Asali ina manufaa mengi kwa mwili, hata hivyo asali kwa mtoto mchanga ina athari hasi. Haishauriwi mtoto mchanga chini ya mwaka mmoja kutumia asali. Kula asali kunamuweka katika hatari ya botulism, na kwa sababu hii, wazazi wote huagizwa kujitenga na kuwapa watoto wachanga asali. Asali huwa na msimbo wa bakteria ya Clostridium botulinum, inapoingia kwenye mwili wa mtoto, hutolewa kama sumu inayo sababisha botulism.
Botulism kwa watoto

Ishara za botulism katika watoto
- Mzio
- Kukosa nguvu
- Kutatizika kula
- Kuvimbiwa
Mtoto aliyekula asali huenda akatatizika kupumua, kulia ama kusumbua mara kwa mara. Ishara hizi hushuhudiwa kati ya masaa 36 baada ya kula asali, huku watoto wengine wakionyesha dalili baada ya wiki mbili.
Watoto wakubwa na asali
Watoto wakubwa na watu wenye umri zaidi pia wanaweza kupata botulism lakini kwa viwango tofauti ikilinganishwa na watoto wachanga. Kwa sababu hii, wanakubalishwa kula asali kwani athari kwao sio nyingi kama kwa watoto wachanga. Pia, watoto wakubwa wanaweza kupata botulism kutokana na ulaji wa vyakula vilivyo haribika ama vyenye sumu ya botulinum ama majeraha.
Kwa watoto wenye umri wa miaka miwili na zaidi, wanaweza kula asali raw isiyoongezwa kitu chochote. Katika visa vingine, kuchanganya kijiko kimoja cha asali na yai kunatumika kama matibabu. Pollen iliyo kwenye asali isiyochakatwa imedhibitishwa kusaidia kudumisha kinga ya mwili.
Katika nchi zingine, asali inatumika kutibu jeraha kufuatia msimbo wake wa antimicrobial. Ama badala ya antibiotics kutibu bakteria.
Asali iliyo na polen inaweza kusababisha matatizo yafuatayo:

- Kumfanya mtu kuhisi kizunguzungu
- Kuzua maumivu ya kichwa
- Kuchochea kupata saratani
- Kusababisha kichefuchefu
- Mapigo ya kasi ya moyo
- Kumfanya mtu kutapika
Baada ya mwaka mmoja, mzazi anaweza kuanza kumwanzishia mtoto asali kwa kuongeza kwa vyakula anavyovipenda. Baada ya kuongeza asali kwa chakula chake, mpe siku nne kabla ya kumlisha tena ili kuona iwapo ataonyesha dalili zozote za mzio dhidi ya asali. Mzazi anaweza kuongeza asali kwenye maziwa ya bururu, smoothie, kupaka kwa mkate ama kuongeza kwa pancakes zake.
Ni muhimu kwa wazazi kuepuka kuwapa watoto wachanga asali, kwani asali kwa mtoto mchanga in athari nyingi hasi. Badala yake wanaweza kuwapa vitu vingine mbadala vilivyo pitishwa na madaktari wa watoto wao.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Maumivu Ya Tumbo Kwa Mtoto Mchanga, Ishara Na Vyanzo Vyake