Kama mzazi, unazingatia mahitaji ya familia yako, watoto, bwana, bibi, nyumba na kuhakikisha kuwa mambo yote yako shwari. Wazazi wengi huwa makini na watoto wao na kusahau mahitaji yao na kujipa muda. Na kuwafanya wapate uchovu wa ulezi ambapo wanahisi kuwa wamechoka na hawana nishati ya kuendelea.
Wazazi wengi wanaposhuhudia jambo hili, wanafikiria kuwa ni kawaida katika ulezi. Na kuhisi lawama wanapotaka kuchukua muda wa kupumzika. Pia wana aibu ku wa wataonekana kuwa wao sio wazazi wazuri. Uchovu huu wa ulezi huwa na athari hasi kwenye afya ya kiakili, kihisia na hata kifizikia.
Athari za uchovu wa ulezi

Kuchoka katika ulezi humfanya mzazi kuhisi kuchoka wakati wote, kujitenga kihisia na watoto na mchumba, kuwa na lawama na kuhisi kuwa yeye sio mzazi bora. Athari ambazo zina athiri afya kwa ujumla. Mzazi huenda akahisi kuwa anatatizika kufikiria, kufanya uamuzi, kuhisi kuchanganyikiwa, kusombwa na mawazo, kusahau ovyo, kuhisi ako peke yake, ama hata kukosa usingizi.
Kwa wanawake, uchovu wa viwango vya juu huenda ukasababisha mabadiliko ya viwango vya homoni mwilini, kisukari, ugonjwa wa moyo, kukosa usingizi na kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
Uhusiano kati ya wachumba utaathiriwa. Ambapo kutakua na matatizo ya mazungumzo, kuto sikizana ama hata kuchukiana.
Mzazi anayetatizika na uchovu wa mzazi atahisi kuwa uhusiano wake na watoto umeathiriwa na kuhisi kuwa kuna umbali kati yao.
Kutatua suala hili
Mara nyingi, huenda mchumba asifahamu kinachoendelea. Kumweleza ni jambo la kwanza ili aweze kusaidia katika majukumu ya kinyumbani na kuwachunga watoto. Msaada wa kihisia ni muhimu kutatua hali hii. Usipomweleza mchumba wako unavyohisi, ni vigumu kwake kukusaidia ama kuelewa yanayokukumba.

Mazoezi huboresha utoaji wa vichocheo vya kuhisi vizuri mwilini, na kupunguza mawazo mengi na kusombwa na mawazo. Kufanya mazoezi kunaweza kuwa kuogelea kwa dakika chache kwa siku ama kutembea kwa dakika 20.
Jamii inawasingizia wanawake kuhisi lawama wanapowaacha watoto na kwenda likizo kupumzika. Ukweli ni kuwa, ulezi ni jukumu kubwa na sio jambo jipya mzazi wa kimsingi kuhisi kuwa anazidiwa na majukumu yote aliyotwikwa. Ni muhimu kuchukua mapumziko ya mara kwa mara.
Chanzo : WebMD
Soma Pia: Matatizo Ya Ulezi (Changamoto 3 Kuu Za Ulezi Katika 2021)