Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Begi La Mama La Kujifungua Linapaswa Kuwa Na Vitu Hivi!

2 min read
Begi La Mama La Kujifungua Linapaswa Kuwa Na Vitu Hivi!Begi La Mama La Kujifungua Linapaswa Kuwa Na Vitu Hivi!

Ni wakati wako kuanza kutayarisha virago utakavyo beba unapo elekea hospitalini kujifungua. Kumbuka kuwa, ni vyema kupanga vitu hivi wakati kabla ya uchungu wako wa uzazi kukaribia. Unapo ngoja hadi dakika ya mwisho, huenda ukasahau kubeba vitu vingine unapo kuwa katika pilka pilka za kukusanya virago ukitoka kwenye nyumba. Kuna vitu muhimu vinavyo hitajika kuwa kwenye begi la mama la kujifungua. 

Ni vyema kwa wanandoa kuhakikisha kuwa vitu vyote viko tayari miezi miwili kabla ya siku wanayo tarajia mtoto wao. Hakikisha kuwa pesa ziko tayari za kulipa hospitalini, gari ya kumpeleka mama hospitalini uchungu wa uzazi unapo anza na begi ya mama ina kila kitu kinacho hitajika.

Begi la mama la kujifungua linapaswa kuwa na nini?

begi la mama la kujifungua

  • Bomba la sindano
  • Kitita cha pamba
  • Nyembe za kupasulia
  • Dawa za kupunguza uchungu
  • Taulo la kike la uzazi (pedi za maternity)
  • Mpira wa mkono (surgical gloves)
  • Nguo mpya za mtoto zilizo safishwa
  • Kibana kitovu (umbilical cord clamp)

Kwa mama, ni vyema kujihami na vitu vitakavyo msaidia kuwa na starehe anapo kuwa hospitalini akingoja kujifungua na siku chache baada ya kujifungua.

Hakikisha kuwa mkoba wako wa mama una vitu hivi

  • Dera ama rinda lisilo kubana. Wakati huu, unapo hesabu siku ama dakika chache kabla ya kumpakata mwanao mikononi mwako, haungependa kuwa na mavazi yanayo kubana kwa sana. Dera litakusaidia kuzunguka kwenye korido za kituo cha afya kwa urahisi. Hakikisha una mavazi mawili ya aina hii.
  • Soksi. Hizi zinakulinda dhidi ya baridi wakati wa usiku na unapolala.
  • Kitabu cha kusoma. Ni vyema kujiweka na shughuli za kufanya. Ikiwa wewe ni msomi, usipitishe nafasi ya kusoma jambo jipya kila siku.
  • Mafuta ya kupiga masi. Kufuatia uchungu unao zidi kuhisi katika siku hizi chache za mwisho, ni vyema kubeba mafuta ya kupiga masi ili mchumba wako ama marafiki wako wakupatia masi katika kipindi hiki.
  • Vitafunio ama vitamu tamu. Kuwa na kitu cha kula mara kwa mara kutakusaidia kutoa mawazo yako kwenye uchungu utakao hisi. Pia, hakikisha kuwa una vinywaji vinavyo kuongeza nguvu.
  • Mito. Ni muhimu sana kwa mama ili kupunguza uchungu unao hisi ama kukosa starehe unapo lala kwa upande mmoja.
  • Vibanio vya nywele

begi la mama la kujifungua

Ikiwa mama atapelekwa hospitalini na mchumba wake ama rafiki, ni vyema kuhakikisha kuwa wao pia wamejihami na vitu watakavyo vihitaji.

Vitu kama vile:

  • Simu
  • Chaja ya simu
  • Nguo za kubadilisha
  • Kitabu cha kusoma
  • Vitafunio na kinywaji

Chanzo: healthline

Soma Pia:Manufaa Ya Tendo La Ndoa Kwa Mama Mjamzito!

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Becoming a Mama
  • /
  • Begi La Mama La Kujifungua Linapaswa Kuwa Na Vitu Hivi!
Share:
  • Tumbo La Mama Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kulipunguza!

    Tumbo La Mama Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kulipunguza!

  • Matayarisho Ya Mwisho Kabla Ya Mama Kujifungua

    Matayarisho Ya Mwisho Kabla Ya Mama Kujifungua

  • Yote Unayo Hitajika Kujua Kuhusu Utunzaji Baada Ya Kujifungua

    Yote Unayo Hitajika Kujua Kuhusu Utunzaji Baada Ya Kujifungua

  • Jinsi Ya Kuboresha Lishe Na Siha Kwa Mama Mjamzito

    Jinsi Ya Kuboresha Lishe Na Siha Kwa Mama Mjamzito

  • Tumbo La Mama Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kulipunguza!

    Tumbo La Mama Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kulipunguza!

  • Matayarisho Ya Mwisho Kabla Ya Mama Kujifungua

    Matayarisho Ya Mwisho Kabla Ya Mama Kujifungua

  • Yote Unayo Hitajika Kujua Kuhusu Utunzaji Baada Ya Kujifungua

    Yote Unayo Hitajika Kujua Kuhusu Utunzaji Baada Ya Kujifungua

  • Jinsi Ya Kuboresha Lishe Na Siha Kwa Mama Mjamzito

    Jinsi Ya Kuboresha Lishe Na Siha Kwa Mama Mjamzito

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it