Kulala Sana Kuna Athari Hasi Kwa Afya Yako

Kulala Sana Kuna Athari Hasi Kwa Afya Yako

Kila mtu huongea kuhusu kupata usingizi tosha, wakati ambapo hakuna jambo mbaya na kulala, utafiti mpya unaonyesha athari hasi za kulala sana

Kila mtu huongea kuhusu kupata usingizi tosha, wakati ambapo hakuna jambo mbaya na kulala, utafiti mpya unaonyesha athari hasi za kulala sana. Pia una eleza kinacho tendeka unapo lala sana.

Nini inatendeka unapo lala sana?

Somo hili lili lenga kuonyesha kinacho tendeka unapo lala sana.

Kulingana na utafiti ulio chapishwa kwenye Neurologu, kulala sana zaidi ya masaa tisa kwa mara moja na kulala kwa muda mrefu kuna ongeza nafasi zako za kuugua kiharusi. Utafiti huu uliangazia mtindo wa kulala kwa watu 31,750 katika Uchina kwa kipindi cha miaka sita. Pia, utafiti huu uliangalia mambo yanayo sababisha hatari ya kiharusi kama vile kuvuta sigara, kunywa pombe na historia ya kiharusi na matatizo mengine ya moyo.

Kati ya wahusika wa somo hili walio lala kwa zaidi ya masaa tisa walikuwa katika hatari ya asilimia 23 ya kupata kiharusi. Wakati ambapo walio lala kwa dakika zaidi ya 90 kati kati ya siku wali ripoti hatari ya asilimia 25 zaidi. Tena, kwa watu ambao mara nyingi hulala kwa masaa tisa mchana walikuwa na hatari asilimia 85.

"Sio vyema kulala kwa muda mdogo, na pia sio vyema kulala sana," alieleza Sheila Garland. Ambaye ni mwana saikolojia aliye sajiliwa na profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Memorial University katika Newfoundland.

Kuna maana gani unapo lala sana?

faida za kiafya za kulala mchana

Kufahamu kinacho maanisha huenda kukatatiza kwa sababu unapolala sana, huenda ikawa ishara ama chanzo. Kulala sana kunaweza kuletea matatizo ya kiafya na huenda kukawa ishara ya tatizo la kiafya ulilo nalo. Na kuifanya iwe vigumu kudhibitisha.

Sababu kwa nini huenda una lala sana ni kama vile:

Hypersomnia: Ikiwa una hypersomnia, ina maana kuwa una lala sana na unashuhudia hali ya kimatibabu. Hali hii ina sababisha kuhisi usingizi siku yote. Hata unapo kuwa umelala na unapo amka, bado unahisi haja ya kurudi kulala na uchovu hauja kuacha. Ikiwa jambo hili lina kutendekea, unapaswa kumwona daktari. Huenda circadian rhythm yako ikahitaji kuangaliwa.

Seasonal Affective Disorder: Hii ni aina nyingine ya kufilisika kimawazo inayo fuata mabadiliko ya msimu na kuwa kwenye mwanga. Ishara ni kama vile, kuchoka, kukosa matumaini na kulala sana.

Utumiaji mwingi wa vileo. Circadian rhythm ya mlevi mzito huenda ika athiriwa na unywaji mwingi wa vileo na kumfanya alale sana. Utumiaji wa mihadarati sana unaweza kuwa na athari hii.

Obstructive Sleep Apnea: Hali hii inatendeka wakati ambapo mfumo wako wa hewa una fungana unapo lala kwa sababu misuli ya koo imetulia. Na kukufanya uamke kwa ghafla kutoka usingizini, na kuathiri ubora wa usingizi unao pata.

Kugundua kwa nini mtu hapati usingizi tosha ama ana lala sana kunapaswa kufanyika kwa mitihani ya kifizikia na kisaikolojia.

Nini Inafanyika unapo lala sana: Athari hasi za kulala sana

Kulala Sana Kuna Athari Hasi Kwa Afya Yako

Usingizi ni mojawapo ya vitu muhimu sana ili kuwa na afya bora, pamoja na lishe bora na mazoezi, alisema Charles Morin. Ambaye ni mtafiti na profesa katika chuo kikuu cha Laval huko mji wa Quebec. Wakati ambapo Garland anasema kuwa usingizi mzuri una husisha vitu vitatu: "kulala kwa wakati tosha, ubora wa usingizi na kulala wakati unaofaa."

Kwa Morin, kinacho fanya usingizi uwe mzuri ni tofauti kwa kila mmoja wetu, lakini watu wazima wanapaswa kupata angalau masaa manane ya usingizi kila usiku. Morin anasema kuwa ni sawa kupata kiwango kidogo ama kingi zaidi lakini tofauti isiwe zaidi ya lisaa limoja. Kama anavyo shauri, kumwona daktari ikiwa unalala zaidi ya masaa kumi usiku na bado unahisi kuchoka.

Kulingana na Garland, kila mtu husikiza circadian rhythm yake, utendaji wa ubongo unao dhibiti mwili wako unacho fanya na homoni. "Inakuelezea unapo paswa kuwa umeamk na unapo faa kuwa umelala. Na ina athiri utoaji wa homoni. Kila seli ina saa inayo iambia izeme na iwake."

Jinsi ya kuepuka kulala sana

  • Tengeneza ratiba mpya na yenye starehe ya kulala na uizingatie
  • Epuka kunywa kaffeini kwa sababu itakufanya ukae kwa muda mrefu kabla ya kulala na uanze kulala sana
  • Kufanya mazoezi mara kwa mara kuna kusaidia kulala kwa kasi na kupata usingizi bora. Unapo pumzika vya kutosha usiku, hauta hitaji kulala sana
  • Epuka kulala sana kwa sababu ni wikendi. Kufanya hivi kuta fanya iwe vigumu kwako kupata usingizi wiki inayo fuata
  • Jaribu kuacha pazia za madirisha yako yakiwa wazi kabla ya kulala. Kwa njia hii utagundua kunapo kucha kwa sababu ya mwangaza
  • Usi sinzie baada ya saa kumi jioni, kwa sababu itakuwa vigumu kwako kupata usingizi usiku

Wakati wowote unapo anza kulala ghafla, huo ni mwili wako unakuongelesha. Ikiwa sio tatizo la kiafya, huenda ikawa ni ishara ya tatizo la kiafya. Hakikisha umemwona daktari.

Soma pia:Ulezi Wa Usiku Kwa Watoto: Mbadala Wa Kuwafunza Kulala Wakati Wa Usiku

Written by

Risper Nyakio