Athari Hasi Na Chanya Za Bitter Leaf Kwa Mama Mwenye Mimba

Athari Hasi Na Chanya Za Bitter Leaf Kwa Mama Mwenye Mimba

Yote unayo paswa kujua kuhusu bitter leaf na mimba.

Faida za bitter leaf unapokuwa na mimba hazipaswi kuwa jambo la shaka. Hii ni iwapo unajua kula vyakula kwa viwango vinavyo hitajika hasa wakati huu ambapo una mimba. Kula viwango vikubwa vya chakula huenda vikakufanya kuwa na uzito mwingi wa mwili na kutatiza zoezi la kujifungua. Je, athari za bitter leaf kwa mimba ni zipi?

Athari Za Bitter Leaf Kwa Mimba: Athari zake kwa mwili

athari za bitter leaf kwa mimba

Mmea huu unapatikana katika sehemu nyingi hasa katika bara la Afrika. Ni mmea wa kipekee unaojulikana kufuatia ukali wake na huwa na majina tofauti kulingana na mahali ama watu wanao ishi sehemu fulani.

Ukali wake hufanya watu watumie wakati mwingi wakiosha ili ukali ule upunguke na kisha watumie matawi yale katika mapishi yao. Bitter leaf pia ina faida za kimatibabu. Inatumika kutibu matatizo kama vile kisukari, shinikizo la juu la damu na magonjwa mengine.

 Athari Za Bitter Leaf Kwa Mimba Ni Zipi?

athari za bitter leaf kwa mimba

Chanzo cha picha; Shutterstock

Madaktari hushauri wamama wanao kuwa na mimba kuwa makini sana wanapo tengeneza lishe yao na chakula chochote wanacho kila. Kwa sababu huenda baadhi ya vyakula hivi vikawa na athari hasi kwa afya yako ama ya mtoto wako. Huenda ukawa na shaka iwapo bitter leaf ni salama kuliwa mama anapokuwa na mimba. Unapaswa kujua faida za kimatibabu za mmea huu.

benefits of bitter leaf during pregnancy

Kupunguza kisukari

Bitter leaf  imesifiwa sana kwa faida zake za kupunguza kisukari kwa watu wanao kuwa na tatizo hili. Baadhi ya watu huila kupunguza ugonjwa huu na kukabiliana na ugonjwa wa sukari.

Bitter leaf dhidi ya saratani

Bitter leaf imedhihirishwa kisayansi kuwa na uwezo wa kupunguza hatari za saratani na kuwa na uwezo wa kupunguza kusambaa kwa seli zilizo na saratani kwa watu ambao wana saratani. Hii ni kweli hasa kwa watu wanao tatizika na ugonjwa wa saratani ya kibofu.

Wanawake wanashauriwa kuongeza bitter leaf kwenye lishe yao na kufanya mazoezi ili kupunguza nafasi za kuugua ugonjwa wa saratani ya matiti.

Malaria

Sharubati ya bitter leaf ina aminika kusaidia kuponya magonjwa mengi kama vile malaria na typhoid.

Kupunguza shinikizo la damu

Watu wanao tatizika kutokana na shinikizo la damu wana shauriwa kunywa sharubati ya bitter leaf ama kutafuna matawi yake. Kwani yana saidia kupunguza shinikizo la damu. Kuna utafiti mwingi umefanyika kudhibitisha ukweli wa imani hii.

Uwezo wa kuzalisha

Bitter leaf helps with conception. Matawi haya yana saidia kutunga. Katika makala yaliyo andikwa na daktari Grace Johnson na kuchapishwa katika Guardian Nigeria, matawi haya yana boresha afya ya kijumla na kusaidia ovari kutoa mayai yenye afya na kusawasisha homoni. Ukikula matawi haya mara kwa mara, bila shaka utaboresha uwezo wako wa uzalishaji.

Athari hasi za bitter leaf kwa mimbacan bitter leaf abort pregnancy

  • Kupoteza mimba

Kula bitter leaf kwa viwango vingi unapokuwa katika trimesta ya kwanza ya mimba yako huenda kuka sababisha kupoteza mimba.

Wanawake wanashauri kula bitter leaf kwa viwango vya wastani ili kuepuka janga la kupoteza mimba. Ni salama kwa wanawake walio pita trimesta ya kwanza ya mimba yao.

  • Kuto chakata chakula tumboni

Mwanamke mwenye mimba akizoea kula bitter leaf mara kwa mara, huenda akapata tatizo la kuto chakata chakula tumboni ama hata kukosa maji tosha mwilini.

Kula matawi haya yakiwa kwenye supu ni salama zaidi kwani ukali wake huwa umepunguka na ni vigumu kuwa na madhara kwa mimba yako. Kwa njia hii, unaweza kula chakula chako bila shaka ya kula viwango vingi.

Ni vyema kwa kila mama kufuata vidokezo tulivyo angazia vya athari za bitter leaf kwa mimba ili kuhakikisha kuwa safari yao ya ujauzito iko salama na hawa kumbani na matatizo yoyote yale.

Kumbukumbu: Natural Remedy Lab

DrHealth.com 

International Journal of Environmental Research and Public Health

Soma pia: Bleaching during pregnancy: Is it safe?

Written by

Risper Nyakio