Mwanamke mjamzito huenda akapata anemia anapokuwa mjamzito. Kuna aina 3 za anemia katika mimba. Anapougua ugonjwa huu, damu yake haina seli nyekundu tosha za kusafirisha hewa kwa mtoto.
Mwili huzalisha damu zaidi katika ujauzito ili kutoa damu tosha kuegemeza ukuaji wa mtoto na kutosheleza mahitaji ya mama. Kutokuwa na chuma tosha mwilini kutaathiri kiwango cha seli nyekundu ambazo mwili unazalisha.
Ni kawaida kwa wanawake kuwa na anemia ya kiwango cha chini katika mimba. Anemia ya kiwango cha juu husababishwa na sababu tofauti. Humfanya mama kuhisi uchovu, kukosa nguvu na kumweka katika hatari ya kupoteza mimba isipotibiwa.
Aina za anemia katika mimba
Seli za damu nyekundu
- Anemia ya ukosefu wa chuma
- Anemia ya ukosefu wa vitamini B12
- Anemia ya ukosefu wa folate
Vyanzo vya aina hizi za anemia
- Anemia ya ukosefu wa vitamini B12
Mwili unahitaji vitamini B12 kutengeneza seli nyekundu zenye afya. Mwanamke mjamzito asipopata vitamini B12 tosha kutoka kwa liseh yake, mwili hauna uwezo wa kutengeneza seli nyekundu. Lishe isiyokuwa na nyama tosha, bidhaa za maziwa na mayai humweka mama mjamzito katika hatari ya kukosa vitamini B12. Mtoto ako katika hatari ya kupata kasoro za kuzaliwa ama kujifungua kabla ya wakati.
- Anemia ya ukosefu wa folate
Folate inapatikana kwenye mboga za kijani. Mwili unahitaji folate kutengeneza seli mpya ikiwemo seli nyekundu za damu. Kukosa folate tosha mwilini hufanya iwe vigumu kwa seli nyekundu za damu kupitisha hewa mwilini. Mwanamke anastahili kuchukua tembe za nyongeza za folate ili kufikisha kiwango tosha cha virutubisho hitajika.
- Anemia ya ukosefu wa chuma
Aina hii hufanyika mwili unapokosa chuma tosha ya kutengeneza hemoglobin ambayo ni protini ya seli za damu nyekundu. Zina jukumu la kusafirisha damu kwenye mapafu na mwili wote.
Wanake walio katika hatari ya kuugua anemia

- Walio na mimba ya zaidi ya mtoto mmoja
- Waliokuwa na anemia kabla ya kupata mimba
- Wasio kula vyakule vyenye chuma tosha
- Walio pata mimba wangali vijana
- Kupata mimba inayofuatana kwa karibu
- Wanaotatizika kutokana na ugonjwa wa asubuhi
Hatari za anemia katika mimba
- Kujifungua mtoto mwenye uzani wa chini zaidi
- Kujifungua mtoto mwenye anemia
- Kujifungua mtoto anayechelewa kukua
- Kutatizika kutokana na postpartum depression ama kusombwa na mawazo baada ya kujifungua
Matibabu ya anemia katika mimba
- Kuchukua vitamini za prenatal
- Kuchukua tembe za nyongeza za virutubisho vya vitamini B12
- Kula nyama, mayai na bidhaa za maziwa
- Kula mboga za kijani
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Athari 5 Hasi za Sukari Kwenye Afya