Aina kumi ya wazazi ambao unaweza kuwapata nchini Kenya na sifa zao

Aina kumi ya wazazi ambao unaweza kuwapata nchini Kenya na sifa zao

Uzazi sio jambo rahisi. Kuna aina mbali mbali ya wazazi na wanatumia njia tofauti za ulezi. Baadhi ya wazazi utakao wapata nchini Kenya ni wale wa Mamlaka na pia wa waandishi.

Kuna aina tofauti za wazazi Kenya. Tuta angazia baadhi ya wazazi hawa na athari wanazo kuwa nazo kwa watoto wao. Mzazi bora anafaa kumpenda mtoto wake, kuwa mwandani wake na kujua mahali anapo weka mipaka na kumkanya mtoto wake anapo kosea.

Kuna Aina Tofauti za Wazazi Nchini Kenya

Aina Ya Wazazi Wa Mamlaka:

Hawa ni wazazi bora. Wana msimamo katika wanacho sema ila hawatumii njia 

kali za kuwaadhibu watoto wao na isio kali. Wako huru kuwa na mjadala na watoto wao. Wana funza watoto wao kuwa na uhusiano wa maana na watu wengine na adaptation skills. Wana wapenda watoto wao na panapo hitajika, wanawapa mapenzi kali panapo stahili. Watoto wao wanaweza kutangamana vyema na watu wengine katika jamii, wana weza kujitegemea, kuwapenda watu na huwa na uhusiano bora na watu wengine. Niko katika jamii hii ya wazazi.

Wa Andishi:

Hawa ni wazazi ambao wanapenda watoto kufanya mambo kuzingatia njia walio

wachagulia wenyewe. Hawa waruhusu kufanya wanachotaka ama kuwa na mjadala kuhusu jambo hili. Ni wazazi wa kuamuru na wana amini katika kuwaadhibu watoto wao wanapo kua.  Kwa mara nyingi, wana waadhibu watoto wao kwa kutegemea hisia zao ila si kwa kutumia mawazo na fikira zao. Wanapo hisi kuwa mtoto ametenda kosa na haja fanya jambo kulingana na jinsi wanayo ipendelea, wana mwadhibu. Kwa mara nyingi, watoto waliolelewa kwa njia hii, wana uoga mwingi, kuwa na usumbufu, na pia wana hasira nyingi maishani na pia kwa watu walio karibu na wao. Wanapo kuwa watu wazima na kubarikiwa na watoto, kwa mara nyingi wana kuwa kama wazazi walio walea, na kutumia njia ya kuadhibu watoto wao.

wazazi na kutumia mitandao

Aina Ya Wazazi Wa Kupuuza:

Hawa ni wazazi ambao hawana wasaa wa watoto na familia zao. Kabisa watoto wa

wazazi hawa hawajui inavyo hisi kupata mapenzi na ulinzi wa mzazi. Kwa maana wakati mwingi wazazi hawa wana yashughulikia mambo yao na hawa muda wa kuwa na watoto wao na kujuana. Wakati mwingine unapata kuwa wako kazini kutoka asubuhi hadi jioni. Majukumu ya kuwalea watoto wao wana mwachia mfanya kazi wao.  Pia hawa ni wazazi ambao wanapigana nyumbani. Hawana mapenzi kati yao wenyewe, na hasira wanazo kuwa nazo wanazitoa kupitia kwa watoto wao. Watoto walio na wazazi wa aina hii hawawezi kujieleza na hawana mtu wa kumkimbilia wanapo kua na matatizo maishani. Wanakosa ujasiri maishani na kuto jiamini.

Halali:

wazazi wa aina hii hawaweki mipaka yoyote ikija kwa watoto wao. Wana amini 

kuwa kumpa mtoto chochote kile anacho taka ni njia ya kuonyesha mapenzi yao. Kwa njia hii, wanataka kukubalika na watoto wao. Watoto hawa Wanaamini kuwa lazima wapate chochote wanachotaka hata wanapokua wakubwa. Wana ponyimwa wana kasirika.

Wabinafsi:

wazazi wa aina hii wana wafunza watoto wao kutimiza mahitaji yao. Badala ya

kuwa hapo watoto wanapo wahitaji, wanawafunza kuwa wanafaa kuwa hapo wazazi wao wanapo wahitaji. Pia kuwa wanafaa kuwaambia wanacho taka kuskia. Watoto wa aina hii wana mahitaji mengi na wanaonekana kupotea njia.

Kinga zaidi:

Wazazi wanao wapa watoto ulinzi zaidi, wana maanisha vyema kwa watoto ila 

Wanafuata fikira zao za kutokua salama. Wanaogopa matukio ya maisha na hawawakubalishi watoto wao kusoma kutoka kwa makosa yao. Watoto wanao kua kwa njia hii hawana ujasiri wa kupambana na matukio tofauti maishani.

Ubaguzi:

Hii ni mojawapo ya aina za wazazi wasio bora. Wazazi wawili hawakubaliani jinsi ya kuwalea watoto. Kwa hivyo wakati wote kuna

vita kati yao. Huenda watoto wakaskizana na mzazi anayefanya mambo ya kuwa furahisha na kumtenga huyo mwingine. 

Walio Jitenga:

Wazazi hawa wamejitenga na jamii na marafiki zao. Hawajui jinsi ya kutangamana

na watu wengine. Pia hawana mawasiliano mema kati ya wenyewe. Watoto wa wazazi hawa hawajui jinsi ya kuwasiliana na watu wengine.

Wategemezi:

Wazazi wa aina hii hawataki kutengana na watoto wao. Kwa hivyo wana funza

watoto wao kuwa tegemea wasaa wote. Wana wafunza watoto wao kukaa nyumbani na kuwapa fikira hasi kuhusu kuwa nje na kutangamana na watu wengine.  Watoto kutoka familia hizi hawajui kujitegemea katika lolote maishani.

Aina Ya Wazazi Sumu:

Hawa ni wazazi wasio faa hata kamwe. Kuna hadithi inayo simuliwa kuhusu mama aliye

onekana kumpenda kijana wake. Alikua anamsaidia kutafuta kazi na kupatana na watu tofauti. Ila alifanye hivi kwa kumvunja moyo. Kijana huyu alibaki kukosa ujasiri na kuwa mnyonge. Kwa mara nyingi wazazi hawa wanaonekana kuwa na uhusiano bora na watoto wao ila wazazi hawa hawana upendo unaofaa kutoka kwa wazazi.

Read Also: Funny Quiz: Dear Parent, Just How African Are You?

Written by

Risper Nyakio