Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Athari Za Mitandao Ya Kijamii Kwa Ulezi: Jinsi Mitandao Inavyo Athiri Maoni Kuhusu Ulezi

3 min read
Athari Za Mitandao Ya Kijamii Kwa Ulezi: Jinsi Mitandao Inavyo Athiri Maoni Kuhusu UleziAthari Za Mitandao Ya Kijamii Kwa Ulezi: Jinsi Mitandao Inavyo Athiri Maoni Kuhusu Ulezi

Athari za mitandao ya kijamii kwa ulezi ni kama vile kubadili mawazo ya watu kuhusu jinsi ulezi unavyopaswa na kuwajulisha watu kila kitu.

Je, unakumbuka zama za kale ambapo ulezi ulikuwa rahisi zaidi? Wakati ambapo ulezi mwingi ulifanyika nyuma ya milango iliyofungwa, kando na ngumzo za mara kwa mara katika sherehe za kifamilia. Hakuna aliyefahamu jinsi familia yako ilivyokuwa? Hivi sasa, mambo yamebadilika kwa sana, kufuatia utumizi wa juu wa mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii imeathiri ulezi na haya ndiyo unayopaswa kuhusu athari hasi za mitandao ya kijamii kwa ulezi.

Mitandao imeathiri jinsi wazazi wengi wanavyo lea watoto wao kwa njia tofauti. Pia imeathiri mawazo ya watu kuhusu ulezi. Ni muhimu kukumbuka kuwa unayoyaona kwenye mtandao ni kiasi cha mambo ambayo watu wanataka kukuonyesha. Kuna mambo zaidi yanayo fanyika ambayo hawaonyeshani kwenye mitandao ya kijamii.

Athari za mitandao ya kijamii kwa ulezi

athari za mitandao ya kijamii kwa ulezi 

  1. Kumfanya mama akwazwe kimawazo

Mitandao huathiri ulezi kwa kuwafanya mama wahisi wanakwazwa kimawazo kujihusu. Wana waangalia mama wengine wakiweka picha na familia zao waki zuru sehemu tofauti za dunia pamoja na watoto na wachumba wao na kuonekana wako sawa. Wanawaangalia mama wengine wakionyesha mafanikio ya watoto wao na kuanza kujilinganisha.

Huenda wakaanza kushangaa kwa nini watoto wao wanachukua muda mrefu hivyo kutimiza hatua fulani maishani. Kujilinganisha na wanawake wanaojifungua kisha kurudi kwenye shepu yao ya hapo awali kwa kasi wiki chache baada ya kujifungua. Wanapojiangalia kwenye vioo, wanahisi vibaya kwani wameongeza uzani usiopungua.

Usichokifahamu ni kuwa kuna upande mwingine wa mambo. Kila mama unayefikiria kuwa maisha yake yako sawa, huenda akawa hulia kila usiku kabla ya kulala ama anatumia madawa ya kupunguza kukwazwa kimawazo. Sio rahisi kujua.

Mama anayezuru duniani kote huku akitabasamu na mahela yasiyo isha huenda akawa anajaribu kukabiliana na tatizo la mchumba kutoka nje. Hatuna habari.

Huenda wanawake hawa wakayaangalia maisha yako na kuyatamani. Sio rahisi kujua yote yanayo endelea maishani mwa watu. Usiamini kila kitu unacho kiona.

2. Kuwafanya mama wawe wenye hukumu nyingi

athari za mitandao ya kijamii kwa ulezi 

Kuna baadhi ya wamama ambao huenda wakaona kuwa hawana doa. Wanajifikiria kwa hali ya juu na kuamini kuwa hakuna anaye fanya ulezi kwa njia bora kuwaliko. Wanatumia mitandao ya kijamii kugombanisha mama wengine kwa wanachokifanya na kuwaambia wanachofikiria kila wanapopata nafasi. Wanasema wanachofikiria kwasababu kunawafanya wahisi vyema wanapokuwa na usemi. Kuwaona wanawake wengine wakihisi vibaya kujihusu kunawafanya wahisi vyema kujihusu.

Mbali na hayo, mitandao inawafanya mama wahisi kana kwamba wanashindana. Kujaribu kufanya bora kuliko mama mwingine. Ulezi sio mashindano na safari ya kila mtu huwa tofauti. Na kila mama ni bora kwa njia yake, usijaribu kuwa kama wazazi wengine, kumbuka kuwa watoto wako pia ni tofauti.

Soma Pia: Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Parenting
  • /
  • Athari Za Mitandao Ya Kijamii Kwa Ulezi: Jinsi Mitandao Inavyo Athiri Maoni Kuhusu Ulezi
Share:
  • Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

    Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

  • Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

    Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

  • Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

    Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

  • Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

    Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

  • Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

    Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

  • Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

    Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it