Mahali Bora Zaidi Kula Brunch Nairobi

Mahali Bora Zaidi Kula Brunch Nairobi

Brunch in Nairobi! Chakula hiki kimekuwa kawaida sana hasa kwa watu wanao ishi Nairobi. Haijatambulika kilipo anzia kuwa kawaida ila cha muhimu ni kuwa kinasaidia sana. Iwapo umetoka kujivinjari usiku wote na ukaingia kwa nyumba usiku, chakula hiki ni bora kwako. Kina chukuliwa kwa kawaida baada ya masaa ya kiamsha kinywa kupita na kabla ya masaa ya chakula cha mchana.

Tuna angazia hoteli zinazo julikana kuwa na brunch bora zaidi Nairobi. Jiunge nasi kugundua mahali utakapo enda wikendi inayo fuata!

brunch in nairobi

  1. Artecaffe

Hoteli hii ina chakula cha kupendeza na inasifika kwa sana. Ikiandamana na kikombe cha kahawa chenye harufu ya kukuvuta kutoka kitandani mwako. Hapa ni pahali bora zaidi pa kutembelea na kukifurahikia chakula chako. Artecaffe ina hoteli katika sehemu tofauti mjini kama vile Westgate Mall, Oval Centre, Lavington, Capital Centre na Junction Mall.

Masaa yao ya kazi ni: 7.30 am- 12.00 am

Nambari za mawasiliano: 0709 202 024/ 0706 555 555

  1. Baluba at Ovenpick

Wana chakula cha kupendeza kutoka sehemu tofauti za dunia. Una jivinjari kwa kula chakula kitamu zaidi kinacho pikwa ukitazama. Wanatumia viungo kutoka pande tofauti za nchi kuhakikisha kuwa unaifurahia mapishi yao na chakula chao. Hakikisha kuwa unawatembelea kuona chakula tofauti wanazo tayarisha. Wanapatikana sehemu tofauti kama vile Westlands na Mkungu Close.

Masaa yao ya kazi: 6:30 am-10:30 am, 12 pm- 3pm, 6 pm- 10:30 pm

Nambari zao: 0709 548 000

  1. Larder at Raddison Blu

Wana chakula cha aina nyingi kutoka kwa sushi, salad, tacos na  sangria. Utakipenda chakula zaidi hasa ukienda na kikundi chako cha marafiki ili mjaribu vyakula tofauti walivyo navyo.  Kitu cha kupendeza zaidi ni kuwa kuna nafasi tosha watoto kucheza na kukimbia baada ya kula. Wana patika Upperhill  na Elgon Road.

Masaa yao ya kazi: 6.30 am- 8.00pm

Nambari zao: 0748 590 481

Mahali Bora Zaidi Kula Brunch Nairobi

  1. Shamba Caffe

Pahali pa kupendeza zaidi palipo jificha na penye utulivu. Kuhakikisha kuwa una furahia wakati wa kipekee. Wana pahala pa moto ambapo mna zunguka wakati wa usiku kupata joto mkiendelea na kuunywa mvinyo wenu. Wanapatikana upande wa Loresho Ridge Nairobi.

Masaa yao ya kazi: 9.00 am-10.00 pm

Nambari zao: 0740 345 168

  1. About Thyme

Ina mazingara yaliyo tulia na inapatikana sehemu za Westlands.  Wanakitengeneza chakula tofauti kutoka sehemu mbali mbali nchini na sehemu zinginezo duniani kote. Wana chakula cha bei isiyo ghali kwa mwananchi wa kawaida. Wanapatikana Eldama Ravine Rd.

Masaa yao ya kazi ni: 10.00 am- 3.00pm

brunch in nairobi

Picha kulingana na mums village

  1. Mercado Mexican Kitchen and Bar

Inajulikana kwa tacos na margaritas za kupendeza na kwa ujumla chakula cha kupendeza cha kimexico. Jitayarishe kukisherehekea chakula cha kutamanisha kutoka Mexico.  Wana patikana Terrace (T) Floor, South Wing, Kenrail Towers, Ring Road Parklands, Westlands area.

Masaa yao ya kazi: 10.00 am- 3.30 pm

Nambari zao: 0700 245 795

Vyanzo: yummy.co.ke  na mumsvillage

Written by

Risper Nyakio