Hadithi Za Kuadhibiwa Na Aina Za Adhabu Za Wanafunzi

Hadithi Za Kuadhibiwa Na Aina Za Adhabu Za Wanafunzi

Katika Nigeria, aina za adhabu za wanafunzi huenda mara  nyingi zikawa kali kuliko kitendo ambacho mtoto alifanya.

Je, wewe huwaadhibu watoto wako? Watu wengi huamini kuwa wazazi na walimu wasio waadhibu watoto walio tenda mabaya wanawaharibu. Adhabu kali ni kawaida manyumbani, shuleni na mashirika ya kidini. Watu wana amini kuwatia watoto adabu kwa njia hii wanasema kuwa huenda ikasaidia watoto kuwa na adabu. Katika Nigeria, aina za adhabu za wanafunzi huenda mara  nyingi zikawa kali kuliko kitendo ambacho mtoto alifanya. Mitandao imejazwa na hadithi za adhabu zilizo enda mrama.

types of punishments for students

Kabla tuangalie njia tofauti ambazo watu wenye wamamlaka wanatumia kuwaadhibu watoto shuleni, unapaswa kujua kuwa maana ya adhabu kali.

Hadithi za adhabu na aina zingine za adhabu kwa wanafunzi

Baraza la Uropa lina elezea adhabu kali kama adhabu yoyote ambapo nguvu za kifizikia zinatumika kusababisha uchungu ama kukosa starehe. Jina hili ni la ki-latin – limetoka kwa jina corpus lenye maana ya mwili. Kutumia adhabu za kifizikia kugeuza tabia za mtu sio jambo jipya. Watu wamekuwa wakifanya hivi kwa wakati mrefu sana.

Aina tofauti za adhabu za wanafunzi

Kupigwa sio aina ya adhabu kali zinazo tumika kulainisha tabia ya mtoto. Wakati ambapo adhabu ya mtoto ilianza kutokea kuhusu watoto kuchapwa hadi wakafa na walimu wao, watu walio na mamlaka shuleni wamelazimika kutafuta njia mbadala za kuwaadhibu wanafunzi bila kuwagusa.

Kwa ujumla, kuna baadhi ya njia ambazo watu wana waadhibu watoto:

  • Kurusha mateke
  • Kuwauma
  • Kuwatingiza
  • Kupiga kofi
  • Kugonga kwa kichwa
  • Kuwalazimisha wanafunzi kufanya mazoezi kwa muda mrefu
  • Kuwalazimisha watoto kukaa kwa nafasi za kuumiza mili yao
Kwa nini watoto huadhibiwa shuleni?

Kuchelewa

Kuto fanya kazi ya ziada kwa wakati unaofaa

Kupigana

Kuanguka darasani

Kuzurura shuleni

Kuanguka mitihani ama kupata alama za chini

Kuto waheshimu walimu ama watu wengine wa mamlaka

Kuvunja amri na masharti ya shule

Baadhi ya aina za adhabu za watoto katika shule tofauti

Katika shule tofauti, walimu na watu wengine wenye mamlaka wamekuwa wabunifu sana inapofika kuadhibu watoto. Kwani lengo ni kurekebisha na sio kua, aina ya adhabu shuleni huonyesha lengo hili. Hakuna shule ama mwalimu anayetaka kuwa kwenye habari kwa kumchapa mtoto hadi akamwua, kwa hivyo aina zingine za adhabu zisizo na uchungu mwingi zinatumika.

Hapa ni baadhi ya adhabu:

1. Kuosha vyoo

Vyoo vya umma vinajulikana kwa kuwa vichafu. Vyoo vya shule vina uchafu mwingi zaidi. Watoto wa shule baadhi ya wakati wanafanywa waoshe vyoo vichafu vya shule na baadaye walimu kuvikagua kuhakikisha ni visafi. Adhabu za kuosha vyoo huenda zikawa za hadi wiki moja.

