Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Je, Nastihili Kupanga Nini Kwenye Mkoba Wa Kujifungua Ninapo Enda Hospitalini?

2 min read
Je, Nastihili Kupanga Nini Kwenye Mkoba Wa Kujifungua Ninapo Enda Hospitalini?Je, Nastihili Kupanga Nini Kwenye Mkoba Wa Kujifungua Ninapo Enda Hospitalini?

Wazazi wanashauriwa mara zote kuhakikisha kuwa begi la kujifungua mama anapoenda kujifungua uko sawa mwezi mmoja kabla ya siku kuu kuwadia.

Amina aliikata simu kisha kuiweka kwenye begi la kujifungua alilokuwa ameshika mkononi. Kisha akazama na kukaa kitako kwenye kiti chake spesheli kilicho mwezesha kuinyoosha miguu yake. Alikuwa katika hali ya kuhisi wasiwasi na kuwa na furaha. Baada ya miezi tisa iliyokuwa na mafunzo tele, na kumfungua katika dunia ya mambo mapya, siku kuu ilikuwa imewadia. Hata kama alikuwa na ujasiri kuwa kila kitu kilikuwa shwari, alikuwa na shaka kuwa huenda kuna vitu alivyosahau alipofanya ununuzi wa mahitaji ya mtoto. Mume wake alikuwa njiani yuwaja kumpeleka kwenye kituo cha afya walichokichagua cha kujifungua.

Mwezi huu wa mwisho ulijazwa na panda shuka tele. Kutoka kutatizika kulala vyema usiku, kuumwa na miguu hadi kwa kuhisi amechoshwa na safari hii ya ujauzito. Alimtamani kumpakata binti yake mikononi. Tayari alikuwa ameenda scan na kuvumbuliwa jinsia ya mtoto aliyemtarajia. Ila siku ilipowadia, alihisi kuwa anashaka, pamoja na hadithi zinazosambaa kuhusu uchungu wa uzazi. Hakuwa na uhakika kuwa alikuwa tayari. Je, itakuwa vipi iwapo kuna vitu vya mtoto nilivyo sahau kuvinunua? Tuna angazia mkoba wa kujifungua unapaswa kuwa na nini?

Begi la kujifungua

begi la kujifungua

Begi la hospitali linapaswa kuwa na vitu hivi:

  • Taulo za uzazi za kike ama pedi za maternity
  • Kitita cha pamba
  • Mavazi ya mtoto (sweta, suruali na vesti)
  • Nyembe ama surgical blades
  • Nyuzi za kushona
  • Dawa za kupunguza uchungu
  • Mpira wa mikono ama gloves za surgical
  • Blanketi ndogo ya mtoto

Vitu muhimu kwa mama

begi la kujifungua

  • Vazi pana kama vile dera lisilo mbana. Atakalo valia anapokuwa hospitalini anapokuwa na uchungu wa uzazi. Na baada ya kujifungua.
  • Soksi na sweta za dhidi ya baridi wakati wa usiku.
  • Mafuta ya kujipaka, yasiyo kuwa na harufu kali.
  • Vibanio vya kushika nywele iwapo mama ana nywele.

Ni muhimu kwa mama kubeba vinywaji laini na vitafunio vya siku kabla ya kujifungua. Anayempeleka hospitalini anastahili kuhakikisha ana beba mavazi zaidi ya kubadilisha huko anapomngoja mama mjamzito kujifungua. Chaja ya simu pamoja na jarida ama kitabu cha kusoma kupitisha muda. Iwapo wazazi wangependa kuchukua picha za mtoto mdogo angali siku moja, ni vyema kuiweka kamera kwenye mkoba wenu.

Wazazi wanashauriwa mara zote kuhakikisha kuwa begi la kujifungua mama anapoenda kujifungua uko sawa mwezi mmoja kabla ya siku kuu kuwadia. Kwa kufanya hivi, wana uhakika kuwa hakuna kitu muhimu kilicho sahaulika. Na iwapo kuna baadhi ya vitu vilivyo sahaulika, wana muda tosha wa kuvichukua.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Hali Ya Anemia Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kuitatua

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Becoming a Mama
  • /
  • Je, Nastihili Kupanga Nini Kwenye Mkoba Wa Kujifungua Ninapo Enda Hospitalini?
Share:
  • Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

    Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

  • Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

    Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

  • Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

    Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

  • Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

    Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

  • Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

    Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

  • Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

    Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it