Kipindi cha hedhi ni njia ya maisha ya mwanamke. Kinaashiria kuwa afya ya mwanamke iko shwari na kuwa hana mimba. Hata hivyo, hedhi huwafanya wanawake kukosa vitu vingi maishani. Kuna athari kadha wa kadha za vipindi vya hedhi kwa maisha ya wanawake.
Baadhi ya wanawake hukosa kwenda shuleni wanapo kuwa na vipindi vya hedhi. Kufuatia uchungu mwingi wa hedhi ama kukosa pedi za hedhi. Kukosa kwenda shuleni kwa wiki moja kila mwezi husababisha matokeo yao shuleni kudorora.
Mbali na masomo, mabinti hukosa kujihusisha na mazoezi na vitendo vingine vya kijamii wanapokuwa na hedhi.
Ishara za kipindi cha hedhi kichungu

Mara nyingi, dysmenorrhea ambao ni uchungu mkali katika hedhi, huandamana na ishara kama vile:
- Uchovu
- Kuvimbiwa
- Maumivu makali ya kichwa
- Kuhisi kichefuchefu
- Kutatizika kuwa makini katika jambo
- Maumivu ya mgongo
- Kuharisha
- Hedhi chungu huenda ikawa ni kufuatia kuwa na fibroids, endometriosis ama magonjwa mengine ya kiafya.
Jinsi ya kupunguza uchungu katika hedhi

- Kupata masi ama kukandwa mwili
- Kula lishe bora na kuepuka vyakula vyenye ufuta mwingi, chumvi ama sukari
- Kuwekelea chupa yenye maji ya moto kwenye tumbo
- Kula matunda na mboga kwa wingi
- Kuchukua dawa za kutuliza maumivu kama ibuprofen
Licha ya hedhi kuwa kipindi cha kawaida cha kila mwezi katika maisha ya mwanamke, humfanya kukosa katika vitu vingine maishani. Athari za vipindi vya hedhi ni kama kudorora kwa masomo yake na kukosa kushuhudia michezo hasa kama yeye ni mchezaji.
Katika sehemu ambapo watoto wa kiume hawajaelimishwa kuhusu vipindi vya hedhi. Huenda wakajitenga na wasichana wanapokuwa katika vipindi vyao vya hedhi.
Bila shaka ni muhimu kuzidisha elimu kuhusu hedhi kwa watu wa jinsia zote. Kwa njia hii, wanawake na wasichana watahisi wako huru zaidi kuzungumza kuhusu hedhi, wanapohisi uchungu katika hedhi na kusumbuliwa na vitu vingine katika kipindi hiki.
Wanawake wanaokuwa na vipindi vichungu vya hedhi wanapaswa kuzungumza na daktari. Ili kudhibitisha chanzo cha uchungu huo. Kuna nafasi kubwa kuwa wanatatizika na matatizo mengine ya kiafya.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Hedhi Isiyo ya Kawaida: Utambuzi, Ishara na Jinsi ya Kulinda Dhidi ya Vipindi vya Hedhi Visivyo vya Kawaida