Athari 5 Hasi Za Kunywa Maji Moto Sana Mara Kwa Mara

Athari 5 Hasi Za Kunywa Maji Moto Sana Mara Kwa Mara

Watu wengi wanafahamu kuwa kunywa maji moto kunasaidia miili yao, lakini je, ni kweli?

Je, unafahamu kuwa kunywa maji moto sana mara kwa mara kuna athari hasi? Ni maarifa maarufu kuwa kunywa maji moto kuna orodha ndefu ya manufaa; walakini kunywa mara kwa mara kuna athari hasi kwa afya yako. Watu wengi wanaofikiria kuwa kukunywa maji moto ni mojawapo ya njia bora za kuwa na afya. Imani hii sio kweli. Baadhi ya watu hukunywa maji moto kwa sababu nyingi kama vile hali ya anga na sababu za kiafya, lakini inaweza hatarisha afya yako. Unashauriwa kunywa maji ya vuguvugu badala ya maji moto. Makala haya yana lenga kukuelimisha kuhusu athari za kunywa maji moto mara kwa mara.
Side effects of drinking hot water

Chanzo: [Pintetrest]

Hapa kuna baadhi ya athari hasi za kunywa maji moto mara nyingi

  1. Yana uchafu mwingi
athari za kunywa maji moto

Maji moto yana uchafu zaidi ikilinganishwa na maji baridi [New York Post]

Watu wengi hufikiria kuwa maji moto ni safi lakini sio kweli. Ikiwa unakunywa maji moto kutoka kwa mfereji, kuna nafasi kubwa kuwa yana uchafu mwingi. Hii ni kwa sababu maji moto yana vitu vingi vilivyo kwama kwenye maji hayo. Ikiwa mfereji umezeeka sana, chembe za lead zita changanyika kwenye maji hayo yanayo kuwa kwenye mtungi.
Unashauriwa kutumia birika kuchemsha maji yako ili yawe salama ya kunywa.

2. Kutokuwa na usawa wa maji mwilini

Utafiti umedhibitisha kuwa asilimia 55-65 ya mwili una maji. Kunywa maji kuna manufaa mengi kwa afya na pia kusaidia mwili kuwa na maji tosha na pia kutoa chembe chembe za sumu mwilini. Kunywa maji moto mara kwa mara hata usipokuwa na kiu kunaweza sababisha kutokuwa na usawa wa maji mwilini. Na kufanya uwe na upungufu wa maji mwilini.

3. Matatizo ya kulala usiku

athari za kunywa maji moto

Kunywa maji moto sana kuna sababisha matatizo ya kulala [EUR This N That]

Kunywa maji mengi yaliyo moto kuna sababisha matatizo ya kulala. Epuka kunywa maji moto kabla ya kuenda kulala kwani yanaweza tatiza usiku wako na kukufanya uende msalani mara kwa mara.

4. Kushinikiza figo yako

Figo ina mfumo unao saidia kutoa maji zaidi na sumu mwilini. Kunywa maji mengi yaliyo moto kuta shinikiza figo kwa kuongeza kasi ya kufanya kazi yake.

Kwa sababu kunywa maji moto kunasababisha upungufu wa maji mwilini. Kunaweza ongeza kazi ambazo figo yako inapaswa kufanya na kuzidishia kiungo hiki kazi.

Hatimaye, huku kuta athiri figo yako.

5. Kuchoma viungo vya mwili

Kunywa maji moto sana kuna weza sababisha kuchoma viungo vya ndani ya mwili vilivyoko kwenye koo. Unaweza choma midomo yako, sehemu ya ndani ya mdomo na hata ulimi wako.

Hakikisha kuwa una angalia joto ya maji kabla ya kuyanywa. Ni vyema kuyanywa yakiwa ya vuguvugu badala ya yakiwa moto.

Makala haya yalichapishwa tena na idhini ya Pulse.Ng

Soma pia: Je, Ni Salama Kunywa Maji Moto Ukiwa Na Mimba?

Written by

Risper Nyakio