Mbinu za uzazi wa mpango hasa zenye homoni zinafahamika kuwa salama kwa watu wengi. Hata ingawa kuna baadhi zilizo na athari hasi kwa afya ya mwanamke. Je, kuna muda ambao mwanamke anaweza kutumia uzazi wa mpango bila matatizo ya kiafya? Je, athari za uzazi wa mpango ni zipi?
Kuna watu ambao wanachukua tembe za kudhibiti uzalishaji kwa muda mrefu bila kuchukua muda wa mapumziko. Tembe zilizo na vichocheo vya progesterone ama estrogen na huwa na athari mwilini. Usalama wa mbinu yoyote ile ya uzazi wa mpango inalingana na vitu kama vile umri, historia ya kiafya na kadhalika. Kuna athari za muda mfupi na mrefu za kutumia uzazi wa mpango.
Athari za muda mfupi za uzazi wa mpango

- kuvuja damu
- maumivu ya kichwa
- kuhisi kichefu chefu
- Kuvuja damu baada ya kipindi cha hedhi
- Ongezeko la uzito kwa kasi
- Mhemko wa hisia
Athari za muda mrefu za uzazi wa mpango

Kwa watu wengi, utumiaji wa uzazi wa mpango kwa muda mrefu hauna athari zozote hasi. Ila kuna baadhi ya wanawake wanao teseka kutokana na utumiaji wa mbinu za kupanga uzazi kwa muda mrefu. Hasa kwa wanao tumia mbinu zenye vichocheo. Kuna wanawake wanao shauriwa kutumia mbinu hizi za kupanga uzazi ili kudhibiti hali za kimatibabu za muda mrefu. Kama vile endometriosis.
Kulingana na utafiti uliofanyika na Shirika Kuu la Saratani, kuna utafiti unao dokeza kuwa mbinu za kupanga uzazi zenye vichocheo huenda vikaongeza hatari ya kuugua saratani ya kizazi na ya matiti.
Hata hivyo, utafiti huo huo una kisia kuwa huenda mbinu hizo zikapunguza hatari ya mwanamke kupata saratani ya ovari, na endometrial. Vichocheo vya progesterone na estrogen vilivyoko kwenye tembe hizi, huenda vika punguza ukuaji wa baadhi ya seli zinazo sababisha saratani, huku ziki ongeza ukuaji wa seli zingine.
Utafiti zaidi una sema kuwa watu walio tumia tembe wako katika hatari ya hadi zaidi mara mbili kuugua ugonjwa wa saratani ya matiti ikilinganishwa na wale ambao hawaja tumia.
Watu wengi wanaweza kutumia uzazi wa mpango kwa miaka mingi kwa usalama. Lakini ni vyema kuhakikisha kuwa daktari wako amekushauri. Huenda daktari wako akakushauri kutumia ama kuepuka mbinu zingine. Kwa mbinu za kupanga uzazi zilizo na homoni, huenda zikasababisha matatizo kulingana na historia ya kiafya na umri.
Soma pia : Vyakula Bora Kwa Afya Ya Mwanamme Ili Kuboresha Afya Ya Kiume