Afya Ya Ujauzito: Mambo Unayo Paswa Na Usiyo Paswa Kufanya!

Afya Ya Ujauzito: Mambo Unayo Paswa Na Usiyo Paswa Kufanya!

Kutunza mtoto hakuanzi anapo zaliwa, mbali angali tumboni mwa mama na mjamzito ana shauriwa kuwa mwangalifu wa afya yake.

Kutunza mtoto hakuanzi anapo zaliwa, mbali angali tumboni mwa mama. Hii ndiyo sababu kwa nini mama mjamzito ana shauriwa kuwa mwangalifu wa afya yake na mtindo wa maisha wake katika kipindi hiki. Orodha yetu ya afya ya ujauzito na mambo ambayo mama anapaswa na asiyo paswa kufanya yata kuelimisha zaidi kuhusu vitu muhimu unapo kuwa katika safari yako ya ujauzito.

Afya ya ujauzito: Mambo ya kutofanya ukiwa na mimba

afya ya ujauzito

  1. Usinywe pombe

Pombe ina mwathiri mtoto kwa njia hasi, hasa katika ukuaji na maendeleo yake akiwa tumboni na hata baada ya kuzaliwa. Athari sugu za pombe kwa mtoto ni kusababisha kifo chake akiwa tumbo ama hata kuwa na matatizo ya kimaumbile baada ya kuzaliwa.

2. Usivute sigara

Moshi ya sigara ni hatari kwa mtoto kwani huenda mtoto akazaliwa akiwa na matatizo ya kimwili, kutatizika kusoma ama kuwa na uzito mdogo wa mwili. Kulingana na utafiti, watoto walio zaliwa kwa mama aliye vuta sigara akiwa na mimba, huenda wakaanza kuvuta sigara pia wangali wachanga.

3. Usinywe kafeini nyingi

Kafeini huongeza mpigo wa moyo wa mtoto.

4. Usiketi kwa sauna ama hot tub

Joto jingi iliyoko kwenye sauna huenda ikawa hatari sana kwa mama mjamzito. Epuka kutumia hizi katika trimesta yako ya kwanza ya mimba kwani huenda ukaongeza hatari yako ya kupoteza mimba.

Afya ya ujauzito: Mambo unayo paswa kufanya

  1. Chukua tembe za vitamini

Usichukue tembe za vitamini badala ya chakula halisi. Hakikisha kuwa unakula lishe yenye afya ili mwili wako upate virutubisho bora na tosha ili kuegemeza ukuaji wa mtoto tumboni. Tembe za vitamini ni muhimu kukusaidia kufikisha kiwango cha vitamini mwili wako unahitaji kila siku. Hakikisha kuwa unachukua tembe za kalisi, iron na folic acid. Ni muhimu sana katika ukuaji wa kiinitete chako.

2. Fanya mazoezi

Afya Ya Ujauzito: Mambo Unayo Paswa Na Usiyo Paswa Kufanya!

Kufanya mazoezi kunasaidia mama mjamzito na mtoto anaye kua tumboni mwake. Unapofanya mazoezi katika mimba, una epuka kukosa usingizi usiku, uchungu wa misuli, kuongeza uzito mwingi na kudhibiti mhemko wa hisia.

3. Usingizi wa kutosha

Afya Ya Ujauzito: Mambo Unayo Paswa Na Usiyo Paswa Kufanya!Afya Ya Ujauzito: Mambo Unayo Paswa Na Usiyo Paswa Kufanya!

Mabadiliko mengi yana fanyika mwilini mwako katika kipindi hiki, kama vile kubadilika kwa viwango vya homoni mwilini, kuwa na wasiwasi na huenda ukakosa usingizi. Mimba ina hitaji nguvu nyingi, kwa hivyo hakikisha kuwa una lala vya kutosha kila siku. Una shauriwa kulenga kupata usingizi masaa kati ya 7-9 kila usiku.

4. Kufanya mapenzi

Kuna baadhi ya watu ambao huwa na uwoga kuwa kufanya mapenzi ukiwa na mimba haku ruhusiwi. Ikiwa ujauzito wako hauna matatizo yoyote, usione haya kufanya mapenzi na mchumba wako. Kumbuka kutumia mitindo isiyo shinikiza mama na yenye starehe kwake.

Kipindi cha mimba ni cha kusisimua sana hata ingawa kina panda shuka zake. Hakikisha kuwa una itunza afya yako katika kipindi hiki.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Dalili Za Mimba Ya Kiume: Jinsi Ya Kufahamu Jinsia Ya Mtoto Unaye Mtarajia

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio