Kutumia Paracetamol Kulainisha Nyama Kuna Hatarisha Maisha Yako: Wataalum Waonya

Kutumia Paracetamol Kulainisha Nyama Kuna Hatarisha Maisha Yako: Wataalum Waonya

Wana Nigeria wamejulikana kwa kutumia paracetamol kwa muda mrefu katika mapishi yao. Paracetamol ni dawa zinazo saidia kupunguza maumivu. Ila, kwa wana Nigeria, dawa hii ni ya miujiza kwao, na hawawezi washukuru vya kutosha walio iibua. Naam, naelewa kwa sasa una maswali mengi. Kutaka kujua kwa nini dawa hii ina yaokoa maisha yao na kuwasaidia sana. Kwa muda mrefu, wamekuwa wakiitumia katika mapishi yao kwa kulainisha nyama na maharagwe. Makala haya yana angazia athari za paracetamol kwa afya inapo tumika kwa nyama.

Athari za paracetamol kwa afya

athari za paracetamol kwa afya

Hata baada ya kuonywa mara nyingi na The National Agency for Food and Drugs Administration and Control kuwa tembe hizi zinaweza sababisha maradhi sugu mwilini kama figo na mafua kuto fanya kazi.

Jisababu lao ni kuwa tembe za paracetamol zina wasaidia kulainisha maharagwe na nyama. Kwa njia hii, chakula chao kina iva upesi na wanaweza kupika vyakula vingine na kuwa uzia wateja wao. Tembe hizi zina patikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Tembe za paracetamol zinatumika kutibu uchungu na joto jingi. Ila zinapo pikwa, zina poteza uwezo wake wa kutuliza uchungu na kuwa na asidi nyingi inayo hatarisha maisha ya binadamu inapo kuliwa.

Kwa muda mrefu, uajenti huu umejitosa katika kufanya kampeni kwa wanafamilia na wanabiashara wanao uza chakula na kutumia tembe hizi kuwaelimisha kuhusu hatari za kuzitumia katika mapishi yao.

Lengo lao ni kuwajuza watu kuhusu madhara ambayo wanaweza pata. Pia, wana washauri watu waripoti kwa uajenti wao wanapo gundua kuwa mwanabiashara fulani anazidi kuzitumia kupika nyama.

Kulingana na professa Mojisola Adeyeye, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa uajenti huo, paracetamol ni kemikali inayo badilika wakati ambapo joto ni nyingi na kuwa paraminophino kisha benzoquin. Kemikali ambazo huharibu figo.

Kuepuka kutumia paracetamol kulainisha nyama, watu wana weza tumia njia mbadala za kutimiza lengo hili. Mbinu maarufu za kulainisha nyama ni kama vile:

Kutumia Paracetamol Kulainisha Nyama Kuna Hatarisha Maisha Yako: Wataalum Waonya

 

  • Kutumia chumvi, weka kiwango kisicho kingi kwa nyama dakika 30 kabla ya kuanza kupika
  • Kutumia papai kulainisha nyama
  • Kuchanganya siki na nyama isiwe ngumu
  • Kupika nyama na kitunguu saumu na tangawizi ina isaidia iwe laini
  • Kuchanganya nyama na sharubati ya ndimu ama vidai kabla ya kupika

Soma Pia:Jinsi Ya Kutengeneza Chakula Chenye Afya Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja

Written by

Risper Nyakio