Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Athari Hasi Za Kutumia Tembe Za Kupanga Uzazi

2 min read
Athari Hasi Za Kutumia Tembe Za Kupanga UzaziAthari Hasi Za Kutumia Tembe Za Kupanga Uzazi

Athari za tembe za uzazi wa mpango kwa wanawake ni kama vile kuumwa na kichwa mara kwa mara ama kushuhudia mhemko wa hisia.

Kuna njia tofauti za uzazi wa mpango, mojawapo ikiwa ni kutumia tembe za kupanga uzazi. Zinafanya kazi kwa kuepusha kupevuka kwa yai. Zinadhibiti kutolewa kwa yai, kwa hivyo manii hayawezi kurutubisha yai. Na hivyo basi, hakuna ujauzito unaofanyika. Manii kutoka kwa mwanamme yanapokutana na yai lililoachiliwa, yanalirutubisha, kisha linajipandikiza kwenye kuta za uterasi na ujauzito kufanyika. Hata hivyo, kuna athari za tembe za uzazi wa mpango kwa wanawake.

Tembe zote za kupanga uzazi huwa na vichocheo vya estrogen ama progestin ama vyote viwili. Vichocheo hivi vina jukumu la kuathiri mzunguko wa kiasili wa homoni mwilini na kuepusha ujauzito. Homoni zinadhibiti kupata vipindi vya hedhi na kupevuka kwa yai, pia, huenda zikadhibiti manii kuingia kwenye kizazi kwa kutoa kamasi ya uke. Tembe hizi pia zinaweza kudhibiti kupata mimba kwa kufanya kuta za uterasi kutoweza kupandikiza yai. Hata hivyo, tembe hizi zina athari hasi.

Athari hasi za kutumia tembe kupanga uzazi

Kuongeza uzani wa mwili

athari za tembe za uzazi wa mpango

Kuna uhusiano kati ya utumizi wa tembe za kupanga uzazi na mabadiliko ya uzani wa mwili, wanawake wengine huenda wakapoteza uzito, huku wengine wakiongeza. Kuongeza homoni mwilini huathiri utendaji kazi wa homoni zilizo mwilini na kuchangia katika mabadiliko mwilini.

Kichefuchefu

Mwanamke huenda akahisi kichefu chefu anapokuwa akitumia tembe za kudhibiti uzalishaji hasa katika siku za mwanzo. Njia ya kupunguza athari hii ni kwa kula kabla ya kuchukua tembe hizi unapoenda kulala. Wasiliana na daktari wako kichefu chefu kisipo pungua baada ya miezi mitatu.

Maumivu ya kichwa

kusombwa na mawazo baada ya kujifungua

Wanawake wengi wanaotumia uzazi wa mpango wa tembe wameripoti kushuhudia maumivu ya kichwa. Hasa tembe zilizo na viwango vya juu vya homoni. Maumivu haya hupungua baada ya muda, yasipo, wasiliana na daktari wako.

Mhemko wa hisia

Tembe hasa zilizo na homoni huathiri mhemko wa hisia na kumweka mwanamke katika hatari iliyo ongezeka ya kuugua fikira nyingi ama kuwa na hisia nyingi. Ni vyema kwa wanawake kuwasiliana na madaktari wao mara kwa mara. Hizi ni baadhi ya athari za tembe za uzazi wa mpango.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Njia Za Uzazi Wa Mpango Kwa Wanaume Na Athari Zake!

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Health
  • /
  • Athari Hasi Za Kutumia Tembe Za Kupanga Uzazi
Share:
  • Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

    Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

  • Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

    Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

  • Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

    Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

  • Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

    Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

  • Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

    Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

  • Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

    Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it