Kulingana na mwongozo wa lishe wa Umarekani, watu hula vijiko 16 vya sukari ya kuongeza kila siku. Athari hasi za sukari mwilini ni kama vile kukuweka katika hatari ya kuugua magonjwa kama ugonjwa wa moyo, figo na saratani.
Unapaswa kula kiwango cha sukari kilicho chini ya asilimia 10 ya kalori unazochukua kwa siku. Ikiwa unachukua kalori 1,000 kwa siku, sukari unayoila siku hiyo inapaswa kuwa 100.
Ishara kuwa unakula sukari nyingi

Kukosa furaha. Kulingana na utafiti, watu wanaokula sukari nyingi huwa na nafasi za juu kukwazwa kimawazo na mhemko wa hisia.
Kufura tumbo. Aina fulani za sukari husababisha gesi kujaa tumboni na kufura tumbo kunako ambatana na matatizo ya mengi ya mfumo wa kuchakata chakula.
Viwango vya chini vya nishati. Lisaa limoja baada ya kula sukari, utahisi uchovu mwingi.
Athari hasi za sukari nyingi mwilini
1.Ongezeko la uzito wa mwili
Kula sukari nyingi kwenye chakula na vinywaji na sukari za kuongeza kunahusishwa na ongezeko la uzito. Vinywaji kama vile sharubati, soda, chai na kahawa. Kula na kunywa vinywaji vyenye sukari hukufanya uhisi njaa baada ya muda mfupi na kutamani vyakula zaidi vyenye sukari. Kula chakula kingi na hasa chenye sukari kunaongeza kalori zaidi mwilini na kuchangia katika ongezeko la uzani wa mwili.
2. Kusababisha chunusi kwenye uso
Lishe yenye wanga, kalori na sukari nyingi zimehusishwa na kuongeza hatari ya kupata chunusi kwenye uso. Vyakula vyenye sukari huongeza sukari kwenye damu na kuongeza utoaji wa ufuta, unaosababisha chunusi kutokea. Lishe isiyo na vyakula vingi vya kuchakatwa hulinda dhidi ya chunusi kutokea.
3. Kuongeza hatari za ugonjwa wa moyo
Vyakula vyenye sukari nyingi vimehusishwa na kuongeza hatari ya magonjwa kama vile ya moyo yanayosababisha vifo vingi. Kula chakula chenye sukari husababisha ongezeko la uzani na uzani wa kupindukia ama obesity, sukari ya damu na shinikizo la damu. Magonjwa haya huongeza hatari ya kuugua ugonjwa wa moyo.
4. Hatari ya kuugua saratani
Kula sukari nyingi kunaongeza hatari ya kuugua aina fulani za saratani.
Vyakula vyenye sukari nyingi husababisha ongezeko la kupindukia la uzito na kuongeza hatari ya saratani. Lishe zenye sukari nyingi husababisha kuvimbiwa na kupunguza kiwango cha insulin kinachotelewa mwilini. Zote ambazo zinaongeza hatari ya kuugua saratani.
5. Ngozi kuzeeka kwa kasi
Kupata makunyanzi huwa dhibiti asili ya kuzeeka. Unavyozidi kuzeeka, ndivyo yanavyozidi kutokea mwilini. Walakini, kula chakula duni na hasa chenye sukari nyingi kunaongeza mchakato huu kufanyika kwa kasi. Ngozi inazeeka mapema kabla ya muda.
Mbali na athari tulizo angazia, ulaji mwingi wa sukari husababisha ugonjwa wa figo, afya ya meno kudidimia na kuathiri afya ya kiakili.
Jinsi ya kupunguza kiwango cha sukari

- Kunywa maji na vinywaji vyenye afya ikilinganishwa na kunywa soda na sharubati.
- Kunywa kahawa bila kuongeza sukari
- Kula matunda na sharubati za matunda freshi ikilinganishwa na sharubati za kununua
- Tupilia mbali unywaji wa pombe
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Manufaa 7 ya Tufaha za Kijani Kwa Afya na Urembo