Athari 5 Hasi Za Kunywa Maji Moto Usizo Tarajia

Athari 5 Hasi Za Kunywa Maji Moto Usizo Tarajia

Ulijua kuwa kunywa maji moto mara nyingi kuna athari nyingi hasi? Ni umaarifa unaojulikana sana kuwa kunywa maji moto kuna orodha mrefu ya umuhimu; walakini kunywa maji haya mara nyingi kuna athari hasi. Watu wengi hufikiria kuwa kunywa maji moto ni mojawapo ya njia bora zaidi za kuzingatia afya ya mwili. Hili si kweli. Baadhi ya watu hunywa maji moto mara kwa mara kufuatia sababu tofauti ama vile kama vile hali ya anga ya mahali ama hali ya afya ila, huenda ikawa na athari hasi kwa mwili wako. Una shauriwa kunywa maji ya vugu vugu ikilinganisha na iliyo moto. Makala haya yata ashiria baadhi ya athari hasi za maji moto unapo yanywa mara nyingi.

effects of drinking hot water

Hapa ni baadhi ya athari hasi za kunywa maji moto mara nyingi

1. Maji haya yana uchafu mwingi

Athari 5 Hasi Za Kunywa Maji Moto Usizo Tarajia

Maji moto huyeyusha uchafu ikilinganishwa na maji baridi [New York Post]

Watu wengi hufikiria kuwa maji moto hayana uchafu ila hisi sio kweli. Iwapo unakunywa maji moto kutoka kwa mfereji, kuna nafasi kubwa kuwa huenda yakawa na uchafu. Hii ni kwa sababu maji moto huyeyusha uchafu ikilinganishwa na maji baridi. Iwapo mifereji hii imezeeka sana na ina kutu, vijisehemu vya madini ya lead yana uwezo wa kuingia kwenye maji haya yanapo pita kwenye mifereji.

Una shauriwa kutumia birika kuchemsha maji kwa usalama.

2. Kukosa kuwa na usawa wa maji mwilini

Utafiti umedhibitisha kuwa asilimia 55-65 ya mfumo wa mwili una maji. Kunywa maji kuna afya na kunasaidia mwili kuwa na idadi tosha ya maji na kutoa sumu mwilini. Kunywa maji moto mara nyingi, hata kama hauhisi kiu huenda kukafanya ukose kuwa na maji sawa mwilini. Na kukufanya ukose maji tosha mwilini.

3. Matatizo ya kulala

side effects of drinking hot water

Kunywa kiwango kikubwa cha maji moto kuna sababisha kutokuwa na usawa wa usingizi [EUR This N That]

Kunywa maji mengi yaliyo moto hufanya ukose kuwa na usawa wa usingizi. Epuka kunywa maji moto kabla ya kwenda kulala kwani jambo hili litatiza usingizi wako na kwenda msalani kila mara.

4. Weka shinikizo kwenye figo

Figo ina mfumo ulio na nguvu wa capillary unao toa maji ya ziada na sumu nje ya mwili. Kunywa maji mengi yaliyo moto kutashinikiza figo kwa kuongeza mwendo ambao unafanya kazi yake.

Kwani kunywa maji moto kuna sababisha kukosa maji tosha mwilini, figo iko hatarini. Inge ongeza kazi ambayo figo inapaswa kufanya, na kufanya kiungo hiki kufanya kazi ziada.

Jambo hili hatimaye lita athiri figo zako.

5. Kuchomeka viungo vya ndani

Unywaji wa maji moto mara kwa mara huenda ukasababisha kuchomeka kwa ndani katika kuta za viungo vya mfumo wako wa mwili. Maji moto kwa urahisi yana weza choma ama kuhatarisha midomo yako na sehemu ya ndani ya mdomo wako na ulimi.

Hakikisha unaangalia joto ya maji kabla ya kuyanywa. Ni vyema zaidi kuyanywa yakiwa vuguvugu ikilinganishwa na yakiwa moto.

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Olamide Ayeni na kuchapishwa tena na idhini ya Pulse.Ng kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.

Soma pia: Is it safe to drink hot water during pregnancy?

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio