Mtu anatatizika na hali ya kisukari, mwili wake hutatizika kutumia insulin ifaavyo na inaweza kusababisha viwango vya juu vya sukari. Baada ya muda, huenda mtu akapata matatizo ya mfumo wa neva, afya ya kiakili na maisha yake ya kingono kuathiriwa. Katika makala haya, tunazungumzia athari za kisukari kwa ngono.
Athari za kisukari kwa ngono kwa wanawake

Kisukari hufanya iwe vigumu kwa mama kuwa aroused kabla ya kitendo cha mapenzi na kumfanya ahisi uchungu wakati wa kitendo cha mapenzi. Kuhisi uchungu katika kitendo kinachopaswa kukufurahisha baada ya muda hukufanya uwachane nacho.
Wanawake wanaotatizika na hali ya kisukari wana nafasi zaidi za kutatizika kutokana na maambukizi ya kingono ama thrush na kuwafanya kutofurahia kitendo kile zaidi.
Athari za kisukari kwa wanaume
Kulingana na utafiti, wanaume walio na kisukari huwa na viwango vya chini vya testosterone, na hamu yao ya kufanya mapenzi kuathiriwa. Wakati mwingi, wanaume walio na kisukari hutatizika na erectile dysfunction. Hii ni hali ambapo mwanamme hawezi kudumu kitandani. Ili mwanamme aweze kudumu kitandani, damu tosha inapaswa kufika kwenye uume wake. Kisukari huharibu mishapa ya damu na kufanya iwe vigumu kwa damu kufika kwenye kibofu chake. Mbali na hayo, kisukari huharibu mfumo wa neva na kufanya iwe vigumu kubaki wima katika kitendo cha ndoa.
Athari kwa watu wa jinsia zote
Watu wanaotatizika na hali ya kisukari huwa na matatizo kama kuchoka ovyo na hamu ya chini ya tendo la ndoa. Kwa jinsia zote, kisukari huwafanya kujiona tofauti, kuwa na wasiwasi mwingi na kusombwa na mawazo. Watu wanaotatizika na hali hii pia hujitenga na watu, kuhisi upweke na kuwa na kujiamini duni.
Matibabu

Kisukari husababisha matatizo ya neva na kuathiri maisha ya kingono. Ili kuepuka matatizo yanayoambatana na kuwa na kisukari, ni muhimu kudumisha viwango vya kisukari vyenye afya.
Kuna dawa ambazo wanaume wanaweza kutumia kuboresha mzunguko wa damu mwilini. Hata hivyo dawa hizi zinapaswa kushauriwa na daktari baada ya kudhibitisha hali ya afya ilivyo. Wanawake wanaweza kutumia lubricants wanapofanya mapenzi kupunguza uchungu.
Mbali na hayo, ni muhimu kuzingatia mtindo wa maisha wenye afya. Kula chakula chenye afya, kufanya mazoezi mepesi mara kwa mara na kuhakikisha kuwa wanadumisha uzito wa mwili wenye afya. Kisha kuhakikisha kuwa wanapunguza mawazo mengi kwa kusikiliza muziki, kufanya mazoezi ama kusoma kitabu.
Kukosa hamu ya ngono kufuatia kisukari sio chanzo cha kuhisi aibu. Badala yake hakikisha kuwa unazungumza na mtaalum na kudumisha mtindo wa maisha wenye afya.
Soma Pia:Kufanya Ngono Baada Ya Kukoma Hedhi: Vidokezo Muhimu Vya Kuzingatia