Vitu Muhimu Vya Kununua Kabla Ya Kujifungua

Vitu Muhimu Vya Kununua Kabla Ya Kujifungua

Pamba na wembe ni baadhi ya vitu ambavyo mama anapaswa kubeba anapo enda kujifungua.

Vitu vinavyo paswa kuwa kwa begi ama mkoba wa kujifungua ni kama nini? Safari ya mimba ni mojawapo ya vipindi katika maisha vinavyo kuwa vya kusisimua na vyenye furaha zaidi. Ila, mambo yote sio rahisi inavyo onekana, kuna changamoto nyingi ambazo wazazi watarajia hukumbana nazo. Miongoni mwa hivi ni kichefu chefu na hata ugonjwa wa asubuhi. Kuna vitu vingi ambavyo unapaswa kupanga kwenye begi yako ya kujifungua kabla ya siku kuwadia. Unapaswa kuhakikisha kuwa kadi yako ya hospitali ina fanya kazi. Chagua hospitali ambayo ungependa kujifungua na kisha ujue gharama yake kwa kujifungua kwa kawaida ama kupitia upasuaji. Hakikisha kuwa una pesa za kutosha kabla wakati huo kufika.

begi ya kujifungua

Begi ya kujifungua inapaswa kuwa na:

Yote hayo yakiwa sawa, ni wakati wa kuhakikisha kuwa begi yako ina vitu utakavyo hitaji hospitalini. Mama mjamzito hushauriwa aanze kufanya ununuzi wa nguo za mtoto anapokuwa katika trimesta yake ya kwanza ama ya pili kwani huenda akakosa wasaa ama akawa katika uchungu mwingi anapokuwa kwa trimesta yake ya tatu na kumzuia kununua vitu vya mtoto. Vitu kama vile nguo za mtoto na fulana zake. Unapo anza kununua mavazi ya mtoto kabla ya kufanya ultrasound kudhibitisha jinsia yake, unashauriwa kununua nguo zinazo faa jinsia zote mbili na kwa rangi zilizo tulia kama vile nyeupe, nyeusi, ama grey. Hii ni kwa sababu rangi hizi zina tambulika na jinsia zote mbili na hakuna inayo husishwa na jinsia moja kama vile bluu huwa ya wavulana na pinki ya wasichana.

Vitu vya kununua kwa ajili ya uchungu

 • Taulo ya uzazi ya kike (maternity pad)
 • Mipira ya mikono (surgical gloves)
 • Nguo za mtoto
 • Pamba kubwa laini
 • Wembe wa kupasulia (surgical blades)
 • Nyuzi za kushonea
 • Bomba la sindano
 • Dawa ya kupunguza uchungu
 • Vibana kitovu (umbilical cord clamp)

begi ya kujifungua

Mbali na hizo, ni muhimu kuwa na vitu vifaavyo kwa begi ya kujifungua. 

 • Nguo za mtoto kama nne
 • Blanketi ya mtoto
 • Taulo ndogo za kumpanguzia mtoto
 • Gauni utakalo valia kabla ya kwenda kwa chumba cha kujifungua na nyingine ya kuvalia baada ya kujifungua na kuoga.
 • Malapa yaliyo rahisi kuvalia na kuvua
 • Mafuta ya kukanda mwili kupunguza uchungu
 • Ni vyema kumwuliza mwenzi wako ama mojawapo ya wanafamilia ama rafiki unaye mwamini akupeleke hospitalini unapo enda kujifungua. Unapata ujasiri kwani unajua hauko peke yako, pia wanakusaidia kuto kuwa na fikira nyingi unapo ngoja kujifungua.

begi ya kujifungua

Vitu ambavyo mwenzi ama rafiki yako anapaswa kubeba

 • Viatu vyepesi vya kuvaa aina mbili
 • Soksi iwapo kutakuwa na baridi usiku
 • Simu na chaja
 • Nguo za kubadilisha
 • Pia anaweza beba vitamu tamu
 • Kamera ya digitali ama simu yenye kamera nzuri iwapo ungependa kuwa na kumbukumbu za siku hiyo.

Soma Pia: Jinsi Ya Kuchagua Hospitali Ya Kujifungua

Written by

Risper Nyakio