Kuna njia tofauti za uzazi wa mpango zinazolinda dhidi ya kupata mimba. Baadhi ya njia hizi ni kama vile kutumia tembe, kondomu ama IUD. Tembe inalinda dhidi ya kupata mimba kwa kuufanya mwili usitoe yai. Manii yanapoingia mwilini mwa mwanamke, hakuna yai la kurutubisha na mimba haiwezi fanyika. Kondomu kama njia ya kupanga uzazi haina athari hasi inapotumika ipasavyo. Tuna angazia athari hasi za uzazi wa mpango.
Mbinu za kupanga uzazi huwa na homoni za estrogen ama progesterone ama zote mbili. Homoni hivi zinaweza kuathiri mwanamke na kumfanya ahisi uchungu mwingi wakati wa hedhi, apate chunusi ama kuwa na vipindi vizito vya hedhi.
Athari Hasi za Uzazi wa Mpango
Tembe za kupanga uzazi huathiri viwango vya homoni mwilini na kuathiri utendaji kazi wa kawaida wa mwili.
- Kuhisi kichefuchefu

Baadhi ya wanawake huhisi kichefuchefu baada ya kuchukua tembe lakini hisia hizi hupunguka baada ya muda. Tembe za uzazi wa mpango hazipaswi kuwafanya wanawake wagonjeke, ni muhimu kuwasiliana na daktari hali ya kuhisi kichefuchefu isipopungua.
2. Kuvunja damu

Kuvunja damu katikati ya vipindi vya hedhi huwa mojawapo ya athari hasi za uzazi wa mpango. Kuvunja damu husababishwa na mabadiliko ya viwango vya homoni mwilini. Hali hii ikiendelea kwa zaidi ya miezi mitatu, hakikisha kuwa unarudi hospitalini.
3. Ongezeko la uzani

Wanawake wengi hutatizika kutokana na ongezeko la uzani wanapotumia IUD ya uzazi wa mpango. Huku wanawake wengine wakidhibitishwa kupoteza uzani wanapotumia tembe za kupanga uzazi.
4. Maumivu ya kichwa

Tembe zinazotumika kupanga uzazi zinaongezeka maumivu ya kichwa. Mabadiliko ya homoni za kingono za progesterone na estrogen husababisha maumivu ya kichwa.
5. Kukosa kipindi cha hedhi

Kutumia uzazi wa mpango huathiri vipindi vya hedhi, na kuvifanya viwe vizito ama vyepesi. Miezi ya kwanza michache baada ya kuwekwa IUD, huenda mwanamke akakosa kupata vipindi vyake vya hedhi. Iwapo atapata vipindi vya hedhi, huenda vikawa vyepesi ama vizito zaidi.
Mbali na athari za uzazi wa mpango tulizoangazia, mwanamke huenda akawa na hamu ya chini ya kufanya mapenzi na kuwa na maziwa laini kuliko ilivyo kawaida.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Sababu 3 za Kukosa Hedhi Baada ya Kutumia Uzazi wa Mpango