Simu Za Rununu Zinaweza Athiri Afya Ya Akili Wa Watoto Wa Umri Ya Miaka Miwili

Simu Za Rununu Zinaweza Athiri Afya Ya Akili Wa Watoto Wa Umri Ya Miaka Miwili

Wazazi, wacha kungoja simu ikulelee mtoto, itasababisha madhara mengi kwenye watoto wako!

Kama mzazi, ni kweli kuwa baadhi ya mara, mimi huwapa watoto wangu simu wacheze nayo ama watazame runinga. Mara nyingi ninapo taka kufanya kazi ama nina mkutano na nataka kuwa na nafasi ya kufanya kazi bila kelele nyingi. Lakini je, jambo hili ni sawa kwa afya ya akili ya watoto wachanga?

Ni vigumu kukaa mbali na teknolojia  kwani watoto watoto wetu wana patana nazo kila mara.

Hata shule hutumia vifaa vya elektroniki kufunza wanafunzi na kuwapa kazi za ziada.

Afya ya akili ya watoto wachanga

Kutumia masaa mengi kwenye simu na vifaa vya elektroniki mara nyingi kume husishwa na kuathiri afya yetu ya akili. Utafiti mpya una sema kuwa hatari huenda ikaanza kwa watumiaji wachanga kama watoto wa miaka miwili.

Baada ya lisaa limoja la kutazama televisheni, watoto na watu wazima huenda wakawa hawana hamu ya kuuliza maswali, viwango vya chini ya kudhibiti hisia, kuto jiamini ambako kunaweza sababisha viwango vya juu vya fikira nyingi na kuwa na shaka wakati wote kulingana na utafiti ulio chapishwa na US kwenye jarida la Preventive Medicine Reports.

Watafiti walipata kuwa walio kuwa na umri wa miaka 14-17 wako katika hatari zaidi, lakini wakagundua tatizo hili katika watu wachanga na watoto wadogo, ambao akili zao bado zinakua.

mental health in young kids

walio na umri wa miaka 14 hadi 17 year wana hatari zaidi | Chanzo: Pixabay

Hatari fiche

Utafiti ulipata kuwa watoto wa shule ya chekechea walio tumia runinga mara kwa mara walikuwa katika hatari mara mbili ya kukasirika ovyo.

Pia ilionyesha kuwa asilimia 9 ya walio na umri wa miaka kati ya 11 hadi 13 walio tumia lisaa limoja kwa siku kwenye runinga zao hawakuwa na hamu ya kusoma mambo mapya, idadi iliyo ongezeka hadi asilimia 22.6 kwa wale ambao walitumia masaa saba kwa siku ama zaidi.

Waandishi Professa Jean Twenge, wa Chuo Kikuu cha San Diego, na Professa Keith Campbell, wa Chuo Kikuu cha Georgia, alisema: “Nusu ya magonjwa ya akili huibuka watu wangali katika miaka midogo kutoka miaka 15.

Kwa hivyo kuna haja kuu ya kudhibitisha sababu zinazo husika na matatizo ya afya ya akili ambazo zinaweza kusuluhishwa katika umri huo kwani kuna umri ambao ni vigumu kusaidia.

Kuwahimiza wazazi na walimu wapunguze wakati ambao watoto wanatumia kwenye mtandao, kucheza video ama kutazama runinga ili kuepuka hili.

Shirka la National Institute of Health linasema kuwa watu wachanga wanatumia wastani wa masaa 5 hadi 7 kwenye runinga katika wakati wao wa ziada.

Kipi ambacho tunaweza fanya kukomesha kuathirika kwa afya ya akili ya watoto?

Hapa kuna vidokezo ambavyo wazazi wanaweza fuata wakati ambapo watoto wao wanatumia vifaa vya elektroniki. Ni lazima kwa wazazi kufuatilia wakati ambao watoto wao wanatumia kwenye vifaa hivi.

 1. Tenga wakati wa kutizama runinga
  Ni vigumu kuepuka wakati wa kutizama runinga asilimia 100, kwa hivyo punguza wakati ambao watoto wako wanatumia kwenye vifaa vya elektroniki. Usiwakubalishe kuvitumia wakati ukiisha na upunguze wakati wanao tizama runinga.
 2. Wahamasishe wakacheze nje
  Wahamize watoto wako kucheza nje na marafiki zao na wadogo wao ili wafahamu jinsi ya kuingiliana na kuzungumza na watoto wengine. Ni vyema zaidi kucheza na wanyama wa nyumbani kama mbwa na paka na watoto wengine badala ya kutizama programu za wanyama.
  afya ya akili ya watoto
 3. Wape kazi zingine ama uwahusishe katika vitendo tofauti
  Sio wazo la busara kuwaweka watoto wako wakiwa kwenye vifaa vya elektroniki ili ufanya kile ambacho unataka kwa amani. Badala yake, hakikisha kuwa wana vidoli vya kucheza, vitabu vya hadithi, ama vitabu vya kupaka rangi.
 4. Hakikisha watoto wako wanapata usingizi tosha
  Watoto lazima wapate usingizi tosha kwa angalau masaa kumi kwa siku. Usingizi mzuri unasaidia kupona kutokana na kutaabika kwa macho na kwa akili kufanya kazi vizuri. Usingizi mzuri ni muhimu kwa afya bora.

Chanzo: Time

Soma pia: Jinsi Ya Kuwasaidia Watoto Waanze Kuongea Kwa Ufasaha

Written by

Risper Nyakio