Bila shaka, simu zimeleta manufaa mengi maishai na kurahisha vitu vingi. Kwa njia sawa, zina madhara hasi hasa usipofahamu mipaka ya kutumia simu. Jambo ambalo limekuwa maarufu kwa watu wengi ni kutumia simu kwa muda mrefu. Kitu cha mwisho unachofanya kabla ya kulala ni kuangalia simu, na cha kwanza baada ya kuamka ni kuangalia simu kuona kilichotendeka usiku. Wataalum wanashauri dhidi ya kulala na simu kitandani. Unafahamu athari za kulala na simu kitandani? Tunaangazia jinsi mazoea ya kutumia simu kitandani yana athiri usingizi na maisha yako kwa jumla.
Athari za kulala na simu kitandani

Kuharibu ratiba ya kulala
Tofauti na siku za awali, simu imekuwa kifaa muhimu maishani. Inakuwezesha kutuma na kupokea jumbe kutoka kwa watu walio mbali nawe. Kutazama kinachoendelea sehemu tofauti duniani na pia kufanya kazi ukiwa mahali popote pale. Kutumia simu kitandani ama katika chumba cha kulala kuna athiri ratiba yako ya kulala. Mara nyingi utapata haja ya kuendelea kutumia simu hata baada ya wakati wako wa kulala kufika. Jambo linalosababisha kutatizika kulala ama ukosefu wa usingizi.
Mwangaza
Mwangaza kutoka kwa kifaa kile utafanya iwe vigumu kwako kupata usingizi. Viwango vidogo vya usingizi kutoka kwa simu huchelewesha usingizi. Watu wanaotumia simu dakika nyingi kabla ya kulala hutatizika kupata usingizi kwa kasi. Mwangaza huo huleta matatizo ya macho. Kutopata usingizi wa kutosha usiku kutafanya uamke muda baada masaa yako ya kawaida ya kuamka. Kutopata usingizi tosha huathiri utendakazi wako.
Kutoweka simu chumbani cha kulala kunashauriwa. Ni rahisi kujitenga na haja ya kuangalia simu mara kwa mara unapokosa usingizi ama unapoamka kati kati ya usiku.
Kuboresha ratiba yako ya kulala

Kwa watu wanaotatizika kulala kwa kasi ama kuchukua muda mrefu kabla ya kupata usingizi, kutumia simu chumbani cha kulala kunafanya iwe vigumu zaidi kulala.
Ondoa simu chumbani cha kulala
Unapoenda kulala, wacha simu yako sebuleni. Kwa njia hii, hutahisi haja ya kuangalia simu yako kila mara.
Tengeneza mazingira ya kulala
Uwezo wako wa kupata usingizi huathiriwa na mazingira ya kulala. Ili kupata usingizi kwa kasi, ni muhimu kuhakikisha kuwa chumba chako cha kulala kiko katika hali bora zaidi. Ni kisafi, hakuna mabaki ya chakula na unalalia shuka safi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Madhara Ya Kukosa Usingizi Na Wakati Wa Kumwona Daktari