Kuto Lala Vyema Kuna Kuweka Katika Hatari Ya Kupata Saratani

Kuto Lala Vyema Kuna Kuweka Katika Hatari Ya Kupata Saratani

Kuto lala vyema usiku kumehusishwa na ongezeko la ugonjwa wa saratani. Soma zaidi kuhusu athari hasi za kuto lala vyema usiku.

Usingizi mwanana ni nadra sana hasa kwa wamama wanao fanya kazi- tuna fahamu kutimiza majukumu yako kazini na ya kinyumbani kama mzazi ni ngumu, haijalishi umri wa watoto wako. Walakini, hakuna haja ya kuwa mama mkuu huku siku ikiisha unasikia kichwa kimechoka na kuugua athari hasi za kuto lala.

Usipuuze umuhimu wa kupata usingizi tosha kila siku. Bila kulala ya kutosha, una ukaribisha mwili wako kuteseka athari hasi za kiafya.

Lala mapema ama uugue athari hasi za kuto lala

how to prevent oversleeping

  1. Nafasi kubwa ya kupata saratani

Usipo pata usingizi tosha, una nafasi za juu za kuugua saratani ya matiti na ya prostrate kwa wanaume, kulingana na National Sleep Foundation. Mtandao wa John Hopkins Medicine unaeleza haya kwa sababu ya usumbufu kwa 'saa ya kibiolojia' ya mwili wako, inayo ongoza usingizi. Na kuongeza nafasi za kupata saratani ya matiti, colon, ovari na prostrate.

2. Hatari za juu za kupata ugonjwa wa moyo na inflammation

Mojawapo ya athari hasi za kuto lala ni ongezeko la ugonjwa wa cardiovascular, kulingana na somo hili. Pia una hatari ya kuhisi uchungu, joto jingi, kufura, kuwa na rangi nyekundu na kupoteza utendaji- ishara ya ugonjwa wa moyo. Anza kulala vyema, hasa kama familia yako ina historia ya ugonjwa wa cardiovascular.

3. Kupoteza uwezo wako wa kukumbuka

Masomo yamegundua kuwa kuto lala kuna athari hasi kwa uwezo wa kukumbuka mambo madogo, kama kukumbuka maneno na kukumbuka mambo makubwa pia. Utafiti zaidi ulio chapishwa kwa jarida la American Medical Association, unavumbua kuwa usingizi unao sumbuliwa una husishwa na matatizo ya kiakili kwa watu wazima. Kwa hivyo ikiwa una jukumu kubwa ulilo tikwa kazini, hakikisha kuwa unapata usingizi wa kutosha, siku chache kabla ya siku yako kuu kufika.

athari hasi za kuto lala

4. Matatizo ya uzito

Unahisi hamu ya kula vitamu tamu ukiwa kazini baada ya kujaribu kumlaza mtoto wako? Usijali, hauko peke yako. Utafiti huu ulivumbua kuwa mwili huanza kuitisha viwango vingi vya kalori unapokosa usingizi, na kuongeza hamu yako ya kula pia. Wanao kuwa katika harakati za kupunguza uzito wa mwili wanapaswa kuhakikisha kuwa wana lala mapema.

5. Ngozi yako ina zeeka mapema

Kwa wanao itunza ngozi yao kwa umakini, hii ndiyo mojawapo ya athari hasi za kuto lala ambayo bila shaka utachukia. Utafiti umegundua kuwa, kukosa usingizi kuna fanya ngozi ya juu ikose kutenda jukumu lake na ngozi yako inazeeka mbio. Fikiria usingizi kama utaratibu wa utunzaji wa ngozi yako wa usiku, wanawake.

6. Athari hasi kwa mhemko na afya yako ya kiakili

Kuto lala vya kutosha kume husishwa na mhemko na matatizo ya afya ya kiakili. Huenda ukahisi upweke, kukasirika na kufilisika kiakili, ambayo huenda ika geuka iwe matatizo sugu kwa afya yako ya akili. Utafiti huu umegundua kuwa watu wanao tatizika kulala wana nafasi mara mbili za kufilisika kimawazo ama kuwa na mawazo mengi ikilinganishwa na watu wanao pata usingizi tosha.

Vidokezo Kwa Mama Wasio Pata Usingizi Tosha

Hapa kuna baadhi ya ushauri ili kuepuka athari hasi za kuto pata usingizi tosha.

Lala mapema. Unajua, kama mama, huenda ukaamshwa usiku wa maanani kwa jambo moja ama lingine. Ili kuitika unapo itwa, lala mapema. Na ikiwa hautapata tatizo lolote kutoka kwa watoto, utapata wakati zaidi wa kulala.

Saidiana na bwanako. Uliamka mara tano baada ya saa tisa usiku kushughulikia mtoto aliye na tatizo la tumbo? Ongea na mwenzi wako msaidiane kuwa shughulikia watoto usiku ili uwe na usingizi zaidi usio katizwa.

keeping your toddler safe in bed

Saidia kitinda mimba chako kulala vyema. Ikiwa una watoto wazee wanao kuwa na tatizo la kulala, jaribu kutengeneza utaratibu wa kulala na kupata vitu vitakavyo fanya chumba chao kiwe na giza zaidi. Lakini matatizo yakizidi, huenda ikawa ni wakati wa kumtembelea mtaalum wa afya ya watoto. Kwa watoto wachanga, wanachukua kati ya miezi 3 hadi 6 kupata ratiba ya kulala. Tazama njia za kuwasaidia watoto kulala vyema.

Pumzika, tulia kabla ya kwenda kitandani. Watoto wako hupata wimbo, hadithi ya kulala ama kukumbatiwa. Na je wewe? Anza kusoma kitabu, kusikiza muziki ama ununue kitanda chenye starehe, blanketi na mto. Jaribu zoezi la kupumua ikiwa una tatizika kupata usingizi.

Chanzo: WebMD     Byrdie

Soma PiaUtafiti Wa Kisayansi Waonyesha Faida Za Kiafya Za Kulala Mchana

Written by

Risper Nyakio