Mama anapo jaribu kutunga mimba, anakuwa makini na kila kitu anacho fanya. Anataka kuongeza nafasi zake za kushika mimba kwa kasi. Kuna baadhi ya vitu ambavyo huenda vika athiri uwezo wake wa kushika mimba. Vitu kama vile, uzani wa mwili, wa juu ama wa chini zaidi. Umri wa mama, mama hutatizika kushika mimba anapo fikisha miaka 35 na zaidi. Vyakula anavyo kula ikiwemo uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe. Kuna baadhi ya dawa ambazo zinaweza punguza uwezo wa mama kushika mimba kwa kasi, kama vile antibiotics. Unafahamu jinsi antibiotics zinavyo zuia kushika mimba?
Wakati wote, mwanamke anaye kuwa katika harakati za kushika mimba hushauriwa kuzungumza na daktari kabla ya kuchukua dawa zozote. Unapo enda kufanyiwa vipimo, ni muhimu kumjuza daktari kuwa unajaribu kutunga mimba. Kwa njia hii, atakuwa makini na aina ya dawa anazo kupatia.
Jinsi antibiotics zinavyo zuia kushika mimba

Kuna baadhi ya antibiotiki zinazo sababisha matatizo ya uzalishaji katika wanaume. Kwa kuathiri kiwango na ubora wa manii ambayo mwanamme anawachilia. Manii yanapo punguka kwa idadi na kupunguza uwezo wa kuogelea kwa kasi, inakuwa vigumu kumfanya mwanamke ashike mimba. Antibiotics hizi ni kama vile:
- erythromycin
- Neomycin
- Tetracyclines
- Gentamicin
Jinsi antibiotics zinavyo boresha uzazi

Maambukizi ya bakteria ni mojawapo ya vyanzo vikuu vya matatizo ya kizazi katika wanawake na waume. Maambukizi ya kingoni kama gonorrhea huenda yaka athiri uterasi katika wanawake na njia inayo tumika na manii katika wanaume.
Huenda mwanamke akakosa kufahamu kuwa ana maambukizi ya kingono. Kwani kuna baadhi ya maambukizi yasiyo kuwa na ishara zozote. Yasipo tibiwa, maambukizi haya huenda yaka sababisha vidonda kwenye uterasi ama mirija ya ovari. Kuna kufanya ovari itatizike kuachilia yai lisafiri kwenye mirija ya ovari na kurutubishwa na manii. Antibiotiki zinasaidia kutibu maambukizi na kuepusha maambukizi kuharibu sehemu za kizazi.
Baadhi ya antibiotics huenda zika athiri mbinu ya uzazi wa mpango ambayo mama anatumia. Na kuifanya isiwe na nguvu tosha za kudhibiti kushika mimba. Antibiotics kama Rifadin huwa na athari hii. Ni vyema kumwuliza daktari iwapo mnaweza tumia mbinu nyingine ya kinga kama vile mpira.
Hitimisho
Kwa wanawake wanao jaribu kushika mimba, ni vyema kuwasiliana na daktari wao kabla ya kutumia antibiotics zozote zile. Pia kwa walio na mimba, hakikisha wakati wote unachukua dawa baada ya kuagizwa na daktari anaye fahamu hali yako.
Chanzo: healthline
Soma Pia: Dalili Za Mimba Ya Mwezi Mmoja Baada Ya Kufanya Tendo La Ndoa!