Hongera! Anita Nderu na bwana yake Barret Raftery ndiyo wazazi wapya mjini! Anita Nderu na bwana yake wakaribisha mtoto wao wa kike.

Baada ya kutangaza ujauzito wao kwa njia ya kufana, Anita kupitia kwa kurasa yake ya mtandao wa kijamii ya Instagram, aliwajuza mashabiki wake kuwa walimkaribisha mtoto wao wa kike siku ya Ijumaa. Mwanao ana jina la kipekee, Kaya Gacheri Catalina Raftery.
Katika chapisho lake alisema, "Siyuko mjamzito tena. Barretraftery nami hatimaye tulipatana na mtoto wetu wa kike. Zimekuwa siku zenye kimbunga. Tunafuraha zaidi, shukrani na upendo mwingi kwa mtoto wetu. Tumerudi nyumbani. Rafiki yetu asiyelipa kodi ya nyumba ako karibu kutuonyesha rangi zake za kweli. Huku akitufunza trimesta ya nne. Ulezi 101 unaendelea".

Watu walimpa hongera kwa kujifungua mtoto salama.
Tarehe 9 mwezi wa September mwaka uliopita, Anita na Barret walifanya harusi ya kufana. Iliyohudhuriwa na familia na marafiki wa karibu.
Tunawatakia kila la heri katika safari yao mpya ya kuwa wazazi.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Je, Anita Nderu Ana Mimba?