Athari hasi za kumtishia mtoto ni kama vile mtoto kutatizika kuwasiliana na watu wengine. Katika video iliyovuja mitandao mapema mwezi huu, mwimbaji wa nyimbo za injili Kasolo anaonekana nyumbani mwake akimtetesha na kumtishia mtoto wake wa kike maisha. Katika kisa hiki, mwimbaji alimtaka mtoto wake mdogo kumwelezea kwa nini alikuwa anacheza na chupa ya maji, na asipo angemnyonga.

Kwa maneno yake, alisikika akisema, "Unacheza aje na kitu ya kunywa maji? Kwanini umevunja mpira ya pesa nyingi hivyo, nikuue?" Mtoto anaonekana akilia kwa nguvu. "Nikunyonge mimi, nikuue? Utavunja tena?" Mtoto anajibu, "Nakupenda baba". Mwimbaji anaonekana akicheka na kutabasamu baada ya kuyasikia maneno haya kutoka kwa mwanawe.
Athari hasi za kumtishia mtoto
Wazazi wengi hasa wa kiafrika wana tamaduni ya kuwatishia watoto. Kulingana na wazazi hawa, kuwatishia watoto kunawasaidia kuwa na nidhamu zaidi. Je, hii ni kweli? Kuwatishia watoto kwa kutumia maneno makali kama, nitakuua, nitakunyonga, nitakufukuza, mimi siyo mzazi wako na kadhalika kuna athari hasi katika saikolojia ya mtoto. Tazama jinsi watoto wanaokua katika mazingira wanapotishiwa kila mara na wazazi wao wanavyoathiriwa.
- Kuharibu uhusiano kati ya mama na mzazi
Mtoto anapotishiwa kila mara na mzazi wake, anaanza kuwa na chuki kwake. Anahisi kuwa mzazi wake hamwelewi, huku mzazi akihisi kuwa haheshimiwi. Inageuka kuwa ushindani wa atakayesikizwa wa kwanza. Huenda mtoto akajitenga na mzazi wake kabisa. Hata anapokuwa na tatizo, hawezi kumwambia mzazi wake.
2. Mtoto kudhani ni jukumu lake kumfurahisha mtoto
Katika kisa tulichoangazia hapo mwanzoni, mtoto mchanga tayari anajua kuwa anapaswa kumwambia mzazi wake kuwa anampenda ili asiathibiwe. Hata kama mtoto huyu mara nyingi anahisi kumchukia ama kumwogopa mzazi wake, njia ya kipekee ya kuepuka adhabu ni kwa kumfurahisha. Jambo litakalokuwa na athari hasi kwa saikolojia ya mtoto, kwani atajaribu kufanya hivi kwa watu wote hata walimu na marafiki kuepuka kuwakasirisha. Mwishowe, watu wengi watamtumia isivyofaa.
3. Kuharibu motisha ya mtoto

Kuna baadhi wazazi wanaowatishia watoto wasipofuzu darasani. Kuwatishia watoto siyo njia sawa ya kuwapa motisha, badala yake, mtoto anakosa motisha, hamu ya kusoma ama kufuzu. Huenda watoto wa aina hii pia wakaanza kukosa kwenda shuleni, kwani wanahisi kuwa juhudi zao masomoni hazithaminiwi. Athari nyingine kwa watoto hawa ni kuanza kuwachukia walimu na kujitenga na watoto wengine shuleni.
4. Kuathiri mawasiliano ya mtoto
Mtoto anapotishiwa mapema maishani mwake, anahisi kuwa mzazi wake hamwelewi. Pia atakuwa na uwoga kuwa huenda chochote atakachokisema kitamkasirisha mzazi wake. Kwa njia hii, mtoto ataepuka kuzungumza na mzazi wake, kuepuka mazungumzo ya mada anazohisi kuwa huenda zikamkasirisha mzazi wake. Mtoto anapokua bila kuzungumza, hatafahamu jinsi ya kujieleza hata anapokuwa mtu mkubwa.
Soma Pia:Wazazi Kuchoka Katika Ulezi, Ishara Na Vyanzo Vyake