Anemia ni hali ambapo damu mwilini huwa na upungufu wa seli nyekundu. Kuna baadhi ya wanawake wanaotatizika na hali ya anemia baada ya kujifungua. Inasababishwa na kupoteza na kupungukiwa na madini ya chuma baada ya kupata mtoto.
Dalili za anaemia baada ya kujifungua

- Kuhisi uchovu mwingi
- Kukauka ngozi
- Mpigo wa kasi wa moyo
- Kupunguka kwa hamu ya kufanya mapenzi
- Kukosa nguvu
- Kuumwa na kichwa
Vyanzo vya anemia baada ya kupata mtoto
Lishe duni: Lishe ni muhimu sana, sio wakati wa ujauzito tu, mbali hata baada ya kujifungua. Kukosa madini ya chuma tosha hupelekea katika mama kuugua tatizo la anemia. Kuna tembe za virutubisho zinazo msaidia mama kuchukua kiwango tosha cha anemia kutosheleza mahitaji ya mwili.
Kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua kunasababisha mwili kuwa na upungufu wa madini na kumfanya mama awe na hali ya anemia punde tu baada ya kujifungua.
Maradhi kwenye tumbo la chakula kama vile kufura huongeza ufyonzaji wa madini ya chuma. Kukosa madini ya chuma tosha mwilini hupelekea mama kuugua ugonjwa wa anemia.
Hatari za anemia isipotibiwa
- Kutatizika kufanya majukumu ya kila siku
- Hatari iliyoongezeka ya kujifungua mtoto njiti
- Kutatizika kujifungua
- Kizunguzungu na kuzirai
- Kifo cha ghafla
- Wanadada walio katika hatari ya kuugua hali ya anemia
- Wajawazito wa mimba ya mapacha ama zaidi
- Kujifungua kabla ya wakati
- Kupata mimba muda mfupi baada ya kujifungua
- Uzito mwingi wa mwili zaidi ya BMI 24
- Jifungua kupitia upasuaji wa C-section
- Walio na shinikizo kubwa la damu wakati wa mimba
Kutatua hali ya anemia baada ya kujifungua

Mama anapaswa kufanya mambo haya ili kutatua hali ya ukosefu wa seli nyekundu mwilini.
- Kutumia virutubisho vya madini yenye chuma kuongeza madini kwenye damu
- Kuhakikisha lishe ina vyakula vilivyo na wingi wa madini, kama vile mboga za kijani
- Kula lishe yenye vitamini C kama vile matunda hasa machungwa
- Pumzika vya kutosha
- Hakikisha unaenda kwenye kituo cha afya mapema kabla ya hali ya anemia baada ya kujifungua kuwa sugu.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Ishara 4 Zinazodhihirisha Kuwa Mama Ana Ujauzito Wenye Afya