Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Athari 5 Hasi Za Mitandao Ya Kijamii Kwa Ndoa

3 min read
Athari 5 Hasi Za Mitandao Ya Kijamii Kwa NdoaAthari 5 Hasi Za Mitandao Ya Kijamii Kwa Ndoa

Hata kama mitandao ya kijamii ni vyombo vya mawasiliano, vinaweza haribu jinsi tunavyo wasiliana na watu wengine. Tazama jinsi ambavyo mitandao ya kijamii huathiri mahusiano yetu.

Mitandao ya kijamii inachangia pakubwa katika maisha tunayo ishi sasa hivi. Kifaa kikuu kinacho tuwezesha kudumisha mahusiano na mazungumzo kwa urahisi. Walakini, mitandao ya kijamii huwa na athari hasi hasa katika mahusiano yetu. Inaweza kufanya uharibifu kwa ndoa zetu. Kivipi? Njia ambazo mitandao ya kijamii inaharibu ndoa na mahusiano. Tazama athari hasa za mitandao ya kijamii kwa ndoa.

Athari Hasi Za Mitandao Ya Kijamii Kwa Ndoa

athari hasi za mitandao ya kijamii kwa ndoa

  1. Mitandao ya kijamii huchukua muda mwingi

Mara nyingi sisi huchukua simu na kuanza kuangalia kinachofanyika kwenye mitandao ya kijamii tusipokuwa na kitu cha kufanya. Bila kufikiria kuzihusu, simu zetu za rununu zimekuwa kimbilio letu tusipokuwa na chochote cha kufanya. Kuchukua wakati mwingi ukitumia mitandao ya kijamii halionekani kuwa jambo kubwa, lakini wakati ambapo wewe na mchumba wako mnatumia wakati mwingi kwenye simu zenu ikilinganishwa na mnapowasiliana na kuwa na muda wa kipekee pamoja, hilo ni suala la kutia shaka.

2. Mitandao ya kijamii inakufanya utamani maisha "bora"

Kumbuka wakati wote kuwa unachoona kwenye mitandao ya kijamii sio kweli kuhusu maisha ya watu wengine. Kila mtu huwa na picha nzuri ya kuonyesha kwa mitandao hata wakati ambapo mambo na maisha yake hayaendi vizuri. Kwa hivyo unapoona kuwa mahusiano ya watu wengine yana ufanisi kwenye mitandao, kumbuka kuwa kuna upande wasio onyesha.

3. Mitandao ya kijamii itakuunganisha na watu wabaya

Wengi wetu tulikuwa na uhusiano na watu wengine kabla ya kufanya ndoa na wachumba wetu, na mitandao ya kijamii inafanya iwe rahisi zaidi kuungana na watu tuliokuwa nao hapo awali. Kupatana na ex inaonekana kama jambo lisilo na ubaya- hauna mawazo mabaya sio? Walakini, kufanya hivi kunaweza ibua hisia za hapo awali na kujipata katika hali tata. Sharti huwa moja, unapofikiria kuungana na mchumba wako wa hapo awali, usifanye hivyo, kwani utamwumiza mchumba uliye naye kwa sasa hivi. Mambo ya kale yanapaswa kubaki ya kale.

athari hasi za mitandao ya kijamii kwa ndoa

4. Mitandao ya kijamii inaweza kufanya uwaeleze watu zaidi kuhusu mahusiano yako

Kuandika jumbe kuhusu mchumba wako mara kwa mara ni sawa, lakini usifanye mara zaidi. Hatutaki kusikia kuhusu makorofishano yako na mchumba wako yaliyo tendeka hivi majuzi. Hata kama unaweza hisi haja ya kuandika kinachofanyika kwenye mitandao unayo itumia. Mara zinapotoka, huna uwezo wa kuathiri kitakachofanyika. Baada ya kutatua matatizo yenu, utajuta kwanini uliweka jumbe zile kwenye mitandao.

5. Mitandao ya kijamii huharibu uwezo wa kuwasiliana

Hata kama mitandao ya kijamii ni vyombo vya mawasiliano, vinaweza haribu jinsi tunavyo wasiliana na watu wengine. Tunapo enda kwa mitandao kuwasiliana badala ya kuwasiliana na wachumba wetu, kuna tatizo kubwa. Wakati wote kuangalia simu zetu tunapokuwa pamoja na wachumba wetu, sio vyema. Mchumba wako hapaswi kujua kinachoendelea maishani mwako kupitia kwa jumbe mitandaoni.

Chanzo: Huffington Post

Soma Pia: Wanandoa Wenye Furaha Huongeza Uzito Pamoja Kulingana Na Sayansi

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Relationship & Sex
  • /
  • Athari 5 Hasi Za Mitandao Ya Kijamii Kwa Ndoa
Share:
  • Ishara 5 Kuwa Hauko Tayari Kufunga Ndoa

    Ishara 5 Kuwa Hauko Tayari Kufunga Ndoa

  • Mambo 3 Ya Kufanya Unapomshuku Mchumba Wako Kuwa Na Mpango Wa Kando

    Mambo 3 Ya Kufanya Unapomshuku Mchumba Wako Kuwa Na Mpango Wa Kando

  • Ishara 5 Kuwa Uko Katika Mapenzi Bandia

    Ishara 5 Kuwa Uko Katika Mapenzi Bandia

  • Ishara 5 Kuwa Hauko Tayari Kufunga Ndoa

    Ishara 5 Kuwa Hauko Tayari Kufunga Ndoa

  • Mambo 3 Ya Kufanya Unapomshuku Mchumba Wako Kuwa Na Mpango Wa Kando

    Mambo 3 Ya Kufanya Unapomshuku Mchumba Wako Kuwa Na Mpango Wa Kando

  • Ishara 5 Kuwa Uko Katika Mapenzi Bandia

    Ishara 5 Kuwa Uko Katika Mapenzi Bandia

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it