Athari Mbaya Za Paracetamol: Kwa Nini Watu Wanapaswa Kuacha Kutumia Paracetamol Kulainisha Nyama

Athari Mbaya Za Paracetamol: Kwa Nini Watu Wanapaswa Kuacha Kutumia Paracetamol Kulainisha Nyama

Ripoti ya hivi karibuni imeonyesha kuwa hoteli nyingi zinatumia paracetamol kulainisha nyama. Kunywa viwango vikubwa vya dawa hii kuna sababisha figo na maini kutofanya kazi.

Ilipojulikana kuwa paracetamol ilikuwa na nguvu za kulainisha nyama mbio, ilionekana kama gunduo nzuri sana. Baada ya yote, paracetamol haina bei ghali, unawez inunua mahali popote kunako uzwa dawa kwa bei ya chini, na tembe moja inaweza fanya makuu katika kulainisha nyama. Lakini kitu ambacho watu wanayo itumia kulainisha nyama huenda hawakutilia maanani ni athari mbaya za paracetamol.

Athari mbaya za paracetamol: Inaweza fika kiwango kipi?

does paracetamol cause long term damage

Katika miaka ya hapo awali ya 1960, kulikuwa na hofu kuwa aspirin na dawa zingine za uchungu kama vile Ibuprofen zina athari kali kama vile vidonda, tumbo kutoka damu na zinginezo. Uwezekano wa athari hizi ziliwafanya watu kuangalia upande mwingine na kutumia madawa kama vile paracetamol. Kama tokeo, watu wanapohisi maumivu, wange enda kwa zahanati na kununua paracetamol. Kutoka wakati huo, paracetamol ikawa dawa ya kukimbilia ya maumivu mepesi kama vile kuumwa na kichwa. Katika hatua fulani, wana sayansi wakaanza kuangazia kuwa paracetamol inge sababisha matatizo ya muda mrefu kwa kipekee, ila kwa miaka mingi hakujakuwa na utafiti dhabiti kuthibitisha haya.

athari mbaya za paracetamol

Kwa Adeola, mama mchanga aliyeongea na mwandishi wa OperaNews, paracetamol inapaswa kuwa kwenye chungu cha kupika. Ni rahisi zaidi kuchemsha nyama na paracetamol. Nimeitumia kupika mguu wa ng'ombe mara nyingi. Ukiongeza tembe moja, nyama yako ita yeyuka na kuwa laini kwa dakika kumi," alisema.

Mojawapo ya vitu ambavyo ni sawa kwa Adeola na watu wengi wanaochukua dawa hii kutuliza uchungu ni kuwepo kwa dawa hiyo katika maisha ya kila siku. Watu wengi huenda kwa hatua ya kujaza nyumba zao na paracetamol ili wazifikie kwa urahisi. Adeola na watu wanayo itumia mara kwa mara wana hatarisha maisha yao bila ya kujua. Paracetamol inaua inapokunywiwa mara kwa mara kutuliza uchungu, ila inapopikwa chunguni, huenda mtu akawa anataka kupata maradhi ya figo ama maini kutofanya kazi.

Athari mbaya za paracetamol: Kwa nini unapaswa kuacha kutumia paracetamol kulainisha nyama

athari mbaya za paracetamol

Mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa Facebook aliwajulisha watu kuhusu utumiaji wa paracetamol kupika nyama ya mbuzi 'supu ya pilipili' kwa Uyo, taifa la Akwa Ibom na sehemu zingine zinazo izunguka. Sababu ya kitendo hiki ni kuwa inasaidia kuwa hudumia wateja wao kwa mbio zaidi, kuokoa kuni, gesi na mafuta. Ila paracetamol inapo ingia ndani ya nyama na kupatana na joto, uwezo wake wa kutuliza uchungu unapotea, na kuacha nyuma asidi ambayo ni hatari sana kwa ulaji wa binadamu. Katika mchakato wa kupika, kulingana na wataalum, paracetamol inavunja vunjwa na kuwa 4-aminophenol, ambayo ni ina sumu sana kwa figo na mafua.

