Tatizo La Upungufu Wa Damu Mwilini Baada Ya kujifungua

Tatizo La Upungufu Wa Damu Mwilini Baada Ya kujifungua

Hali ya anaemia mwilini baada ya kujifungua ni sawa na aina zingine za magonjwa. Na bila shaka hali hii inaweza tatuliwa.

Mama ako katika hatari ya kuugua kutokana na upungufu wa damu mwilini ama anaemia baada ya kujifungua. Hali inayo sababishwa na kukosa madini ya chuma tosha mwilini.

Vyanzo vya anaemia baada ya kujifungua

anaemia baada ya kujifungua

Mlo duni: Ulaji wa chakula kisicho na viwango tosha vya madini ya chuma baada ya kujifungua kuna husishwa na hali hii. Mama anahitaji madini ya chuma kwa siku ya viwango visivyo pungua 4.4 mg. Ikiwa mama anatatizika kufikisha kiwango hiki cha madini ya chuma kutokana na chakula, anaweza kutumia tembe za virutubisho. Zitakazo msaidia kufikisha viwango vinavyo hitajika. Ni vyema kuwasiliana na daktari katika kisa hiki.

Kupoteza damu wakati wa kujifungua: Mama hupoteza damu nyingi katika mchakato wa kujifungua. Na asipo kula chakula kilicho na madini tosha ya chuma kuregesha damu aliyo poteza, ako katika hatari ya kuugua hali ya anaemia.

Maradhi ya tumbo: Kuna maradhi ya tumbo la chakula kama vile uvimbe yanayo ongeza nafasi za kufyonzwa kwa madini ya chuma na hivi basi kusababisha upungufu wa idadi ya madini haya mwilini.

Dalili za anaemia baada ya kujifungua

  • Kuhisi uchovu mwingi wakati wote
  • Ngozi kuonekana imekauka
  • Kujihisi mnyonge
  • Maziwa ya mama kupungua na hivi basi mtoto kuwa na uzani wa chini
  • Maumivu ya kichwa
  • Upungufu wa hamu ya mapenzi

Fahamu kuwa anaemia ina athii unyonyeshaji. Mama huenda akashuhudia kupungukiwa na maziwa ya mama ama kukosa maziwa tosha mwilini. Na kusababisha mtoto kuwa na afya duni na kupunguza uzani wake.

Matibabu ya hali ya anaemia

kupata mtoto mrembo

Ili kurekebisha hali hii, mama anashauriwa kufanya mambo yafuatayo:

  • Tumia tembe za virutubisho vya madini ya chuma kuongea viwango vya chuma kwenye damu
  • Kula vyakula vinavyo saidia kuongeza madini ya chuma mwilini kama vile mchicha, matunda na mboga zingine za kijani
  • Vyakula vyenye vitamini C kama vile machungwa
  • Mtembelee daktari wako akutibu

Kumbuka kuwa hali ya anaemia mwilini baada ya kujifungua ni sawa na aina zingine za magonjwa. Na bila shaka hali hii inaweza tatuliwa. Usipoteze muda baada ya kugunduwa kuwa una kosa damu tosha mwilini. Unapo tibiwa mapema, utaepuka hali hii kukuzidia na kuwa sugu.

Chanzo: WebMd

Soma Pia:Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ukiwa Na Mimba

Written by

Risper Nyakio