Afya ya Meno: Vidokezo Muhimu Vya Kuzingatia Katika Janga Hili La Corona

Afya ya Meno: Vidokezo Muhimu Vya Kuzingatia Katika Janga Hili La Corona

Kwani hauna ofisi ya kwenda ama watoto wa kuepeleka shuleni, huenda kukawa na uwezekano wa afya ya mdomo kutupiliwa mbali katika shughuli za siku kwa siku. Inayo maana kuwa huenda ukakosa kusugua meno kama ilivyo kawaida. Dr. Tomisin Otolorin Oloko, daktari wa meno aliye na hisa katika Afya ya Meno Ya Mapambo na Implantology ana tupea vidokezo muhimu vya kuzingatia afya njema ya meno katika janga hili la corona na lockdown.

oral hygiene

Picha: Unsplash

Afya Ya Meno Kwa Watoto

Wazazi na wanao chunga watoto wana kazi ya kuwasaidia watoto kukuza afya yao ya mdomo na kuzingatia afya yao ya mdomo. Lengo lao ni kuelewa “mbona”.

  • Kwa nini wanapaswa kusugua meno kwa kutumia dawa ya meno iliyo na madini ya flouride? Kwa sababu inasaidia kuepuka kupata mashimo kwenye meno na kuyafanya yawe na nguvu zaidi.
  • Kwa nini unahitajika kusugua meno mara mbili kwa siku kwa angalau dakika mbili?  Kusugua meno mara mbili kwa siku kuna kusaidia kuepuka janga la kupata viini vinavyo sababisha meno kuoza na kufanya meno yapate mashimo; iwapo kusugua meno kwa dakika 2 ni wakati wa wastani unao hitajika kusafisha sehemu zote za meno na kusafisha ulimi. Tusisahau kusuuza kati ya meno, wakati wa juu, ila inahitajika kwa sana.
  • Kwa nini wanapaswa kusafisha ndimi zao?Ili kutoa harufu mbaya inayo sababisha viini vinavyo sababisha harufu mbaya (halitosis).
  • Kwa nini hawapaswi kula kitu chochote mbali na maji baada ya kusugua meno wakati wa usiku kabla ya kulala? Ili janga la viini lisimpate wakati wa usiku.

Nafikiria wanapo elewa sababu kwa nini, watahimizwa na wana jitolea kutunza meno na midomo yao kwa ujumla.

Kwa kuyasema hayo, mazungumzo yana tegemea na umri na watoto wanao angaliwa hadi wanapo fikisha umri wa miaka 8.

Pia, jaribu kufanya liwe jambo la kufurahia kwao, kusugua meno hakupaswi kuwa la kuboeka. Kucheza hivi kunasaidia sana, hasa kwa watoto wa umri mdogo. Kwa mfano, mtoto mdogo atafurahikia kuimba kwa nini na jinsi ya kusugua meno yao. Watoto walio na umri mkubwa kidogo huenda wakafurahikia wakati mwema wa dakika mbili unaofanana na glasi ya nusu saa.

Wazazi wanapaswa kutumia zaidi wakati wanao pata wa kuwa na watoto wao katika kipindi hiki kwa kuwasimamia wanapo sugua meno, kufanya afya ya meno na masomo yawe ya kufurahisha na pia kuangalia wanapo fanya kazi za kinyumbani.

oral hygiene

Picha: Pexels

Huduma za afya ya meno katika janga la Covid-19

Haja ya kutembelea kliniki ya meno wakati huu wa janga hili lazima iwe ni ya dharura. Iwapo sio ya dharura, tafadhali baki nyumbani na uongee na daktari wako wa meno kwa kutumia simu ili upate ushauri.

Na kama ni jambo la dharura, unashauriwa kuwasiliana na daktari wako wa meno iwapo unaweza kabla ya kwende kwenye kliniki. Huku kutamkubalisha daktari wa meno kufanya uamuzi na kufanya mipango inayofaa kabla ufike kwenye kliniki.

Mtoto anapaswa kupelekwa na mtu mmoja mzima na wote hawa wawili wanapaswa kuzingatia tahadhari za kuepuka kupata maambukizi ya homa ya corona kama vile kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji ama mitakasio.

Visa vyote ambavyo sio vya dharura na michakato imeahirishwa mpaka mambo yatakapo rudi kawaida.

Katika wakati huu, kliniki nyingi za afya ya meno zinahudumia visa vya dharura tu. Na iwapo lazima umwona daktari, fahamu kuwa wataalum wa afya na wafanyakazi wengine wanachukua hatua mwafaka kukulinda na kuwalinda katika janga hili. Kwa mfano, kuwapima wagonjwa iwapo wame tembea ama wana dalili, kwa kutumia vifaa vya kujilinda, na bado kuhakikisha kuwa wanafuata maagizo yaliopewa kuthibiti virusi hivi, kuosha na kutoa maambukizi kwa sehemu za umma mara kwa mara kwa vitu kama milango, viti ama vyumba vya kujisaidia vinavyotumika kwa sana.

Iwapo sio jambo la dharura, wagonjwa wote wanashauriwa kubaki nyumbani na kuwapigia madaktari wao wa meno ili wapate ushauri mahitaji yakitukia.

oral hygiene

Picha: Unsplash

Kwa mtu yeyote ambaye angependa jino lake lijazwe, mojawapo kati ya sababu ambazo fillings za meno hutoka kwa ghafla ni kufuatia kuuma vyakula vilivyo vigumu zaidi. Na katika sehemu ya dunia, kuuma mifupa huwa miongoni mwa sababu kuu. Kwa hivyo, huenda ukataka kukaa mbali na kuuma vitu vigumu ili kuepuka kumtembelea daktari wa meno.

Soma pia:

The Correct Guide To Brushing Your Teeth The Right Way

Top 5 Dentists in Lagos: All You Need To Know About These Dental Clinics

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Syreeta Akinyede na kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio