Cha Kufanya Ukigundua Kuwa Mdomo Wa Mtoto Wako Una Rangi Bluu

Cha Kufanya Ukigundua Kuwa Mdomo Wa Mtoto Wako Una Rangi Bluu

Kukosa hewa tosha mwilini huenda kukasababisha mtoto wako kuwa na rangi ya bluu.

Cyanosis, ama blue spells, ni wakati ambapo kiwango kidogo cha damu huingia kwenye mapafu ya mtoto. Kwa sababu damu hubeba hewa, kiasi kidogo cha damu huingia kwenye mwili. Kama tokeo, huenda mtoto wako akaonekana ana bluu. Rangi hii hutoka kwenye kiwango cha chini cha hewa karibu na ngozi. Haemoglobin hukubalisha seli nyekundu kubeba hewa. Haemoglobin yenye hewa huwa na rangi nyekundu iwapo isiyo na hewa huwa ya bluu. Na kufanya mtoto wako kuwa na rangi ya baby blue kwenye mdomo na mwili. Cyanosis ya hali za congenital heart huanza punde tu baada ya kuzaliwa. Baadhi ya wakati huwa haionekani hadi pale ambapo mtoto ana umri zaidi.

Baby Blue Kwenye Mdomo:Je, Ni Jambo La Dharura? baby blue kwenye mdomo

Iwapo rangi ya bluu iko sehemu ya mdomo wa mtoto tu, na sio kwenye sehemu zingine za uso, huenda ikawa sio tatizo kubwa. Kwa watoto walio na ngozi nyeusi, unaweza angalia ndani ya mdomo wake. Ukihusisha ufizi wake, iwapo una rangi isiyo nyingi. Ukigungua kuwa kuna sehemu yoyote ya mwili wa mtoto wako, hakikisha kuwa umeenda hospitalini kupata matibabu.

Ishara zaidi unazo paswa kuwa makini kuangalia:

Nini kinacho sababisha?

baby blue kwenye mdomo

Katika visa vingi, circumoral cyanosis ina aminika kuwa aina ya acrocyanosis. Acrocyanosis inatendeka pale ambapo mishipa midogo ya damu hupunguka kufuatia baridi. Hii ni kawaida sana kwa watoto wachanga katika siku za kwanza chache baada ya kuzaliwa. Cyanosis huenda ikamaanisha kuwa mafua hayana hayapitisha hewa tosha kwenye damu. Ama hakuna damu tosha iliyo na hewa inapita mwilini.

Kwa watoto wenye umri zaidi, circumoral cyanosis mara kwa mara unapotoka kukiwa na baridi ama unapotoka kuoga na maji moto. Aina hii ya cyanosis inapaswa kuisha unapo pata joto. Iwapo haiishi, hakikisha kuwa unamtembelea daktari wako. Circumoral cyanosis ambayo haiishi na joto huenda ikawa ishara ya matatizo makali ya mapafu ama moyo kama vile cyanotic congenital heart disease.

Baadhi ya watoto huwa na rangi ya bluee baada ya kupata baridi ama kuoga: hii si cyanosis.

Cyanosis ni kawaida:

 • Mtoto wako anapo lia kwa nguvu
 • Punde tu baada ya kuamka
 • Punde tu baada ya kunyonya
 • Muda mfupi baada ya mwendo wa tumbo
 • Mtoto wako anakosa maji tosha na anahitaji vinywaji

Sababu za central cyanosis

Central cyanosis ina vyanzo vingi, ikihusisha:

 • Matatizo ya kupumua na mapafu
 • Kasoro za roho zinazo kubalisha hewa humwaga damu kutoka upande wa kulia wa moyo kuichanganya na damu iliyo na wingi wa hewa kwenye upande wa kushoto wa moyo, ili damu inayo tolewa mwilini ina hewa ndogo
 • Matatizo na mzunguko wa damu ndani na kutoka nje ya mapafu kufuatia kutokuwa na kushikana kwema kwa mishipa ya damu kati ya moyo na mapafu ama kuzibwa kwa mishipa ya damu
 • Pulmonary edema- kujazwa na maji kwenye mapafu husababishwa na kukosa kufanya kazi kwa moyo
 • Changamoto za haemoglobin, yenye maana kuwa damu haibebi hewa tosha vizuri

Sababu za peripheral cyanosis

Peripheral cyanosis ina sababishwa na:

 • Temprecha baridi
 • Kulia kwa mtoto aliye zaliwa
 • Pindupindu ama mshtuko
 • Kushtuka miongoni mwa mambo mengine

Congenital heart defects zinazo sababisha cyanosis zina husisha kupitishwa kwa arteries, pulmonary atresia, tetralogy of Fallot, tricuspid atresia, hypoplastic left heart syndrome, truncus arteriosus, na interrupted aortic arch.

Kumsaidia mtoto wako iwapo ana cyanotic ama blue spell

baby blue around mouth

Iwapo mtoto wako ana cyanotic ama blue spell, usiwe na wasi wasi. umsaidia mtoto wako, fuata hatua hizi:

 • Mlaze mtoto wako kwa mgongo.
 • Leta magoti ya mtoto juu hadi kwenye kifua chake na uishikilie kwa nguvu katika nafasi hiyo. Pia unaweza fanya hivi ukiwa umemshika mtoto wako.
 • Mfariji na umlaze mtoto wako kwa upole huku umemkumbatia.
 • Baki mtulivu. Mtoto wako ana uwezo wa kujua iwapo umekasirika, na itakuwa vigumu zaidi kumlaza mtoto.

Circumoral cyanosis kwa watoto huisha bila matibabu yoyote. Kwa watoto wachanga, hii hutendeka siku chache baada ya kuzaliwa. Kwa watoto wenye umri zaidi, inapaswa kutendeka punde tu wanapo pata joto.

Walakini, ukigundua kuwa kuna ishara zozote zisizo za kawaida, hasa zinazo husiana na kupumua, ni vyema kupeleka mtoto wako kwa chumba cha dharura punde iwezekanavyo. Kuna uwezo mkuu kuwa daktari atasaidia kusawasisha mfumo wa pumzi, kupumua na mzunguko kabla ya kujaribu kujua chanzo chake.

 • Iwapo hii ni blue spell ya kwanza ya mtoto wako, mjulishe daktari wa mtoto wako.
 • Iwapo masafa ya blue spell ya mtoto wako huongezeka, mjulishe daktari wa mtima wa mtoto wako.
 • Iwapo blue spell hizi zinadumu zaidi ya dakika moja, mpeleka mtoto wako kwenye idara ya dharura iliyo karibu zaidi nawe.

Soma pia: Blue baby syndrome: A guide for parents

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio