Je, wewe hujipata ukishangaa ni nini ulifanya kisha ukabarikiwa na mwanamke anayependeza zaidi maishani mwako. Shukuru babake kwa hilo! Je, unafahamu athari ya baba maishani mwa bintiye?
Utafiti umedhibitisha kuwa baba huwa na jukumu kubwa katika kukuza utu wa bintiye. Wanawake wanao jiamini, wenye uthubutu na nia kali hufuzu maishani mwao na wakati mwingi, wanawake hawa mara nyingi walikuwa na baba aliyeshughulika na maisha yao wangali wachanga.
Huenda pande zote mbili
Ikiwa wewe ni baba wa binti mzuri, una nguvu za kusaidia kukuza utu wake na pia kuathiri kutosheleka kwake anapokua na kuamua kuoleka. Baba ana athari kubwa kwa jinsi bintiye atakavyo tosheleka katika ndoa. Kuhusika kwa mapema kwa baba kwa kuwa maishani mwa binti yake kunaboresha mtazamo wake wa ndoa.
Kuna baadhi ya baba ambao kwa sababu tofauti hukosa kuwa maishani mwa watoto. Utafiti umedhibitisha kuwa wasichana hawa huwa na nyakati ngumu maishani mwao, kama vile kukosa kujithamini, kutofuzu masomoni na kukosa hamu ya masomo ya Hisabati na Sayansi.
Kutumia nguvu hizi kwa uzuri
Kuna usemi maarufu, "Nguvu nyingi huambatana na majukumu makubwa", una jukumu la kufanya mambo yanayofaa kwa binti yako. Huenda ikawa sio rahisi, hasa ikiwa mmetenganishwa ama una kazi mbili ili kutokimu mahitaji ya familia yako. Walakini, itakuwa na tofauti kubwa unapohusika zaidi katika maisha ya mtoto wako. Kuna visa 5 tofauti ambapo binti yako anaweza kutumia msaada wako.
Athari ya baba maishani mwa bintiye

- Masomo, hasa somo linalohusisha kufikiria kwa kina
Kulingana na tasnifu uliofanyika na mwanafunzi wa shahada ya udaktari, wanawake hawana hamu ya somo la Hisabati isipokuwa pale ambapo baba zao wanahusika katika masomo yao. Sikubaliani na tasnifu hii, lakini kwa sababu ya binti yako, tuchukulie kuwa ukweli.
Msaidie binti yako kufanya kazi ya ziada ya somo la Hisabati. Hata kama una kazi nyingi, tenga muda umsaidie katika somo hili. Ikiwa hana kazi za ziada, unaweza kumfunza mambo machache ya Hisabati.
2. Mambo ya kujifanyia mwenyewe
Bibi yangu anafahamu jinsi ya balbu ya nyumba, hili linapaswa kuwa jambo la kawaida, ila mambo ni tofauti. Anajua hili kwa sababu babake alimhusisha katika kazi za kinyumbani. Kwa hivyo, sisi wawili tunasaidiana na majukumu ya kinyumbani.
Uhodari huu ni muhimu, hata ingawa umepuuzwa kwa sana. Ni vyema kufahamu kuwa hakuna majukumu ya kijinsia. Kwa hivyo kumhusisha binti yako unapotengeneza gari nyumbani ni vyema. Atakapokuwa na gari yake siku moja, atajua linapokuwa na tatizo.

3. Kuendesha baiskeli
Ikiwa kuna wakati ambao baba wanathamini zaidi, ni siku ambapo binti yao aliendesha baiskeli bila usaidizi. Kama nilivyosema hapo awali, sio jambo ambalo ni baba peke yake anaweza kufanya, ila, kama wewe ni baba, usisahau kumfunza binti yako kuendesha baiskeli.
Baadaye maishani, unaweza kumfunza jinsi ya kuendesha gari. Ni baadhi ya uhodari bora ambao mtu anaweza kujifunza.
4. Mfunze jinsi ya kuogelea
Babangu hakujua jinsi ya kuogelea. Lakini hilo halikumsimamisha kuingia kwenye dimbwi la maji nilipokuwa mchanga. Alihakikisha kuwa ningeogelea vyema. Baadaye, nilipata gwiji wa kuogelea aliye nisaidia kupevusha uhodari wangu wa kuogelea.
Ikiwa unaweza, mfunze mtoto wako jinsi ya kuogelea. Mfunze kuuamini mwili wake na hisia zake anapoogelea. Pia unaweza mtafutia gwiji wa kuogelea amfunze. Watoto husoma kwa kasi zaidi ikiwa wazazi wao wako karibu kushuhudia.
5. Mfunze kusoma watu
Hili ni jambo ambalo watu wengi husoma baada ya kuchomeka mara kadhaa. Kama baba wa binti, unakua uwezo wa kunusia hatari ikiwa kwa umbali. Unaweza kuangalia machoni mwa mtu na kufahamu ikiwa hamtakii mema. Msaidie kukuza uwezo huu.
Lakini zaidi ya hayo, kuwa mfano wa anachopaswa kutafuta kwa mwanamme, ili asiwe na mtu ambaye hamthamini. Kuna wanaume ambao huvunja kujiamini kwa mwanamke ili waendelee kuwa nao. Mfunze kuwa uwezo wa kuwa mwanamme si kudhihirisha nguvu ila ni kudhihirisha tabia na utu.
Baba, usipoteze chanya cha kuwa na athari chanya kwenye maisha ya binti yako baadaye maishani kwani athari ya baba maishani mwa bintiye
Chanzo:
- Father absence and its effect on daughters. Mancini Lisa.
Soma Pia:Jukumu La Baba Katika Familia Na Maisha Ya Watoto Wake