Mama yeyote aliyepoteza mimba anafahamu kuwa kupoteza mtoto huwa na athari kubwa kwake. Huenda ikawa vigumu kwake kurejelea alivyokuwa hapo awali. Hasa kama alikuwa tayari kuwa mama. Uponaji baada ya kupoteza mimba sio rahisi. Tuna angazia afya ya mama baada ya kupoteza mimba na mambo muhimu kwake kufanya.
Fanya haya baada ya kupoteza mimba

- Zungumza na watu na usikae peke yako
Mama anapopoteza mimba, huhisi kana kwamba yeye ndiye wa kwanza kupitia hayo. Usihisi hivi. Ukweli ni kuwa, wanawake wengi hupoteza mimba. Tatizo huja mama asipozungumza na watu kuhusu kilichofanyika. Ikiwa hungependa watu wengine wajue, kuna vikundi kwenye mtandao ambapo watu huzungumzia haya.
- Kubali yaliyofanyika bila kujilaumu
Mara nyingi mama anapopoteza mimba, huhisi kana kwamba kuna kitu alichofanya kilichosababisha kuharibika kwa mimba yake. Ni muhimu kwa mama kuelewa kuwa kuharibika kwa mimba hutokea mwili wake usipoendana na mimba ile. Siyo lawama yake.
Positivity ni muhimu sana kwa mama baada ya kushuhudia kuharibika kwa mimba. Usiwasikize watu walio na mambo mengi ya kusema hasa ikiwa mambo hayo ni hasi. Mama anaweza jaribu kusikiza positive meditation kumsaidia kupona kihisia na kiakili.
- Usipuuze mahitaji yako ya kifizikia
Baada ya kuharibika kwa mimba, hisia za mama huathiriwa pakubwa. Huenda akasahau ama kupuuza mahitaji yake ya kifizikia. Mwili hubadilika sana baada ya kupoteza mimba. Ni vyema kwa mama kuitunza afya yake ya kifizikia kwa kufanya mazoezi. Usiusukume mwili wako sana, ikiwa hapo awali hukua unafanya mazoezi, anza kwa kufanya mazoezi mepesi. Pia, unaweza fanya kazi na mtaalum wa mazoezi.

Hata kama hutaki kuwajulisha watu kila kinachoendelea maishani mwako, ni vyema angalau kutaja kinachoendelea maishani mwako. Hata kuwajulisha watu tu kuwa umepoteza mimba na hungetaka kulizungumzia. Maneno haya yatawasaidia marafiki na familia yako kufahamu maneno wasiyopaswa kusema mbele yako.
- Angazia mahitaji yako ya kihisia
Ni sawa kuchukua mapumziko kutoka kazini cha majonzi baada ya kupoteza mimba. Usiendelee na maisha yako kana kwamba hakuna kilichofanyika. Chukua muda ili hisia zako zipone.
Zungumza na mtaalum unapokumbwa na hisia hasi na hata kukufanya ushindwe kutoka kitandani.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Kuharibika Kwa Mimba Na Umuhimu Wa Kusafisha Mji Wa Uzazi