Kwa Nini Kupima Mimba Mapema Sana Hakushauriwi?

Kwa Nini Kupima Mimba Mapema Sana Hakushauriwi?

Nafasi kubwa ni kuwa kipimo ulicho kitumia kina dhihirisha usahihi wa hadi asilimia 99, lakini kuna uwezekano wa kuwa mjamzito kwa sababu ulifanya kipimo hicho mapema.

Kipimo chako cha kwanza cha nyumbani kina majibu hasi. Huenda ukawa na furaha; ama hata huzuni, lakini usirudie vileo na divai bado. Hata kama umetumia kipimo cha hivi majuzi cha kupima mimba kwenye simu kutumia teknolojia iliyo vumbuliwa hivi karibuni. Nafasi kubwa ni kuwa kipimo ulicho kitumia kina dhihirisha usahihi wa hadi asilimia 99, lakini kuna uwezekano wa kuwa mjamzito kufuatia kupima mimba mapema. Kupima mimba mapema kuna athari zipi?

Athari za kupima mimba mapema sana

chumvi kupima mimba

Huku sio kusema kuwa vipimo hivi haviwezi kuaminika ama kuna kasoro iliyo tukia, la. Lakini, nyingi kati ya vipimo hivi hukisia kugundua kuwepo kwa mimba mapema kiasi cha siku ya kwanza baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi. Kulingana na ripoti iliyo tolewa na The Journal of the American Medical Association, hiyo ni mapema sana kuwa na uhakika kuwa hauna mimba.

Vipimo vingi vilivyoko vina wahakikishia wanawake kuwa wanaweza pata majibu sahihi ya vipimo vyao siku ya kwanza baada ya kukosa kipindi cha hedhi. Unapo fanya kipimo mapema hivi, kipimo kitakuwa na majibu hasi. Na huenda mwanamke akarudia maisha ya kutumia vileo, uvutaji sigara ama hata kutumia dawa za kulevya. Zote ambazo zinaweza mwumiza mtoto anaye kua tumboni.

Utafiti uliofanywa na mtaalum Allen J. Wilcox ulidhihirisha kuwa kipimo kinapo fanywa mapema sana, bila shaka majibu yatakuwa hasi. Manufaa ya kupima mapema ni kama mwanamke aliye na mimba ako katika kiasi ambacho mimba inaweza dhihirika na atapata ujumbe utakao mfaa. Na athari hasi za kupima mapema ni kuwa huenda ukaamini majibu hasi na kurudia vitu ambavyo huenda vika athiri ukuaji wa fetusi.

Katika utafiti ulio ongozwa na Wilcox kwenye maabara huko Durham, watafiti walipima wanawake 136 walio panga kupata watoto. Walipo pima mwanamke siku ya kwanza aliyo tarajia kupata hedhi yake, kipimo kimoja kati ya vipimo kumi kilikuwa na majibu yasiyo sawa.

Hitimisho

pregnancy test with salt

Ni asili kwa mwanamke kutaka kujua hali yake ya mimba. Hasa kama umekuwa ukijaribu kutunga mimba kwa muda mrefu. Epuka kufanya kipimo cha nyumbani cha mimba mapema sana kwasababu nafasi kubwa ni kuwa matokeo hayatakuwa sahihi. Kumbuka kuwa matokeo ya sahihi yana dhihirika siku 14 baada ya kufanya ngono isiyo salama. Ikiwa ungependa matokeo kabla ya wakati huo, fanya kipimo cha damu kwenye maabara.

Usikuwe na kasi ya kurudia vileo baada ya kufanya kipimo cha mimba siku unayo tarajia hedhi ya mwezi. Hadi pale ambapo utapata matokeo sahihi kutoka kituo cha hospitali.

Chanzo: Webmd

Soma piaLishe Na Siha Ya Mama Mwenye Mimba: Vyakula Muhimu Katika Mimba

Written by

Risper Nyakio