2. Kupiga magoti na kuinua mikono
aina za adhabu za wanafunzi

Credit: Legit.ng

Kutoka kiwango cha shule ya msingi hadi ya sekondari, wanafunzi lazima wapige magoti kwa makosa kadha wa kadha. Kupiga magoti na kuinua mikono kwa muda mrefu huenda kukamfanya mwanafunzi kukosa usawa wa mwili, ambako kunaweza sababisha mtoto kusumbuka kutumia misuli kupata usawa wa mwili.

Ni kawaida kupata watoto wakihitimu kutoka ya shule ya sekondari huku wakiwa na alama nyeusi zinazo sababishwa na magoti yaliyo umia kufuatia miaka mingi ya kupiga magoti.

3. Kukata nyasi na kisu kisichokuwa na makali

Shule nyingi zina watu ambao jukumu lao ni kukata nyasi na kuangalia shamba za shule. Ila, inapofika wakati wa kulainisha mwanafunzi, walimu kwa mara nyingi huwapatia visu ama panga zisizo na makali. Wanafunzi wanapaswa kukata nyasi uwanjani.

4. Kuokota pini

aina za adhabu za wanafunzi

Kuokota pini ni aina ya adhabu kali, ila ni mojawapo ya adhabu zilizo maarufu sana shuleni. Mtoto lazima ainame na kuweka kidole chake kwenye sakafu na mwili kuwa laini na sakafu huku mguu mmoja ukiwa umeinuliwa nyuma yao.

Baadhi ya aina zingine za adhabu kwa wanafunzi shuleni

5. Kubeba dawati kichwani

Shuleni zinazo kuwa na adhabu kali zinajua jinsi ya kuwa nyamazisha wanafunzi wanao piga kelele darasani. Shule nyingi hushauri vitabu vingi vya kusoma, baadhi ya hizi huwa nzito sana hufanya adhabu hii kufanya kazi. Hii ni mojawapo ya adhabu ambazo wanafunzi huogopa zaidi. Kuwafanya wasimame wakiwa na dawati nzito vichwani huenda likafanya mtoto kunyamaza anapokuwa darasani.

6. Kukaa hewani

Kuchuchumaa hewani kuna umiza hata kwa wanao fanya mazoezi kila mara, ni kali zaidi kwa wanafunzi wanaokaa kwa jinsi hii kwa muda mrefu. Aina hii ya adhabu shuleni husababisha wanafunzi kuumwa na misuli. Wanafunzi wananyoosha mikono yao mbele ya mili yao kisha kuchuchumaa kana kwamba wanakaa hewani. Wanakaa hivi kwa muda mrefu.

7. Kuruka kama chura

Kuruka kama chura huwa maarufu inapofika wakati wa adhabu za nje shuleni. Wanafunzi wanalazamishwa kuchuchumaa kisha kuruka kana kwamba chura.

8. Kupiga kwa kutumia viboko ni mojawapo ya adhabu shuleni

Hapo awali kuwaadhibu watoto kwa kuwachapa kulipokuwa kunakubalika shuleni, walimu walikuwa wanatumia viboko, vijiti, viatu, mishipi, bomba, na kamba za kuanika nguo. Siku hizi, shule nyingi zimepiga marafuku aina hii ya adhabu kwa sababu watoto wamekufa kwa kuadhibiwa kwa njia hii.

Aina za adhabu za wanafunzi: Zipi zinazo kubalika na zisizo kubalika?

Baadhi ya nchi kama vile Sweden zimepiga marufuku adhabu kali nchini kote. Baadhi ya shule katika nchi ya Nigeria-hasa shule za kibinafsi – zimeonya walimu dhidi ya kuchapa watoto. Iwapo mtoto anafanya kitu kisicho kubalika kwenye masharti ya shule na utaratibu, wanaweza katazwa kufika shuleni kwa wiki chache.

Kuna ubaya mwingi wa adhabu kali. Baadhi ya athari hizi hasi huenda zika waathiri maishani mwao mote. Shule zinaweza tumia mbadala wa adhabu ambao hautasababisha uchungu wa kifizikia.

The Council of Europe

Naijagists.com 

Soma pia: Corporal punishment: should you spare the rod and spoil the child?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio