Kuna njia nyingi za kupanga uzazi. Kutumia kondomu, kutumia tembe, kutumia patch ama pete ya uke. Baadhi ya njia hizi zina homoni, ambazo zinaathiri mwili wa mwanamke. Tazama athari hasi za tembe za kupanga uzazi.
Athari Hasi Za Tembe Za Kupanga Uzazi
- Hedhi isiyo ya kawaida na kuvuja damu kati ya vipindi vya hedhi

Kuvuja damu huku hufanyika kwasababu mbinu za uzazi wa mpango huzuia mimba kwa kufanya kuta za uterasi ziwe nyembamba zisiweze kustahimili ujauzito. Viwango vya homoni mwilini huongezeka mwanamke anapotumia tembe zenye homoni. Kuongezeka kwa viwango vya vichocheo mwilini zaidi ya kawaida huathiri utendaji kazi mwilini.
Baada ya miezi mitatu, vipindi vya hedhi huwa vya kawaida tena. Visipo, ni vyema kuwasiliana na daktari wako.
Huku wanawake wengine wakipata vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida na kuvuja damu nyingine, wengine hukosa kupata hedhi yao. Kwa miezi ya kwanza michache ya utumizi wa tembe. Athari za mabadiliko ya homoni mwilini huwa tofauti kwa kila mwanamke.
Mwanamke anapotumia tembe kama njia ya uzazi wa mpango, nafasi zake za kupata maumivu ya kichwa huongezeka. Maumivu haya yanasababishwa na ongezeko la viwango vya homoni. Mara nyingi, maumivu haya huwa siku za kwanza baada ya kuanza kutumia tembe. Kadri mwili unavyozidi kuzizoea, ndivyo athari hii inavyo pungua.

Athari nyingine hasi ya kutumia tembe za homoni kupanga uzazi ni kuhisi kichefu chefu. Mwanamke anashauri kuchukua tembe hizi baada ya kulala ili kupunguza athari ya kuhisi kichefu chefu. Athari hii isipopungua baada ya miezi ya kwanza mitatu, ni vyema kuwasiliana na daktari. Huenda ukawa na tatizo lingine. Baada ya kufanyiwa vipimo, daktari ataweza kubaini tatizo ni gani.
Mabadiliko ya homoni mwilini huchangia pakubwa katika mhemko wa hisia katika wanawake wanaotumia tembe. Mwanamke mwenye athari hii huenda akawa na mawazo mengi na kumweka katika hatari ya kusombwa na mawazo. Ni vyema kuwasiliana na daktari unaposhuhudia athari hii.
- Mabadiliko ya uzito mwilini
Wanawake wengi hushuhudia mabadiliko ya kimwili na uzito wanapoanza kutumia tembe za kupanga uzazi. Hasa katika sehemu kama mapaja, tumbo na matiti, ambapo huwa na ongezeko la uzito na kunenepa. Hata hivyo, kuna baadhi ya wanawake wanaopunguza uzito wa mwili.
Tembe za kupanga uzazi zinawasaidia wanawake walio katika ndoa na uhusiano kuepuka kupata mimba. Kuwapa nafasi ya kupanga uzazi kabla ya kupata ujauzito. Njia inayo shauriwa badala ya kupata mtoto bila njia ya kukimu mahitaji yake. Hivi basi, mwanamke anapohisi kuwa ako tayari kuwa mzazi, anaweza koma kutumia tembe hizi. Zingatia utumiaji wa tembe katika masaa uliyo shauriwa kila siku na kwa makini.
Soma Pia: Mbinu 5 Kuu Za Kupanga Uzazi Na Kuzuia Mimba Baada Ya Ngono