Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Kuketi Chini Kwa Muda Mrefu Kuna Hatarisha Maisha Yako Kwa Njia Hizi

3 min read
Kuketi Chini Kwa Muda Mrefu Kuna Hatarisha Maisha Yako Kwa Njia HiziKuketi Chini Kwa Muda Mrefu Kuna Hatarisha Maisha Yako Kwa Njia Hizi

Kulingana na utafiti uliofanyika na wanasayansi, watu wanao keti kwa muda mrefu wako katika hatari ya kuugua matatizo ya moyo.

Mengi yamesemwa kuhusu afya yetu na elimu nyingi kufanyika kuhusu jinsi tunavyo paswa kuilinda afya yetu. Mambo kama vile kufanya mazoezi na kuwa makini na lishe yetu ni muhimu sana katika kuzingatia afya na siha bora. Ila kuna baadhi ya mambo tunayo yafanya yanayo haribu juhudi zote tunazo tia za kuangazia afya ya mwili. Una fahamu athari hasi za kuketi kwa muda mrefu?

Athari hasi za kuketi kwa muda mrefu

athari za kuketi kwa muda mrefu

Kupunguza urefu wa maisha yako

Unapo kaa kwa muda mrefu, huenda ukaaga dunia kufuatia matatizo yoyote yale ya kimwili. Na haijalishi ikiwa unafanya mazoezi ama la. Hivi si kwamba ukose kufanya mazoezi yako ya kila siku, la, zidi kufanya mazoezi kama ilivyo desturi yako.

Uko katika hatari ya kuugua kisukari

 

Kati ya watu wanao fanya kazi zinazo husisha kutembea mara kwa mara na wanao keti chini siku nzima. Wanao fanya kazi nyuma ya dawati wako katika hatari zaidi za kuugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa sababu hautumii kalori nyingi. Kwa hivyo, ikiwa unafanya kazi nyuma ya dawati, ni vyema kunyoosha mwili wako mara kadhaa kwa siku.

Hatari ya kuugua dementia

Dementia ni maradhi ambapo utendaji kazi wa ubongo wako una athiriwa na huenda ukaanza kusahau vitu ama uwezo wako wa kufanya uamuzi kuathiriwa. Unapo kaa kwa muda mrefu, akili yako huenda ikawa sawa na ya mtu anaye ugua maradhi haya. Pia, uko katika hatari ya kuugua maradhi ya moyo, kisukari, shinikizo la juu la damu na magonjwa mengine sugu. Una shauriwa kuhakikisha kuwa una songa siku yote na pia kufanya mazoezi mara kwa mara.

Kuumiza mtima wako

Kulingana na utafiti uliofanyika na wanasayansi, watu wanao keti kwa muda mrefu wako katika hatari ya kuugua matatizo ya moyo. Kati ya vikundi viwili, kimoja kilicho kaa kwa muda mrefu na kingine ambacho hawaku keti kwa muda mrefu, walio kaa kwa muda mrefu walikuwa na hatari mara mbili zaidi ya kuugua maradhi ya moyo.

Kuongeza uzito wa mwili

Watu wengi wanao kuwa na uzito mwingi wa mwili hawafanyi kazi nyingi. Huenda ikawa kuwa wanatumia muda wao mwingi wakitizama runinga. Kukaa mahali pamoja bila kuuhusisha mwili wao. Uko katika hatari ya kuwa na uzito wa kupindukia. Unaweza saidia kufanya kazi za nyumba, kufanya mazoezi mepesi ama hata kutembea kwa angalau dakika 20 ama 30 kwa siku.

Kuumwa na mgongo

Kuketi Chini Kwa Muda Mrefu Kuna Hatarisha Maisha Yako Kwa Njia Hizi

Kukaa chini kwa muda mrefu kuna maanisha kuwa mgongo wako umebaki mahali pamoja kwa muda mrefu. Na kushinikiza misuli ya mgongo, shingo na uti wa mgongo. Huenda ukapata kuwa una hisi maumivu ya mgongo. Ili kutatua suala hili, unaweza pigwa masi, kujinyoosha na kufanya mazoezi.

Soma Pia: Faida 4 Za Kiafya Za Kitunguu Saumu Kwa Wanaume

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Health
  • /
  • Kuketi Chini Kwa Muda Mrefu Kuna Hatarisha Maisha Yako Kwa Njia Hizi
Share:
  • Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

    Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

  • Dalili 4 Za Kukuonya Dhidi Ya Mshtuko Wa Moyo Kwa Wanawake

    Dalili 4 Za Kukuonya Dhidi Ya Mshtuko Wa Moyo Kwa Wanawake

  • Vyakula 8 Vitakavyo Msaidia Mtoto Wako Kuongeza Uzito Wa Mwili

    Vyakula 8 Vitakavyo Msaidia Mtoto Wako Kuongeza Uzito Wa Mwili

  • Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

    Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

  • Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

    Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

  • Dalili 4 Za Kukuonya Dhidi Ya Mshtuko Wa Moyo Kwa Wanawake

    Dalili 4 Za Kukuonya Dhidi Ya Mshtuko Wa Moyo Kwa Wanawake

  • Vyakula 8 Vitakavyo Msaidia Mtoto Wako Kuongeza Uzito Wa Mwili

    Vyakula 8 Vitakavyo Msaidia Mtoto Wako Kuongeza Uzito Wa Mwili

  • Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

    Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it