Kuna uwezekano kuwa huenda hii ikawa sababu kwa nini nambari ya Wana Nigeria wanao tatizika na maradhi ya figo kutofanya kazi inaongezeka. Haijulikana idadi ya hoteli na bukas zinazo tumia paracetamol kulainisha nyama Nigeria. Lakini kulingana na umaarufu wa jambo hili, hamu ya kuokoa wakati na kutengeneza pesa zaidi, unaweza kubaliana kuwa kuna wengi sana wanao fanya hivi. Mwaka uliopita mwezi wa tatu, Shirika la Nigeria la Nephrology (NAN) ilionyesha kuwa milioni 25 ya watu wa Nigeria, wa sehemu ya asilimia 13 ya nchi angalau watu milioni 180 walikuwa na matatizo ya figo kutofanya kazi. Ufahamu huenda ukahitajika kwa sababu watu wengi hawajui hatari za kutumia paracetamol kupika nyama. Walakini, hatari za paracetamol haziishi na watu wanao itumia katika kupika. Wanao itumia wanapo umwa kidogo wako kwa hatari kubwa pia.

Nini kinacho tendeka kwa mwili wako unapotumia kiwango kikubwa cha paracetamol?

athari mbaya za paracetamol

Huku kupika kukifanya paracetamol hatari, kitu mbadala kinawangoja wanao itumia mara kwa mara kutuliza uchungu. Kwa siku, kiwango kinacho shauriwa cha paracetamol ni gramu 4. Kitu chochote zaidi ya hicho ni kikubwa zaidi, na huenda kikafunya upate matatizo ya maini. Kunywa kiwango kikubwa cha paracetamol hufanyika kwa kupuuza. Dawa ambayo wana Nigeria wengi wana fahamu kama paracetamol sio dawa pekee inayo kuwa na paracetamol. Kwa hivyo, kunywa kiwango kikubwa cha paracetamol hutendeka kwa kuchukua bidhaa mbili tofauti zinazo kuwa na paracetamol. Mtu anapokuwa na maumivu ya kichwa, wanachukua paracetamol, ila wanapokuwa na maumivu ya kichwa na homa, wanachukua dawa mbili tofauti zinazo kuwa na paracetamol. Sababu zaidi kwa nini unapaswa kuongea na daktari wako kabla ya kuchukua dawa zozote.

Jinsi ya kuilanisha nyama yako bila kutumia paracetamol

use ginger or lime

Baadhi ya watu ambao hutumia paracetamol kupika, hufanya hivyo kupunguza wakati wa kupika. Hapa chini kuna njia mbadala ambazo unaweza tumia kuifanya nyama yako iwe laini:

  • Kupika kwa kutumia kifaa cha pressure cooker
  • Kata nyama iwe vipande vidogo. Kwa njia hii unakata misuli ya fibre ya nyama na kuifanya iwe rahisi kupika.
  • Ilowe kwenye vinegar ama sharubati ya limau ama divai kabla ya kupika.
  • Pika nyama hiyo pole pole.
  • Ilowe kwenye brine ama maji yaliyo na chumvi nyingi kwa masaa machache kabla ya kupika. Hata kama chumvi kwa viwango vikubwa sio nzuri kwako.
  • Unaweza tumia tangawizi ama limau ku imarinate ile nyama.
  • Nunua bidhaa za dukani za kulainisha nyama, ila hakikisha kuwa unatumia viwango vidogo kuepusha nyama ile kuwa laini sana.

Kwa ujumla, unapaswa kuepuka kutumika paracetamol kama njia ya kulainisha nyama. Na iwapo utakunywa kiwango cha kupindukia cha paracetamol, mtembelee daktari bila kusita.

Soma PiaCan you take paracetamol in pregnancy?

Chanzo: NIMED Health Nigeria, Web MD

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio