Je, Kupima Mimba Ni Bei Ghali Ama Rahisi?

Je, Kupima Mimba Ni Bei Ghali Ama Rahisi?

Muda wa kupima mimba hutofautiana kati ya mwanamke. Hii ni kwa sababu mizunguko ya hedhi hutofautiana kwa wanawake.

Ujauzito huwa jambo la furaha sana kwa wengi, ilihali kwa wengine huwa jambo la kutamausha. Ili kuwa na uhakika juu ya hali yako, ni vyema kuzingatia kipimo cha mimba. Kuna vipimo tofauti vya ujauzito  na pia bei ya kipimo cha mimba hutofautiana kutoka kipimo kimoja hadi kingine. Vingine havina gharama yoyote.

La kwanza, ni kuelewa kipimo cha mimba hufanya nini haswa? Baada ya yai lilorutubishwa kujipandikiza kwenye ukuta wa uterasi, huwa kuna  ongezeko la kichocheo cha hCG(human chorionic gonadotropin) mwilini. Hiki kichocheo/homoni  hutengenezwa mwilini baada ya siku sita baada ya yai kurutubishwa. Hiki kichocheo kinaweza patikana kwenye damu au mkojo.

bei ya kipimo cha mimba

Hivyo, kuna vipimo viwili maarufu vinavyotumika kutambua iwapo mwanamke ni mjamzito. Kipimo cha damu na mkojo.

  • Kipimo cha damu

Hiki kipimo kinahitaji daktari na maabara. Hakina uzoefu sana kwani gharama yake iko juu ikilinganishwa na vipimo vingine. Hiki kipimo huonyesha ongezeko la  kichocheo cha hCG kwenye damu. Iwapo kuna hCG mwilini humaanisha  una ujauzito.  Kina uwezo wa kuonyesha ongezeko ndogo  sana la hCG.  Hivi huwa bora kutambua ujauzito ata baada ya siku chache.  Pia hiki kipimo cha mimba kina uhakika wa zaidi ya asilimia 99.

  • Kipimo cha mkojo

Hiki kipimo chaweza kufanyika nyumbani  au kwenye maabara. Kipimo hiki cha ujauzito ni cha urahisi na gharama yake iko chini. Hupima kiwango cha homoni ya hCG kwenye mkojo. Kupima ujauzito nyumbani itabidi umenunua stripu (pregnancy test) kwenye duka la dawa. Ukitumia hii stripu unaweza kupima mimba kwa njia mbili:

  1. Weka mkojo kwenye chombo safi kisicho na mafuta ama kemikali yoyote. Hii huzuia kuharibika kwa matokeo. Kisha weka sehemu ya kupimia ndani ya chombo na ufuate maelezo.
  2. Weka sehemu ya kupima kwenye mtiririko unapokojoa ili ilowe. Baada ya vipimo hivi subiri kwa dakika chache ili kupata matokeo.

Majibu hutokea kwa kuonyesha mistari miwili yenye rangi ama alama chanya au hasi. Mifumo ya kidigitali huonyesha ujauzito ama hakuna ujauzito. Wakati mwingine kipimo hutoa majibu chanya. Hili linaweza kusababishwa na mambo kadhaa. Lakini baada ya vipimo viwili bado majibu ikitokea chanya, ni vizuri kutembelea daktari ili vipimo zaidi kufanyika.

Mambo ya kuzingatia unapopima mimba

bei ya kipimo cha mimba

Kujua ni wakati upi mwafaka wa kupima mimba ni muhimu. Wengi hukimbilia kupima siku ifuataye ilihali ata vipimo vya kisasa zaidi huwezi kupata majibu sahihi kwa muda mfupi  hivyo. Wakati mwafaka wa kupima kwa uhakika ni pale mwanamke anakosa kipindi chake cha hedhi. Huu wakati kichocheo cha HCG huwa juu zaidi. Muda wa kupima mimba hutofautiana kati ya mwanamke. Hii ni kwa sababu mizunguko ya hedhi hutofautiana, wengine wana mirefu na wengine mifupi. Yai la mwanamke linaporutubishwa huchukua takriban siku saba mpaka siku kumi kujipandikiza  kwenye ukuta wa uterasi. Baada ya hapo, siku mbili au tatu ili mimba iweze kusoma. Kwa hivyo, kwa ujumla inaweza kuchukua kati ya siku 14 hadi 21 kujua kwa uhakika kama una ujauzito.

Pia wakati mwafaka kwenye siku ni asubuhi pale ile homoni inaonekana vizuri. Bei ya kipimo cha mimba hutegemea ubora wa kipimo. Kipimo cha damu ni uhakika zaidi ya asilimia 99 na kile cha mkojo ni asilimia 99.

Soma Pia: Sababu Zinazo Sababisha Mama Kupata Mimba Ya Mtoto Zaidi Ya Mmoja

Written by

Risper Nyakio