Athari Hasi Za Pombe Kwa Fetusi: Yote Unayo Hitajika Kujua

Athari Hasi Za Pombe Kwa Fetusi: Yote Unayo Hitajika Kujua

Pombe ni chanzo kikubwa cha ulemavu katika watoto. Mama mjamzito anamhatarisha mtoto wake anapo lewa. Tazama athari zaidi za pombe kwa fetusi.

Mimba na pombe hazi andamani. Mama anapaswa kuwacha kunywa pombe anapo anza juhudi za kutunga mimba. Pombe ina athari hasi kwa fetusi na kunywa pombe ukiwa na mimba kuta athiri mtoto baada ya kuzaliwa. Mama anapo kunywa pombe na vileo vingine, vinapita kupitia kwa placenta na kumfikia mtoto. Athari hasi za pombe kwa fetusi ni kama vile kuathiri ubongo. Mbali na hayo, vileo husababisha taabu hizi:

Athari hasi za pombe kwa fetusi

Athari Hasi Za Pombe Kwa Fetusi: Yote Unayo Hitajika Kujua

 • Kujifungua mtoto aliyekufa. Wanawake wanao endelea kunywa pombe na kuvuta sigara katika trimesta ya pili wako katika hatari ya kujifungua mtoto aliye kufa.
 • Uchungu wa mimba usio komaa. Wamama wengi wanao tumia vileo wakiwa wajawazito huwa katika hatari ya kushuhudia uchungu wa uzazi mapema na kujifungua mapema. Watoto walio zaliwa kabla ya miezi tisa kufika huwa katika hatari ya kupata matatizo ya kiafya. Kama vile matatizo ya mafua ama shida za kupumua.
 • Ulemavu wa maumbile. Mama anaye lewa akiwa na mimba ana hatarisha mtoto aliye tumboni mwake na kumueka katika hatari ya kuzaliwa akiwa na ulemavu wa maumbile.
 • Kupoteza mimba. Kunywa vileo ukiwa na mimba kunaweza kufanya upoteze mimba katika trimesta ya kwanza.
 • Kuugua FASDs(Fetal alcohol spectrum disorders). Mtoto aliye na ugonjwa huu huathiri anavyo kaa, kufikiria na kusoma. Ugonjwa huu hudumu maishani mwake mote.

Mtoto aliye na FASDs huenda akawa na shida hizi:

 • Matatizo ya kukumbuka ama kupoteza uwezo wake wa kukumbuka
 • Kuwa na matatizo ya kusoma
 • Kukosa uwezo wa kuwa makini kwa jambo
 • Kuwa mfupi, mdogo kuliko wastani ama kuwa na uzani mdogo
 • Matatizo ya kuzungumza ama kuandamana na kutangamana na watu wengine
 • Kufanya uamuzi mbaya wa vitu

Fanya vitu hivi unapo pata mimba

mimba isiyo pangwa

 1. Koma kutumia vileo. Mama mwenye mimba ana shauriwa kuto tumia vileo, mara tu unapogundua ana ujauzito.
 2. Koma kutumia sigara. Sigara zina athari sawa na vileo, hakikisha kuwa ikiwa una uraibu wa kutumia sigara, umekoma unapo gundua kuwa una mimba.
 3. Wajulishe marafiki na familia yako unapo tunga mimba. Huenda uka alikwa na rafiki zako kwenye sherehe iliyo na vileo. Unapo wajulisha kuwa una mimba, wata kuwa makini na vinywaji wanavyo kupatia ili kuhakikisha kuwa hawatapita mipaka yako.
 4. Ondoa vileo nyumbani mwako. Ni vigumu kutokunywa ukiwa na vileo nyumbani mwako. Unapo tunga mimba, toa vileo vyote nyumbani mwako.

Afya yako ni muhimu sana unapo kuwa mjamzito. Kila kitu unacho fanya ama kunywa kita athiri mtoto aliye tumboni mwako. Hakikisha kuwa unakaa mbali na vileo katika kipindi hiki unapo kuwa na mimba. Ukitatizika kuwachana na pombe, zungumza na mtaalum wa afya unaye fanya kazi naye kipindi hiki na ata kushauri unacho paswa kufanya.

Soma Pia:Jinsi Ya Kujitayarisha Kuitwa Mama: Mambo Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Na Mimba

Written by

Risper Nyakio