Athari Za Dawa Ya Paracetamol Kwa Nyama Inapo Tumiwa Kuilainisha

Athari Za Dawa Ya Paracetamol Kwa Nyama Inapo Tumiwa Kuilainisha

Hatari za kutumia dawa ya paracetamol kwa viwango vikubwa, hasa katika mapishi yako.

Baada ya kuvumbuliwa kuwa paracetamol ina uwezo wa kulainisha nyama, watu wengi walianza kuitumia katika mapishi yao. Kutumia dawa hii katika mapishi kuliwasaidia kutumia muda mfupi katika mapishi yao. Inaaminika kuwa kutumia tembe hizi unapofika kuna kata muda ambao ungetumia kuchemsha nyama yako kabla ya kuikaanga. Kinacho ifanya iwe rahisi zaidi kutumia tembe hizi ni kuwa zinapatikana kwa urahisi na kwa bei ya chini. Watu ambao hutumia tembe za paracetamol katika mapishi yao walisema kuwa inasaidia kuyeyusha nyama na kuifanya iwe laini kwa muda wa dakika 10 ambao ni muda mchache sana wa kupika ikilinganishwa na mapishi ya kawaida.  Ila watu wanao zitumia chembe hizi hawaelewi athari za paracetamol kwa nyama inapo tumika kuilainisha.

 

athari ya paracetamol kwa nyama

Athari  za paracetamol kwa nyama: Athari hasi za tembe hizi

Hapo awali kulikuwa na shaka kuwa dawa za kupunguza uchungu mwilini kama vile aspirin na tembe zinginezo zili sababisha vidonda vya tumbo ama kuumwa na tumbo. Kwa sababu hii watu walikimbilia hiari zingine zilizo patikana kwa urahisi na ambazo hazikuwa na athari hasi mwilini. Watu walianza kutumia paracetamol walipo hisi maumivu ya aina yoyote mwilini bila hata kwenda hospitalini kubainisha chanzo cha maumivu yale.

Matumizi ya juu ya dawa hii iliwafanya wana sayansi kufanya utafiti zaidi kubainisha iwapo dawa hii ina athari hasi za muda mrefu kwa mwili wa watu wanao itumia vibaya.

Watu wengi walio na hoteli za nyama pia huenda walianguka kwa uraibu huu wa kupika nyama kwa kutumia paracetamol ili wawapakulie wateja wao bila kuwafanya wangoje muda mrefu. Ila watu hawa hawajui kuwa wana hatarisha maisha ya wateja wao. Kwani dawa hii inapo pashwa moto inapokuwa kwa chakula, uwezo wake wa kutuliza maumivu huisha. Na huwa na athari hasi hasa kwa mapafu na figo.

athari za paracetamol kwa nyama

Pia wanao tumia tembe hizi kutuliza maumivu mara kwa mara wako hatarini pia. Kunywa viwango vingi vya dawa hii vitaufanya mwili wako ukose kutulia unapo zikunywa kwa sababu ya uchungu.

Huenda ukajiuliza ni njia zipi mbadala unaweza tumia

  • Tumia kitunguu saumu na tangawizi unapo pika nyama yako ili iwe laini zaidi
  • Weka nyama yako kwa maji yaliyo kolea chumvi kwa angalau lisaa limoja kabla ya kupika ili kufanya nyama yako iwe laini. Usifanye hivi kila mara kwani chumvi nyingi ina athari hasi kwa mwili wako
  • Weka papai kwenye nyama yako kwa dakika 30 kabla ya kupika kwani ina uwezo wa kulainisha nyama yako
  • Pia, kukata nyama iwe vipande vidogo kabla ya kupika kutasaidia iwe laini na iive kwa haraka zaidi.

What happens to your body when you overdose on paracetamol?

Baada ya kuangazia athari za paracetamol kwa nyama, ni bayana kuwa zina athari hasi ikilinganishwa na chanya. Tafadhali epuka kutumia paracetamol kulainisha nyama yako ili kuhakikisha kuwa haugonjeki. Pia unapo hisi maumivu ya mwili, kabla ya kutumia dawa zozote zile, wasiliana na daktari wako ili akushauri dawa ambazo zitakufaa.

Soma Pia: Mahali bora zaidi kula brunch Nairobi

Written by

Risper Nyakio