa kufanya hivi, unasaidia damu iwe na mtiririko mzuri na pia mwili wako uweze kufanya kazi vizuri.

This article was republished with permission from TheCable.

Written by

Risper Nyakio