Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Kafeini Huwa Na Athari Zipi Kwa Mama Mjamzito?

3 min read
Kafeini Huwa Na Athari Zipi Kwa Mama Mjamzito?Kafeini Huwa Na Athari Zipi Kwa Mama Mjamzito?

Kwa watu wengi, kafeini huwa na athari chanya kwa viwango vyao vya nishati, kutahadhari, kuwa makini na hata kwa maumivu ya kichwa. Lakini sio salama kwa mama mjamzito. Soma zaidi kwa nini.

Kafeini huwa na jukumu la kuongeza nishati na kukufanya uwe na tahadhari zaidi. Duniani kote, watu hukunywa kafeini yako kwenye kahawa, chai na hata vinywaji laini. Lakini vyanzo vikuu ni kupitia kwa chai na kahawa. Wakati ambapo kafeini ni salama kwa watu wengi kwa jumla, wataalum wa afya wana shauri kupunguza kiwango unacho kunywa ukitarajia mtoto. Kwa nini? Kafeini ina athari gani kwa mama mjamzito? Tuna angazia zaidi kuhusu athari za kafeini kwa mimba.

Je, Ni Salama? Kafeini Ina Athari Zipi Kwa Mimba?

athari za kafeini kwa mimba

Kwa watu wengi, kafeini huwa na athari chanya kwa viwango vyao vya nishati, kutahadhari, kuwa makini na hata kwa maumivu ya kichwa. Pia, baadhi ya vinywaji vya kafeini huwa na athari za kiafya. Lakini kafeini pia inaweza kuwa na athari hasi kwa baadhi ya watu na hatari katika mimba.

Kuna baadhi ya wataalum wa afya watakao kushauri kuwachana nayo na wengine wata kushauri kupunguza viwango. Ni vyema wakati wote kushauriana na daktari kabla ya kufanya uamuzi peke yako.

Kwa hivyo, bado unaweza furahia kikombe cha kafeini mara kwa mara unapokuwa mjamzito. Ila, hakikisha kuwa haupitishi 200mg za kafeini kwa siku. Vikombe viwili vya kafeini.

Ukichukua zaidi ya 200mg za kafeini kwa siku ukiwa na mimba, uko katika hatari zaidi ya kupata mtoto aliye na uzito mdogo wa kuzaliwa. Watoto wanao zaliwa na uzito mdogo huwa katika hatari ya matatizo ya kiafya wanapo zeeka.

Kuna utafiti unao onyesha kuwa, kunywa kafeini nyingi ukiwa na mimba kuna ongeza hatari za kupoteza mimba. Hata kama hatari ni kiwango kidogo.

Kiwango hiki cha 200mg kinahusisha vyanzo vyote vya kafeini. Kwa hivyo, sawa na kahawa, utahitajika kuhesabu chai (hata ya kijani), cola, vinywaji vya nishati na chokleti.

coffee bean

Je, Athari Za Kunywa Kafeini Kwa Mimba Ni Zipi?

  • Kafeini ni kichocheo (stimulant) na diuretic

Kama kichocheo, kafeini huongeza shinikizo la damu na mpigo wa moto. Athari hizi zinapaswa kuepukwa ukiwa na mimba. Kafeini huongeza mara unazo enda msalani, na kusababisha punguko la ugili gili wa damu na kusababisha kukosa maji tosha mwilini.

  • Kafeini hupita kondo la nyuma (placenta) hadi kwa mtoto

Hata kama unaweza kuchakata kafeini yako kwa usalana, mtoto wako hana uwezo sawa kwa sababu viungo vyake bado vina kua. Hata kiwango kidogo cha kafeini kina weza badilisha muundo wa usingizi wa mtoto ama mwendo wa kawaida katika hatua za baadaye katika safari yako ya mimba. Kumbuka, kwa sababu kafeini ni kichocheo, inaweza sababisha mkose kulala, nyote, wewe na mtoto wako.

  • Kafeini ni zaidi ya kahawa

Kafeini haipatikani kwa kahawa tu, mbali hata kwa chai, soda, chokleti, vinywaji vya nishati na baadhi ya dawa za zahanati (dawa nyingi za maumivu ya kichwa huwa na kafeini). Kwa hivyo ni muhimu kufahamu kilichoko kwenye chakula na vinywaji unavyo kunywa.

  • Kafeini husababisha matatizo ya kuzaliwa

Imehusishwa na kusababisha matatizo ya kuzaliwa, kujifungua kabla ya wakati, uzalishaji uliopunguka. Na inaweza ongeza hatari ya uzito mdogo wa kuzaliwa na matatizo mengine. Hata kama baadhi ya utafiti bado hauja hitimishwa, ni vyema kuwa salama na afya ya mtoto wako. Mara nyingi, matatizo haya husababishwa na viwango vingi kwa wakati mrefu.

kupoteza mimba ya wiki mbili

 

  • Kafeini husababisha ugumba

Baadhi ya utafiti umeonyesha uhusiano kati ya viwango vya juu vya kafeini na kukawia kujifungua. Hii ndiyo sababu kwa nini tunashauri wanawake na wenzi wao kujitenga na kafeini wanapo jaribu kutunga mimba.

Viwango vya kafeini vilivyoko kwenye vinywaji na vitamu tamu maarufu

  • Kikombe 1 cha kahawa: 60-80 mg
  • Kikombe 1 cha chai: 10-50 mg
  • Chupa ya 375g ya coca cola: 48.75 mg
  • Chupa ya 250ml kinywaji cha nishati: 80 mg
  • 100g ya chocolate bar: 20 mg

Chanzo: Healthline

Soma Pia: Ishara Na Vyanzo Vya Kuharibika Kwa Mimba

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Kafeini Huwa Na Athari Zipi Kwa Mama Mjamzito?
Share:
  • Athari Hasi Za Pombe Kwa Fetusi: Yote Unayo Hitajika Kujua

    Athari Hasi Za Pombe Kwa Fetusi: Yote Unayo Hitajika Kujua

  • Ni Mtindo Upi Wa Kulala Bora Kwa Mama Mjamzito?

    Ni Mtindo Upi Wa Kulala Bora Kwa Mama Mjamzito?

  • Faida 9 Za Tikiti Kwa Mama Mwenye Mimba

    Faida 9 Za Tikiti Kwa Mama Mwenye Mimba

  • Iwapo Una Mimba, Unapaswa Kula Vyakula Hivi. Pap Ni Nzuri Kwa Mama Mjamzito!

    Iwapo Una Mimba, Unapaswa Kula Vyakula Hivi. Pap Ni Nzuri Kwa Mama Mjamzito!

  • Athari Hasi Za Pombe Kwa Fetusi: Yote Unayo Hitajika Kujua

    Athari Hasi Za Pombe Kwa Fetusi: Yote Unayo Hitajika Kujua

  • Ni Mtindo Upi Wa Kulala Bora Kwa Mama Mjamzito?

    Ni Mtindo Upi Wa Kulala Bora Kwa Mama Mjamzito?

  • Faida 9 Za Tikiti Kwa Mama Mwenye Mimba

    Faida 9 Za Tikiti Kwa Mama Mwenye Mimba

  • Iwapo Una Mimba, Unapaswa Kula Vyakula Hivi. Pap Ni Nzuri Kwa Mama Mjamzito!

    Iwapo Una Mimba, Unapaswa Kula Vyakula Hivi. Pap Ni Nzuri Kwa Mama Mjamzito!

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it