Athari Chanya Za Kujichua Kwa Afya

Athari Chanya Za Kujichua Kwa Afya

Kwa watu wengi, kitendo chao cha kwanza cha kimapenzi kilikuwa kupitia kwa kujichua. Na nafasi kubwa ni kuwa hawa kukoma kujishika hata baada ya kufanya mapenzi.

Kujichua ni kitendo cha kawaida cha kingono. Watu wengi hufanya uamuzi wa kung'amua zaidi kuhusu miili yao katika kitendo hiki cha kujipenda. Ni mojawapo ya njia za kusoma kuhusu mwili wako, kutoa nishati ya kingono iliyo kwama mwilini, kupunguza mawazo mengi na uchungu. Ikiwa ungeuliza watu kuhusu athari chanya za kujichua kwa afya, watasema bila kusita kuwa una jipendeza. Lakini, je, kuna athari hasi unazo paswa kujua?

Kujichua ni nini?

athari chanya za kujichua

Kujichua ni pale ambapo mtu anajifurahisha kwa kugusa sehemu zake za siri na lengo la kufika kilele sawa na katika kitendo cha ngono. Kitendo hiki ni kawaida kwa wote wake kwa waume.

Kujichua: Athari chanya za kujichua

Kweli, kitendo hiki kina manufaa kwa afya yako. Watu wengi kamwe hawatakubali kuwa wao hufanya kitendo hiki. Hii ni kwa sababu, hii ni mada ambayo watu hawapendi kuzungumzia. Kitendo cha ngono pia ni vigumu kukubali, na je kujichua? Kuna baadhi ya watu wanacho kiona kitendo hiki kama makosa. Mbali na haya yote, kitendo hiki kina manufaa kwa afya kama vile:

  • Unaweza kuuelewa mwili wako vyema

Kwa watu wengi, kitendo chao cha kwanza cha kimapenzi kilikuwa kupitia kwa kujichua. Na nafasi kubwa ni kuwa hawa kukoma kujishika hata baada ya kufanya mapenzi. Kujichua huwapa watu siri na ujasiri wa kuzuru na kung'amua kinacho wapendeza kingono. Wanapo fahamu sehemu zinazo wachechua, wana zizungumzia na wachumba wao na kuwafanya wawe na maisha bora ya kingono.

  • Kujichua kuna punguza mawazo na maumivu ya kichwa

matamanio ya kingono

Unashangaa kivipi kujichua kwa dakika chache kuna saidia kupunguza maumivu ya kichwa. Hii ni kwa sababu baada ya mawazo mengi ya kimaisha, kujichua kuna usaidia mfumo wako kuanza upya tena. Sawa na vitendo vyovyote vile vya kingono, kujichua kuna usaidia mwili kuwachilia homoni za endorphins zinazo saidia kutuliza neva zako, kuboresha mhemko wako na unaweza kulala vyema zaidi!

Mbali na anuwai ndefu ya athari chanya za kujichua kwa afya, kitendo hiki pia kinasaidia kwa kukuepusha na maradhi yanayo sababishwa na ngono kati ya wake na waume.

Chanzo: WebMD

NHS

Soma Pia:Sababu Kwa Nini Wanawake Wanapaswa Kufahamu Jinsi Ya Kuanzisha Ngono

Written by

Risper Nyakio