Anthony Madu Aiteka Dunia Kwa Talanta Yake Ya Kudensi Ballet

Anthony Madu Aiteka Dunia Kwa Talanta Yake Ya Kudensi Ballet

Anthony Madu mwenye miaka 11 amekuwa mada kwenye mtandao baada ya video yake akisakata densi maarufu kama ballet kuibuka. Amenasa roho za watu wengi kwa kupitia kwa video hii. Wengi wakisifu ujasiri wake kwa kuingia kwa tasnia ya densi zinazo dhibitika na jamii kama za wasichana. Ballet nchini nyingi huwa tasnia ya wanawake. Ila ameenda mrama na imani hizi na kuwa kijana anaye julikana duniani kote kwa densi hii.

anthony madu

picha shukrani kwa:reuters

Hadithi yake ina linganishwa na ya Billy Elliot, mtoto mwingine wa miaka 11 aliye enda mrama na imani za jamii na kufanya kitu kilicho mfanya ahisi kuwa ana furaha. Anthony Madu hakuficha talenti yake kwa wazazi wake na walimuunga mkono katika uamuzi wake wa kufanya densi hii. Hata kama alikiri kuwa wazazi wake walitaka awe mhubiri. Kitu ambacho hakikuwa rohoni mwake.

Video ya kijana huyu kutoka Nigeria ili onekana kwenye mtandao mwezi wa June. Huku akidensi ballet kwenye mvua na mtindo ambao haukua na doa. Watu walimsifia kwa mwendo wake, kana kwamba alikuwa ana densi mbele ya umati wa watu duniani nzima hata kama alikuwa peke yake kwenye mvua nje ya shule anako somea ballet Leap Dance Academy.

Hata kama kulikuwa kuna nyesha, jambo hilo halikumfanya asi sakate densi kwenye mvua. Zaidi ya watu milioni 15 wametizama video ya Anthony akidensi kwenye mvua. Video ambayo iliteka macho ya American Ballet Theatre na wakampa scholarship na kupanga jinsi angepata mafunzo kupitia kwa mtandao. Mwaka ujao, atakuwa aki soma kudensi Umarekani na shule maarufu ya Ballet Beyond Borders.

Alipo ulizwa, alisema kuwa kuimba humfanya ahisi kuwa anafanya kitu kinacho mfurahisha. Pia, marafiki wake wanapo muona akidensi, wanashangaa kijana huyu anafanya nini? Kwa sababu hii ni densi mpya na sio maarufu kwa wanaume. Sasa ana furaha kwa sasa, densi hii imemtunza na kumfanya apate fursa ya kwenda Umarekani na kujiunga na mojawapo ya shule bora zaidi za ballet duniani kote. Furaha iliyoje!

Na haja jifaidi mwenyewe, kwani hata nchi ya Nigeria itafaidika kutokana na ushupavu wake. Video hii imefanya watu wengi wachange kwa shule anayo enda kujifunza kudensi bila malipo. Na mwanzilishaji wa shule hiyo kusema kuwa ata jaribu kadri awezavyo kuhakikisha watu zaidi wanajua ballet na kujiunga nayo.

Written by

Risper Nyakio