Inapofika kwa kutoa mimba, huenda ukawa umesikia mbinu tofauti ikiwemo njia ya vidonge. Unafahamu athari za kutoa mimba kwa njia ya vidonge? Hata kama njia hii inatumika kwa sana, ina athari hasi kwa afya ya mwanadada. Tuna angazia athari hizi.
Iwapo mwanamke amepata mimba ambayo hakuwa amepangia, anapaswa kuwasiliana na mtaalum wa afya atakayemfanyia vipimo kisha kumshauri anachostahili kufanya.
Athari za kutoa mimba kutumia tembe

1.Maambukizi
Vidonge vya kutoa mimba visipofanya kazi kamilifu, mwanamke huwa katika hatari ya kupata maambukizi. Tishu za fetusi hubaki kwenye uterasi na zisipojulikana mapema vya kutosha, mwanamke huwa katika hatari ya kuugua maambukizi yanayo hatarisha maisha yake.
2. Kukosa matibabu
Matumizi ya vidonge hivi huwa rahisi, ambapo mwanamke anaweza kutumia akiwa nyumbani na kukamilisha bila ukaguzi wa mtaalum wa afya. Hata kama linaonekana kuwa jambo rahisi, ni utaratibu hatari wa kiafya. Mwanamke anaweza kuvuja damu zaidi na kukosa namna ya kupata matibabu ya kiafya ya dharura. Kuna nambari ya wanawake waliopoteza maisha kufuatia utaratibu huu.
3. Kutokwa na damu
Vidonge vya kutoa mimba husababisha kuvuja damu na maumivu makali ya upande wa chini wa tumbo. Mbali na kutokwa na damu kwa kawaida, kuvuja damu zaidi kunaweza fanyika. Kuvuja damu zaidi kunaweza sababisha kifo cha anayejaribu kutoa mimba.
4. Kusombwa na mawazo

Wanawake wengi husombwa na mawazo baada ya kupitia utaratibu wa kutoa mimba. Mhemko wa hisia, kuwa na wasiwasi, kuhuzunika na mawazo yasiyoisha. Mwanamke anaposhuhudia ishara hii, anapaswa kuwasiliana na mtaalum apate usaidizi.
Athari za kutoa mimba kwa njia ya vidonge ni nyingi hasa kama mwanamke anatumia vidonge hivi akiwa nyumbani bila usimamizi wa mtaalum. Anajiweka katika hatari ya kuvuja damu zaidi kunakoweza kumfanya apoteze maisha yake. Utaratibu huu unapaswa kufanyika kwenye kituo cha afya chini ya usimamizi wa daktari mwenye vyeti.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Kuinama Katika Ujauzito Kuna Athari Kwa Fetusi: Madhara Ya Kuinama Kwa Mjamzito