Antibiotiki pia hufahamika kama viuavijasumu. Ni dawa ambazo hupambana na maambukizi kutokana na bakteria. Hazisaidii dhidi ya maambukizi ya virusi kama vile mafua ama homa ya kawaida. Haya makala yaeleza kama antibiotiki zinaweza kuzuia mimba.
Antibiotiki Zinaweza Kuzuia Mimba?

Antibiotiki ni kemikali ambazo hutumika kuua au kuzuia ukuaji wa bakteria ambazo husababisha magonjwa. Antibiotiki nyingi huwa ni sumu kwa bakteria. Hili neno pia limekuwa likitumika kuelezea dawa ambazo hutumika kuzuia magonjwa kama vile malaria. Pia yale yanayosababishwa na virusi au protozoa.
Antibiotiki zote zina tabia ya kuwa na uchaguzi inapotumika kama sumu. Zinakuwa hatari sana kwa viumbe vinavyoingia ndani ya kiumbe kingine. Kuliko vile vinavyokuwa ndani ya mnyama au binadamu ambaye hutumia kama tiba. Dawa za antibiotiki ni kama vile Penisilini, Ampisilini na Amoksilini . Sio kila antibiotiki inaweza kupambana na maambukizi ya bakteria.
Dawa za antibiotiki zenye muundo sawa wa kemikali huchukuliwa kuwa katika familia moja. Ni vyema kuwa na ufahamu juu ya familia za antibiotiki kwa sababu tatu kuu:
- Dawa za antibiotiki kutoka familia moja kwa wakati mwingine hutibu matatizo yanayofanana.
- Kama una mzio kutokana na dawa moja ya antibiotiki, utapata mzio pia kutokana na dawa zingine kutoka kwa hio familia. Hii ina maana kuwa unafaa kutumia dawa nyingine kutoka kwa familia tofauti ya antibiotiki.
- Dawa ya antibiotiki lazima itumiuke kwa kikamilifu. Aidha kukatiza dozi bila kukamilisha siku zote za matibabu huweza kuyafanya maambukizi kuwa sugu zaidi.
Antibiotiki Katika Kuzuia Mimba
Mchakato wote wa kupata mimba huongozwa na homoni. Hamna mahali ambapo antibiotiki huingiliana na hizi homoni. Hivyo basi ni vigumu kwa antibiotiki kuzuia mimba. Pia kuwa na mimba haimaanishi kuwa mtu ana bakteria mwilini. Hili ni jambo ambalo hutokea baada ya yai la mwanamke kurutubishwa na mbegu ya kiume. Ilihali kijusa ni kigeni mwilini, mwili hukitambua kama mmoja wake.
Bakteria ambazo huingia mwilini huwa geni kwenye mwili. Hivyo basi mwili huunda kinga dhidi ya zenyewe. Pia dawa za antibiotiki hutumika kusaidia kupigana na hizi bakteria. Hivyo basi matumizi ya antibiotiki katika kuzuia mimba haina ufanisi. Muundo wa antibiotiki wa kufanya kazi ni kutambua bakteria geni mwilini na kuziua.
Ata hivyo, kuna njia mbalimbali ambazo mtu anaweza kuzingatia ili kuzuia mimba. Hizi ni kama vile:
- Njia za asili: njia ya kuhesabu siku, ngono bila kuingiliana kimwili, unyonyeshaji, kuchomoa ume mwanamume anapofika kileleni
- Njia za kudumu: vasektomi na kufunga kizazi( tubal ligation)

- Njia za homoni: hizi hufanya kazi kwa kuzuia ovari kuachia mayai ya uzazi. Lakini baada ya kuzitisha ovari huanza kutoa mayai tena. Kuna vijiti, sindano ama vidonge vya majira
- Njia za kitanzi ama(intrauterine devices): hizi huwa nyenzo kidogo ambazo huingizwa kwenye kizazi cha mwanamke
- Njia za vizuizi: hizi hufanya kazi kwa kuzuia mbegu za kizazi za mwanamume kufikia yai la mwanamke. Ni kama vile kondomu ya kiume, kondomu ya kike na daframu
Kwa hivyo, jibu kwa swali iwapo antibiotiki zinaweza kuzuia mimba ni la. Antibiotiki hazina athari yoyote kwenye homoni ama mbegu za mwanamume.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Njia Tofauti Za Kuzuia Mimba Kama Vile Kwa Kutumia Chumvi!